tuwasiliane

Friday, December 30, 2011

30 DEC.BREAKING NEWS, Mpiganaji John Ngahyoma afariki dunia


Mpiganaji John Ngahyoma afariki dunia

HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.

HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.

MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.

HIVYO TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI TUTAKAVYOKUWA TUNAZIPATA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA TAARIFA HIZI ZA MSIBA WA MPIGANAJI WA SIKU NYINGI KATIKA TASNIA HII YA HABARI,BW. JOHN NGAHYOMA NA INATOA POLE KWA NDUGU WOTE WA MAREHEMU NA TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONJI.

TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.

30 DEC.HAPPY NEW YEAR WADAU WA BLOG HII


NAWATAKIA HAPPY NEW YEAR WADAU OTE MNAONIPA SUPPORT KUITEMBELEA BLOG YANGU,NAWAAHIDI MAMBO MAKUBWA ZAIDI MWAKA UJAO,KWAKUWA KUTAKUWA NA UDHAMINI,PIA MARIPOTA MBALIMBALI WAMEAHIDI KUFANYA KAZI NA BLOG HII AHSANTENI

30 DEC.SIMBA KUJIBIMA MBAVU LEO

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam leo inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Kutokana na hali hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kesho kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, ambapo timu yao itakuwa ikicheza mechi hiyo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa timu yake ipo imara kwa mchezo huo na wana matumaini makubwa watafanya vizuri.

“Pambano hilo litakuwa la mwisho kwa Simba kucheza jijini Dar es Salaam mwaka huu. Pambano hilo pia litakuwa la mwisho kwa Simba kabla haijaenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopangwa kuanza Januari 2 mwakani, “ alisema Kamwaga na kuongeza kuwa Simba itaenda Zanzibar Jumapili.

“Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic, kukaa kwenye benchi la ufundi na kuiongoza timu yake hiyo ambayo ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

“Profesa Cirkovic ameahidi kwamba kwenye pambano hilo atashusha kikosi kamili cha wachezaji wa Simba ili kubaini ni kwa namna gani wachezaji wake wameyaelewa mafunzo yake.

Nawakaribisha wapenzi na wanachama wa Simba na wapenda soka kwa ujumla waje kwa wingi kuiona Simba ikicheza.

Nimesikia kwamba Uwanja wa Azam ni mzuri na utaendana na aina ya mchezo ambao Simba itakuwa ikiucheza chini yangu. Nataka kuonesha soka la asili la Simba,” alisema Kamwaga akimnukuu kocha huyo.

30 DEC.WACHEZAJI YANGA WAANZA KUPEWA CHAO


WACHEZAJI wa Yanga ya Dar es Salaam ambao hawajalipwa mshahara wao wa miezi miwili
wameanza kulipwa kwa awamu.

Habari zilizopatikana jana kutoka kwa baadhi ya wachezaji hao na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa Yanga, Luious Sendeu ni kuwa wameanza kulipwa fedha zao, ingawa si zote.

“Kuna baadhi ya wachezaji tumelipwa leo, lakini hatujalipwa fedha zote ni mshahara wa mwezi mmoja. “Ilikuwa tukatae lakini kwa sababu ya hali ngumu tumekubali, ila mambo bado si mazuri,” alisema mmoja kati ya wachezaji mahiri wa timu hiyo.

Naye mchezaji mwingine alimpongeza Kocha Mkuu wa timu hiyo Kostadin Papic kwa kuwa mkweli na kwamba bila yeye pengine hali ingezidi kuwa mbaya kwao.

“Papic ndiye mkombozi wa wachezaji Yanga, ingawa tumelipwa kidogo, lakini bila yeye hata hichi tusingepata,” alisema mchezaji huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake.

Jumatatu wiki hii, Papic alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuushutumu uongozi kutokana na hali mbaya ya kifedha inayowakabili wachezaji wake, huku naye akilalamikia
nyumba anayoishi kukatiwa umeme na kukosa huduma ya maji.

Kutokana na hali hiyo alisema imeathiri mazoezi ya timu hiyo jambo ambalo ni la hatari kwa maandalizi ya michuano ya kimataifa, ambapo Yanga itacheza na Zamalek Februari mwakani.

Papic alienda mbali zaidi na kudai viongozi wamekuwa hawampi ushirikiano na kila anapowapigia simu hawapokei.

Lakini akizungumza jana Sendeu alisema suala la mambo ya mshahara uongozi unashughulikia na kwamba wameanza kulipwa hivyo hakuna tatizo.

“Hawajalipwa zote, lakini kiasi fulani tayari wamepokea kwa kuanzia, mambo mengine ukimpata Katibu Mkuu yeye atazungumza, ila ninachokuthibitishia ni kwamba tayari wameanza kulipwa,” alisema Sendeu.

Thursday, December 29, 2011

29 DEC. MTANZANIA ACHUKUA NAFASI YA TANO KTK SHINDANO LA MISS TOURISM INTERNATIONAL


MTANZANIA Nelly Kamwelu ameshika nafasi ya tano katika shindano la Miss Tourism Queen International 2011/12, lililofanyika katika mji wa Xian, nchini China.

Kamwelu alikuwa akiiwakilisha Tanzania katika shindano hilo baada ya kuibuka mshindi wa Miss Universe Tanzania mwaka huu.

Nelly ameshika nafasi hiyo mbele ya warembo wengine 92 katika shindano hilo ambalo ni la 5 kwa ukubwa duniani linalohusu mamiss.

Taji hilo la Miss Tourism Queen International, lilichukuliwa na mrembo wa kutoka nchini Thailand.

Nelly anatarajiwa kurejea nchini leo kwa ndege ya shirika la Emirates.

29 DEC. Dalili 4 za mwanaume aliye tayari kwa maisha ya ndoa!


atumaini umzima kabisa na unaendelea vyema na maandalizi ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2012. Naamini utakuwa ni mwaka wa amani na furaha zaidi kwako. Kikubwa ni kuhakikisha unafanya maamuzi sahihi ya kumteua mtu sahihi wa kuingia naye mwaka huo.

Kama nilivyosema wiki iliyopita, yule aliyekuwa akikuliza na kukukosesha furaha ya mapenzi usimng’ang’anie eti kwa sababu tu umempenda, kama amekuzingua kwa kukupa penzi la kisanii, muweke pembeni huku ukiamini Mungu atakujaalia mwingine ambaye ataufanya mwaka ujao uwe wa amani kwako.

Mpenzi msomaji wangu, wiki hii nataka kuzungumzia kwa kifupi dalili nne za mwanaume aliye tayari kuingia katika maisha ya ndoa. Ni dalili za kitaalam na ukiona huyo uliye naye anazo, una kila sababu ya kumshawishi akuoe tena haraka sana lakini usipoziona ikiwezekana hata ndugu zako wasimjue kwani ni wazi hamuwezi kuingia kwenye maisha ya ndoa ya kueleweka.

Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaume wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuoa kila siku ni wengi lakini je wanaoolewa wote wanaingia kwenye maisha ya ndoa na watu sahihi? Jibu ni hapana, na hii ni kwa sababu wanawake wengine wanakubali kuolewa na wanaume ambao hawakujiandaa kuingia kwenye maisha hayo. Dalili zenyewe ni hizi hapa chini.

Waliobaini kuwa ni muda mufaka
Unaweza kuwa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye umri wake umekwenda lakini bado anaona anastahili kuwa kwenye maisha ya ‘ubachela’. Ukikubali kuolewa na mwanaume wa sampuli hii lazima atakusumbua lakini yule ambaye amekaa, akatafakari kisha akagundua kuwa ni wakati muafaka wa kuoa, ni wazi huyo atakuwa amejiandaa na hata ukimkubalia sidhani kama utajuta.

Anajiamini, siyo tegemezi
Ni kweli mapenzi hayana uhusiano wowote na fedha lakini ukweli usiofichika ni kwamba kama mwanaume hana kazi inayomuwezesha kumuingizia kipato, hawezi kuwa miongoni mwa wale wanaostahili kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Ukikubali kuolewa na mwanaume asiye na kitu eti kwa sababu tu umempenda na moyo wako hauko tayari kumkosa, ujue unajiingiza kwenye maisha ya bahati nasibu kitu ambacho siyo kizuri. Kama huyo uliyenaye siyo tegemezi, ni mtu mwenye uwezo wa kukulisha na kukutimizia shida zako zinazohitaji fedha, usione hatari kumwambia afanye hima akatoe mahari muoane.

Anachukua nafasi ya baba

Kuna baadhi ya wanaume licha kwamba hawajaingia kwenye maisha ya ndoa na hawajafanikiwa kuwa na watoto lakini wameshaanza kuzishika nafasi za ‘ubaba’. Unaweza kuwa na mpenzi akawa ni mtu wa kupenda sana watoto na wakati mwingine kuzungumzia namna wa kwake watakavyokuwa. Huyu ni mwanaume ambaye ana dalili za kutaka kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Anakuchukulia kama mke wake
Chukulia kwamba uko na mpenzi wako lakini jinsi anavyokuchukulia ni kama mke wake. Kwa kifupi utaanza kumuona anachukua nafasi ya mume. Kwa mfano ataanza kuweka mikakati kwa ajili ya maisha yenu ya baadae, atakutambulisha kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, atakuwa akikushirikisha katika kila suala linalogusa maisha yako na yake.
Aidha, mtaalam wa masuala ya mapenzi nchini Marekani, Carol Morgan anaongeza kuwa, licha ya yote hayo pia mwanaume huyo atakuwa ni mkweli na muwazi katika kila jambo.
Hizo ni dalili nne za mwanaume ambaye amejiandaa kuingia katika maisha ya ndoa. Kwa leo niishie hapo, niwatakie kila la kheri katika mwaka mpya unaokuja.

vMwaka umekwisha, unakaribia kustaafu, kuzeeka umejiandaaje?

Inawezekana ninaposema kustaafu wewe kama msomaji wangu unadhani kuwa, nawazungumzia wale walioajiriwa serikalini au kwenye mashirika peke yao. La hasha! Maana yangu kubwa hapa ni kutaka kuzungumzia ukomo wa jumla wa nguvu za kufanya kazi, hii haijalishi aina ya kazi uliyonayo.
Uchunguzi uliofanywa na watafiti wengi duniani kuhusiana na madhara wanayokutana nayo wastaafu wa kazi za kuajiriwa sambamba na wale wanaokumbwa na umri mkubwa wa kushindwa kumudu kufanya kazi umebaini kuwa, watu wengi wamekosa elimu ya kuwawezesha kujua ni wakati gani wa kujiandaa ili kuingia katika tenga hilo la maisha yanayomnyima mhusika fursa ya kujitumikia kwa nguvu zake.
Wengi kati ya wazee waliochunguzwa ambao maisha yao yalionekana ni ya shida na kukatisha tamaa, tangu wale waliokuwa na kazi za kujiajiri mpaka wale waliokuwa wameajiriwa katika viwanda na sekta mbalimbali waligundulika kuwa katika maisha yao ya ujana, kustaafu na kufikiria uzee haikuwa sehemu ya mawazo yao, badala yake waliishi kwa kudhani hali walizokuwa nazo zingedumu, hivyo hawakuwa na hofu ya kuja kuishiwa nguvu na kustaafu kazi.
Hata hivyo, ukweli wanaokubaliana nao watafiti hao wa masuala ya kazi na maandalizi ya uzeeni ni kuwa, mipango ya kustaafu lazima ianze tangu siku ya kwanza mhusika anapoajiriwa kama mfanyakazi au pale anapoingia katika harakati za kimaisha kwa kujitafutia riziki. Wanasema mawazo ya kufikiria uzee na siku za kushindwa kufanya kazi ndiyo yanayochochea juhudi za kimaendeleo, uwajibikaji na utunzaji wa akiba za baadaye.
Hivyo basi, mtu anayetaka kuishi vema baada ya kufikia ukomo wa kufanya kazi ni lazima asiuone ujana kuwa si sehemu muhimu ya kustaafu, wala asidhani uzee unawahusu wenye umri mkubwa, bali auchukulie uwezo wake wa kufanya kazi kama jibu la maisha yake yajayo.
Kustaafu si kitu kinachotokea kwa kushtukiza, bali huja taratibu. Jambo la msingi ni kuzingatia mambo 3 yafuatayo ili uweze kuepuka tabu za maisha baada ya kustaafu au kukosa uwezo wa kufanya kazi. Lakini kubwa zaidi unaloweza kunufaika nalo kwa kuzingatia haya ni kujipatia maendeleo.

KUJIANDAA KIAKILI
Watu wengi hasa wenye kazi za kuajiriwa huwa hawafikirii kuwa kuna siku watakuja kuishi bila kazi. Hawawazi juu ya kufikia ukomo wa nguvu za kumudu majukumu yao ya kazi. Hawaziandai akili zao, ili ziwe tayari kukubaliana na maisha ya uzeeni, ukosefu wa kazi na hata siku za kuugua magonjwa yasiyoponyeka haraka. Ndiyo maana utawakuta watu wanaponda maisha na kutapanya mali kwa kuamini kuwa kesho ya kupata mshahara ipo, huku wakiisahau kesho kutwa ya kukosa mshahara, kustaafu na kukosa nguvu za kufanya kazi.
Kosa hili la kutokujiandaa kiakili ndilo linalochangia wastaafu wengi kupoteza maisha yao muda mfupi baada ya kukosa kazi. Hii inatokana na msongo wa mawazo unaokuja akilini mwao ukitaka kutafuta majibu ya namna ya kuishi katika maisha mapya, ambayo hawakuwahi kuyawaza kabla. Jambo hili ni la hatari sana na wala haipendezi mtu awaze namna ya kuishi baada ya kuwa ameacha kazi au amekosa uwezo wa kujishughulisha.

KUCHAGUA SEHEMU YA KUISHI
Jambo la pili ambalo ni kubwa ni mtu kuchagua mapema sehemu atakayoishi pindi atakapofikia umri wa kustaafu. Watu wengi waliopo makazini au walio na nguvu za kufanya kazi hawachagui sehemu watakayoishi pindi watakapofikia ukomo wa kufanya kazi. Ndiyo maana hawana majibu sahihi ya wapi wanatarajia kuhitimishia maisha yao.
Utamkuta mtu anafikia umri wa kustaafu hajajenga walau banda la kuweka ubavu! Eti wakati anapokabidhiwa malipo yake ndiyo anachukua jukumu la kununua kiwanja na kutaka kujenga nyumba, kitu ambacho huwa kigumu na wengi wamekwama.
Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa wakati ukiwa na nguvu weka misingi ya wapi utaishi, kama ni mjini au kijijini ulikozaliwa. Baada ya uamuzi huo fanya kila uwezalo kuyazoea mazingira na jamii inayoishi kule ulikopanga kuishi. Jenga huko walau kakibanda kadogo. Usingoje kujenga utakapopata fedha za mafao.

29 DEC.BREAKING NEWS RAY APUMZIKA KUIGIZA


STAA mwenye jina kubwa Bongo, Vincent Honorat Kigosi ‘Ray’ ametangaza kupumzika kuigiza filamu kwa muda usioeleweka ili kupisha nafasi kwa wasanii wengine ikiwa ni utaratibu wa Kampuni ya RJ.

Habari zilizotua juu ya dawati la Amani mwishoni mwa wiki iliyopita, zilidai kuwa Ray ambaye ni mkurugenzi wa kampuni hiyo ameamua kufanya hivyo ili kupumzisha akili na kujipanga kwa ubunifu mpya wa kazi zake.

“Kama alivyokuwa amepumzika Johari, naye ameamua kufanya hivyo japo hajasema ni kwa muda gani,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Mwandishi wetu alipomuuliza msanii huyo kwa njia ya simu kama habari hizo ni za kweli, alikiri na kusema:
“Tusubiri mwakani ndipo tuone, lakini mpango huo wa kupumzika upo, si unajua wakati mwingine ni lazima akili ipumzike ili kubuni vitu vikali zaidi,” alisema Ray.



SOURCE GLOBAL PUBLISHERS

29 DEC. PROFESOR JAY ADAI HAUSIKI NA SCRIPT YA KAMILI GADO


Pini jipya la Prof Jay (Kamili Gado) alilomshirikisha Marco Chali litaanza kufanyiwa shooting mapema wiki ijayo chini ya Adam Juma wa Visual lab.

Jay anasema hata husika hata kidogo katika kudirect video hiyo wala kuandika script, na kazi hiyo amewaachia maswahiba wake wa karibu kufanya kazi hiyo ambapo itaandikwa na Frank Gonga, Flaviana Matata, Marcochali, Luca (Bongo 5) na wengine, katika kuonyesha utofauti wa video hiyo na zinginezo.

"Naomba sana watu wajitokeze sana siku hiyo, tuonyeshe jinsi gani tulivyo kamili gado, african girls walivyo kamili gado" amesema Jay.

Wednesday, December 28, 2011

28 DEC.KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WA SENEGAL KWA AJILI YA CAN 2012


Senegal imetaja kikosi chake imara cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku kikiongozwa na mpachika mabao hatari katika Ligi Kuu ya Kandanda ya England, Demba Ba.

Mfungaji hodari msimu uliopita katika Ligi ya Ufaransa Moussa Sow n mshambuliaji wa klabu ya Freiburg Papiss Demba Cisse pia wamo katika kikosi hicho.

Simba hao wa Teranga kama wanavyojulikana, pia watakuwa na mshambuliaji mwengine hatari Dame N'Doye, ambaye alichaguliwa mchezaji bora nchini Denmark mwaka huu.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa Armand Traore, ambaye hivi karibuni alibadili utaifa wake kwa ajili ya kuichezea Senegal, yumo katika kikosi hicho na itakuwa mara yake ya kwanza kucheza michuano mikubwa ya Afrika.

Ni wachezaji sita tu walioiwakilisha Senegal katika michuano ya mwaka 2008 wamesalia katika kikosi hicho.

Mlinda mlango Bouna Coundoul, walinzi Bayal Sall, Souleymane Diawara, Guirane Ndaw, Pape Malickou Diakhate na mshambuliaji Mamadou Niang walikuwemo katika kikosi kilichowakilisha nchini Ghana kilichotolewa katika mzunguko wa kwanza.

N'Doye, ambaye mabao yake 25 katika mechi 31 alizochezea timu yake ya FC Copenhagen yalisaidia timu hiyo kunyakua ubingwa wa Denmark, ni miongoni mwa washambuliaji saba waliochaguliwa na kocha wa timu ya taifa ya Senagal kwa ajili ya mashindano hayo.

Senegal ipo kundi A katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na wenyeji wenza Equatorial Guinea, Zambia na Libya.

28 DEC.BREAKING NEWS SUAREZ AONGEZEWA MECHI MOJA



Taarifa za hivi punde za michezo zinasema mshambuliaji wa klabu ya kandanda ya Liverpool, Luis Suarez amesimamishwa kucheza mechi moja na kutozwa faini ya paundi 20,000 na ameonywa kuchunga tabia yake siku zijazo baada ya kukiri mashtaka yaliyoainishwa na Chama cha Soka cha England juu ya utovu wake wa nidhamu.
Luis Suarez akiri makosa ya utovu wa nidhamu

Suarez hatacheza mechi ya siku ya Ijumaa Liverpool watakapopambana na Newcastle katika uwanja wa Anfield akiwa anatumikia adhabu hiyo.

Hivi karibuni Suarez alipewa adhabu ya kufungiwa kucheza kandanda mechi nane kutokana na kosa la kumtusi kwa maneno ya kibaguzi mlinzi wa Manchester United Patrice Evra, amepewa adhabu hiyo mpya ya mechi moja kwa kuonesha ishara ya matusi walipofungwa bao 1-0 na Fulham tarehe 5 mwezi huu.

Aliinua kidole chake cha kati cha mkono wa kushoto wakati akitoka nje ya uwanja.

Klabu ya Liverpool pia imetozwa faini ya paundi 20,000 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake katika mechi hiyo dhidi ya Fulham.

Wachezaji kadha walimzonga mwamuzi Keith Friend wakati kiungo wa timu hiyo Jay Spearing alipooneshwa kadi nyekundu.

Klabu hiyo imekiri makosa yake kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake lakini imepinga adhabu ya faini.

Hata hivyo, tume huru ya maadili imesema adhabu ya paundi elfu 20,000 ni sahihi.

Liverpool ilisema hawana cha kusema juu ya adhabu hiyo ya kufungiwa kwa Suarez ama faini iliyopigwa klab

28 DEC. HATIMAYE YANGA KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI


HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamethibitisha kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi litaloanza Januari 2 huko Zanzibar.

Yanga iliyokuwa kisuasua kuhusu ushiriki wake kwenye michuano hiyo kwa kutoa sababu mbalimbali kabla ya jana kuthibisha hilo. Katibu Mkuu wa Yanga, Celestin Mwesigwa alisema ni lazima kwa timu yake kushiriki kwenye michuano hiyo ya mapinduzi.

Mwesigwa alisema awali walishindwa kutoa maamuzi kwa kuwa barua ya mwaliko ya kushiriki michuano hiyo ilichelewa kuwafikia."Tulipokea barua ya mwaliko kutoka ZFA (Shirikisho la Soka Zanzibar) Jumamosi na leo 'jana' imejadiliwa hivyo timu yetu itashiriki mashindano hayo," alisema Mwesigwa.

Timu hiyo ni miongoni mwa timu nane zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayoanza Januari 2 hadi12 siku ya kilele cha sikukuu hiyo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyotokea miaka 49 iliyopita.

Timu zitakazoshiriki mashindano hayi ni pamoja na mabingwa watetezi Simba, Azam na Yanga zote za Tanzania Bara, nyingine ni Jamhuri ya Pemba, Mafunzo, Miembeni United, Super Falcon na Kikwajuni zote za Visiwani.

28 DEC.VIKOSI VYA SIMBA NA YANGA KWENYE MICHUANO YA CAF


TIMU za Simba na Yanga zimewasilisha usajili wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya mashindano ya kimataifa mwakani, huku wachezaji Artif Amour wa Yanga na Ulimboka Mwakingwe wa Simba majina yao yakiwa hayapo.

Artif Amour mchezaji chipukizi aliyeripotiwa kukulia kwenye timu ya watoto ya Arsenal, ambayo timu yake ya wakubwa inashiriki Ligi Kuu England ni moja ya wachezaji waliopambwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa wana uwezo mkubwa, lakini jina lake halipo kwenye orodha ya Yanga iliyowasilishwa TFF.

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alithibitisha jana kuwa wamewasilisha majina 28 TFF ili yatumwe makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya ushiriki wa Ligi ya
Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itacheza na Zamalek ya Misri hatua ya awali.

“Tumewaacha Artif na Zuberi Ubwa, lakini wengine wote yameenda hata Rashid Gumbo ambaye baadhi ya magazeti yaliandika ameachwa, jina lake tumelipeleka,” alisema Sendeu.

Wachezaji ambao majina yao yamewasilishwa TFF kuombewa usajili Yanga kwa mujibu wa chanzo chetu ni Nadir Haroub, Shadrack Nsajigwa, Kigi Makasy, Jerry Tegete, Chacha Marwa,
Juma Seif, Bakari Mbegu, Abuu Ubwa, Shamte Ally, Nurdin Bakari, Hamis Kiiza na Keneth Asamoah.

Wengine ni Yaw Berko, Idrisa Rashid, Haruna Niyonzima, Shaaban Hassan, Said Mohammed, Rashid Gumbo, Pius Kisambale, Godfrey Taita, Oscar Joshua na Stephano Mwasika, Omega Seme, Godfrey Bonny, Ibrahim Job, Salum Telela na Athumani Idd. Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kwenye taarifa yake jana kuwa Simba na Yanga tayari zimewasilisha usajili wao na kwamba Simba iliwasilisha wachezaji 24 na Yanga 28.

“Mwisho wa kufanya usajili ni Desemba 31 mwaka huu na kila klabu inaruhusiwa kusajili hadi wachezaji 30. Hata hivyo Agosti mwakani kutakuwa na usajili wa dirisha dogo kwa timu
ambazo hazikumaliza nafasi zote 30,” alisema Wambura ambaye hakutaja majina yaliyowasilishwa TFF.

Hata hivyo, akizungumza baadaye jana na gazeti hili, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wamewasilisha wachezaji 25 na kwamba kulitokea tatizo la kiufundi, hivyo jana
walipeleka barua TFF kurekebisha hali hiyo.

“Ni majina 25 tuliyopeleka, kuna tatizo lilijitokeza, tayari tumeliweka sawa, “ alisema Kamwaga ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina yaliyopelekwa TFF wala walioachwa.

Lakini habari zilizopatikana kutoka ndani ya klabu ya Simba zilieleza kuwa wachezaji Rajabu Isihaka na Ulimboka Mwakingwe majina yao hayamo kwenye usajili huo wa CAF.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ndani ya Simba, orodha kamili iliyotumwa TFF kwa ajili ya kupelekwa Caf ni makipa: Juma Kaseja, Ally Mustapha na William Mweta.

Mabeki ni Nassoro Said, Derick Walulya, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Juma Jabu, Victor Costa, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Obadi Mungusa na Hassan Khatib ambaye amepandishwa
kutoka kikosi cha pili cha Simba.

Viungo; Mwinyi Kazimoto, Machaku Salum, Uhuru Selemani, Patrick Mafisango na Haruna Moshi.

Abdalla Seseme, Frank Senkule, Ramadhan Singano na Jonas Mkude wametoka kikosi cha pili.

Washambuliaji ni Gervas Kago, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na Edward Cristopher aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili.

28 DEC.KAFULILA KUENDELEA KULA POSHO KWA MUDA

MAHAKAMA Kuu imetoa amri kusitisha kutekelezwa kwa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya
Chama cha NCCRMageuzi wa kumfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
hadi kesi aliyofungua itakapomalizika.

Uamuzi huo ulitolewa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Alise Chingwile kutokana na maombi ya zuio yaliyowasilishwa na Kafulila kupitia Kampuni ya Uwakili ya Asyla ya Dar es Salaam.

Wakili wa Kafulila kutoka kampuni hiyo, Daniel Welwel alisema maombi hayo waliyawasilisha Ijumaa iliyopita chini ya hati ya dharura, kupinga kuvuliwa uanachama.

Kwa mujibu wa Wakili huyo, katika maombi hayo, walidai kwamba uamuzi huo wa NCCR-Mageuzi ukitekelezwa dhidi ya Kafulila atakuwa amekosa sifa za ubunge na jimbo litakosa mbunge.

“Tukasema na kesi ya msingi itakuwa haina maana,” alidai Wakili wa mwanasiasa huyo kijana
aliyewahi pia kuwa mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Katika kesi ya msingi ambayo itatajwa Februari 21, mwakani, Kafulila kupitia kwa mawakili wake, anadai uamuzi wa NCCR Mageuzi haukuwa halali kwa sababu Katiba ya chama hicho haikufuatwa.

Vile vile anadai hakupewa haki ya kusikilizwa licha ya kwamba ni haki yake ya msingi.

Anadai pia kwamba wajumbe walioshiriki kupitisha uamuzi huo, wengine hawakuwa wajumbe halali.

Watu wanaomuunga mkono pamoja na walio karibu na mbunge huyo, akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), wameelezea kufurahishwa na uamuzi huo wa Mahakama.

“Kafulila kuendelea na ubunge..... Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita.

Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote,” alisema Zitto kupitia mtandao wa kijamii.

Wengine wamekaririwa wakifurahia kwa kusema hiyo ni habari njema kwa walalahoi kwa kuwa
Uchaguzi Mdogo ukifanyika ni maumivu kutokana na Bajeti ya Serikali kuhamishiwa kwenye
shughuli hiyo.

Uamuzi wa kumfukuza uanachama mbunge huyo pamoja na watu wengine sita akiwemo
Hashim Rungwe aliyegombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ulifanyika Desemba 17, mwaka huu katika kikao cha NEC Taifa ya NCCR-Mageuzi jijini Dar es Salaam.

Chama hicho chenye wabunge wanne wote kutoka majimbo ya Mkoa wa Kigoma, kilitoa siku 14 kwa Kafulila na wenzake kukata rufani.

Naibu Spika Job Ndugai akizungumza na gazeti hili juu ya zuio hilo la Mahakama Kuu, alisema
suala hilo linahitaji wanasheria waliobobea watafsiri sheria ikizingatiwa kwamba Ofisi ya Bunge ilishapokea barua ya NCCR-Mageuzi ya kumvua uanachama mbunge huyo.

“Hapo panahitaji wanasheria wasaidie kutafsiri. Kama tumepata barua ya chama, sisi hatuna cha kufanya isipokuwa kutii. Kama Mahakama imefanya hivyo (kuzuia), Kafulila apeleke nakala ya uamuzi, tujue sheria inasemaje,” alisema Ndugai.

Alisisitiza kwamba, “huwezi kuwa Mbunge kama chama chako kimekukana. Spika anakuwa hana chaguo. Tunahitaji wanasheria waliobobea kutafsiri sheria.”

Awali, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah alikiri kwamba ofisi imekwishapokea barua ya
NCCR Mageuzi ya kumvua ubunge Kafulila na kwamba inafanyiwa kazi, ingawa hakuna muda maalumu wa kutenda kazi hiyo.

Tuesday, December 27, 2011

27 DEC.BREAKING NEWS.YANGA YAJITOA KOMBE LA MAPINDUZI


HAPBARI AMBAZO ZIMETUFIKIA HIVI PUNDE KLABU YA YANGA IMEJITOA KTK MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI,SABABU ZA KUJITOA KWA KLABU HII KTK MICHUANO HIYO NI UKATA AMBAO UMEIKUMBA KLABU HIYO PAMOJA NA KISHINDWA KUFANYA MAZOEZI KWA SIKU 7 .HAYO YAMEBAINISHWA JANA NA KOCHA WA KLABU HIYO AMESEMA KUWA AMEFUTA MICHEZO YOTE YA KIRAFIKI NA WAMEJITOA KUSHIRIKI MICHUANO YA MAPINDUZI. HALI YA KUTOFANYA MAZOEZI KWA SIKU 7 IMETOKANA NA UWANJA WA KAUNDA AMBAO YANGA HUWA WANAUTUMIA KWA AJILI YA MAZOEZI

27 DEC. PAPIC MBIONI KUITEMA YANGA


'NDOA' ya Kocha Kostadin Papic na klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, haijasimama kwenye mstari ulionyoka na kwa sababu hiyo, huenda akaachia ngazi kama uongozi hautarekebisha kasoro zilizopo.Jana, Papic aliyerejea kuifundisha Yanga kwa mara ya pili, alikutana na waandishi wa habari na kueleza wazi jinsi mambo yalivyo magumu Jangwani.

Katika mengi aliyoeleza mbele ya waandishi, msingi mkuu wa malalamiko yake ni kutengwa kiushirikiano na viongozi wa Yanga.Papic alisema hapati ushirikiano wa kutosha toka kwa viongozi wa klabu hiyo pamoja na jitihada kubwa ya kufanya nao mawasiliano.

"Ni kama wamenitenga, hatuwasiliani kama inavyopaswa kuwa, napiga simu zao hawapokea na wakati mwingine hazipatikani."Unafanya vipi kazi na watu wasiokuwa ushirikiano hasa katika kipindi hiki timu inakabiliwa na michuano ya kimataifa," alisema.

"Klabu ina hali mbaya kifedha, mimi na wachezaji hatujalipwa mishahara yetu mpaka leo na uongozi umekaa kimya bila kusema lolote," alilalama Papic.Alisema wachezaji wake wamekaa kimya lakini haina maana kwamba wanafurahishwa na hali ya mambo ndani ya klabu.

"Wachezaji wangu hawajasema lolote, lakini kwa kuwangalia wanaonekana kuumia na hali hii ya kutolipwa mshahara mpaka sasa. Sura zao matumaini zimepotea kabisa."

Alisema anashangazwa na ukimya wa uongozi wa Yanga katika kipindi ambacho wanakabiliwa na mtihani mgumu wa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zamalek.

Papic aliyewahi kufundisha soka nchi kadhaa Afrika, alisema katika mazingira magumu kama hiyo si rahisi kuwaandaa wachezaji kupata ushindi."Siyo kwamba najitetea, lakini kama timu itashindwa kufanya vizuri kwenye mechi hiyo, basi asilaumiwe yeye wala wachezaji wake."
"Hatujafanya mazoezi kwa siku saba ukiacha siku tatu za mvua. Mbali na mazoezi ya uwanjani hata Gym hatujakwenda.

"Nimechukua jukumu la kuwakumbusha mara kwa mara viongozi kushughulikia suala hili, lakini mpaka leo sijapata jibu la maana.Papic amesema amekata tamaa ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo kwa vile uongozi wake umesema wazi hauna pesa."Hakuna mazoezi, hakuna mechi za kirafiki ukiuliza unaambiwa wiki ijayo, kila siku wiki ijayo, hakuna kinachotekelezwa.

"Nimeomba mechi sita za kirafiki za kimataifa lakini hakuna kinachotekelezwa mashabiki wasije kuwalaumu wachezaji kwa lolote hali halisi ndio hiyo.Kuhusu mkataba wake na Yanga, Papic alilalamika kutothaminiwa, akitoa mfano wa kuishi kwenye mazingira magumu baada ya nyumba aliyopangishiwa kukatwa maji na umeme.

"Hali ni ngumu kwangu binafsi na kwa wachezaji wangu, kuamua kwangu kuzungumza ni kwa sababu hali imefika hatua ambayo haipaswi kuvumiliwa."Kujiuzulu ni silaha yangu ya mwisho lakini kwanza napambana, kusaka wadhamini na wadau wa kutusaidia iwapo itashindikana sitakuwa na jinsi," alisisitiza.

"Yanga ina wanachama na mashabiki wengi, ni vizuri wakasikia kilio hiki na kujitokeza kusaidia ili timu ipate mahitaji na kujiandaa vizuri."

Akijibu malalamiko ya Papic, mmoja kati ya viongozi wa juu wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alisema ameshangazwa na kauli za Papic kwa waandishi wa habari.

Alisema kimsingi Papic hakupaswa kuongelea matatizo ya wachezaji kwa vile si jukumu lake. "Ameita waandishi wa habari na kuwaeleza matatizo ya wachezaji, haitasaidia kwa sababu matatizo ya klabu yatamalizwa na klabu na si vyombo vya habari," alisema bosi huyo.

Kuhusu kutaka kujiuzulu, alisema: "Kama Papic anaona ipo sababu ya kufanya hivyo hatuwezi kumzuia kwa vile ana haki ya kuamua bila kushurutishwa."

Kiongozi huyo pia alishangazwa na kauli kwamba (Papic) hajalipwa mshahara mpaka leo. "Nimkumbushe kwamba, aliposaini mkataba na Yanga tulimpa mishahara ya miezi miwili mbele, leo anasemaje kwamba hajalipwa mshahara," alihoji.

Kuhusu suala la kukatiwa maji na umeme, alisema hilo ni jukumu lake. "Hivi ukikatiwa umeme na maji nyumbani kwako utakwenda ofisini kulalamika?"

Kuhusu wachezaji kutolipwa mishahara, alikiri ni kweli hawajalipwa kwa vile tarehe wanayolipwa bado haijafika.
"Mishahara ya wachezaji inalipwa tarehe 28 kila mwezi, sasa leo ni tarehe ngapi mtu afikie kusema wachezaji hawajalipwa mishahara," alihoji bosi huyo.

Kuhusu mazoezi, alisema anachofahamu yeye ni kwamba walisimama wakati wa mvua na si vinginevyo. "Anasema hawajaenda kufanya mazoezi Gym inashangaza kwa sababu klabu ina Gym.

Papic aliwahi kuinona Yanga toka Januari 2009 mpaka 2010 kabla ya kumwaga manyanga kwa madai ya kuingiliwa kiutendaji na uongozi wa Yanga.

Alirejeshwa tena kuchukua nafasi ya Kocha Sam Timbe raia wa Uganda aliyetimuliwa kwa madai ya kushindwa kuibadilisha timu ingawa aliiwezesha kutwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la Kagame.

Kabla ya kutua Yanga pia aliwahi kufundisha timu za Orlando Pirates, Maritzburg United, Kaizer Chiefs na Hearts of Oak.

27 DEC. KHADIJA KOPA ALIVYOPAGAWISHA MASHABIKI UGIRIKI


MALKIA wa mipasho (taarab) nchini, Khadija Kopa, aliwapeleka ‘mbaya’ mashabiki wa Tanzania waishio katika jiji la Athens, Ugiriki, alipoangusha vitu vya uhakika katika ukumbi wa Axum.

Mashabiki waliofurika ukumbi huo ni pamoja na wananchi wa Afrika Mashariki ambao ni kutoka Kenya na Uganda.

Moja ya vivutio vya burudani hio alikuwa ni kijana anayechipukia kwa miondoko hiyo ya ‘rusha roho’ ajulikanaye kwa jina la muziki kama Michael Jackson ambaye jina lake halisi ni Juma Ramadhani. Msanii huyo alishirikiana na ‘mdada’ mmoja wa nguvu ambaye aliweza kuzimiliki vyema nyimbo za malkia mwingine wa taarabu nchini Bongo, Aisha Ramadhani aka Mashauzi.

Ilikuwa ni burudani tosha licha ya kwamba nchi yenyewe ya Ugiriki imekumbwa na matatizo ya kiuchumi, ambapo uchumi wake unatishia kuyumbisha maisha ya wananchi wake.

Monday, December 26, 2011

26 DEC.MATOKEO YA MECHI ZA LEO ZA EPL

CHELSEA 1 FULHAM 1


LIVERPOOL 1 BLACKBURN 1


WEST BROM 0 MAN CITY 0


MAN U 5 WIGAN ATHLETICS 0

26 DEC. MAKUNDI KOMBE LA MAPINDUZI

WAANDAAJI wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi wametoa ratiba ya michuano hiyo, inayoonesha kuwa timu za Yanga na Azam za jijini Dar es Salaam zimewekwa kundi moja.

Kulingana na ratiba hiyo iliyotolewa jana kwa waandishi wa habari na msemaji wa Kamati ya
Kombe la Mapinduzi, Farouk Karim, Yanga itakuwa Kundi B na Azam, Mafunzo ya Unguja na Kikwajuni ya Pemba.

Kwa mujibu wa Farouk Kundi A lina timu ya Simba ya Dar es Salaam ambao ni mabingwa watetezi, Miembeni United na KMKM za Unguja pamoja na Jamhuri ya Pemba.

Ratiba inaonesha kuwa mashindano hayo yataanza Januari 2 mwakani, ambapo jioni Azam
itacheza na Kikwajuni na usiku Yanga itacheza na Mafunzo, mechi zote zikiwa kwenye Uwanja wa Amani.

Farouk alisema kuwa Januari 3 Miembeni United itacheza na KMKM na usiku Simba itacheza
na Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Awali jana, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi, ambaye hakutaka kutajwa
jina lake kwa madai sio msemaji alisema kwamba Yanga ilikuwa bado haijathibitisha ushiriki
wake.

Alisema kutokana na hali hiyo Kamati ya Kombe la Mapinduzi ilikuwa kwenye wakati mgumu
wakati wa kupanga ratiba, ingawa baadaye walikubaliana waiweke.

“Haya si mashindano ya mtu binafsi ni ya taifa na kama haitashiriki tutasema kuwa wametudharau,” alisema mjumbe huyo.

Alieleza kuwa kama Yanga haitashiriki ni vyema ingewaeleza mapema ili waweze kutafuta timu
mbadala badala ya kuamua kukaa kimya mpaka sasa.

Lakini akizungumza jana, Ofisa Habari wa Yanga, Luios Sendeu alisema Yanga itashiriki
mashindano hayo kama walivyopanga na kueleza kuwa Kamati ya Ufundi ya Yanga inalishughulikia suala hilo kwa ukamilifu zaidi.

“Tutacheza hakuna wasiwasi… Yanga haiwezi kukimbia kucheza,” alisema Sendeu.

Akizungumza baadaye jana Farouk alisema Yanga itashiriki mashindano hayo na ndiyo
sababu wameiweka kwenye ratiba.

26 DEC.JAHAZ YAMUANIKA MPENZI CHOCOLATE KWA KISHINDO!



Bendi ya muziki wa mwambao ya Jahaz Modern Taarab, usiku wa kuamkia leo imefanikisha kwa kishindo uzinduzi wa albamu yake ya tano waliyoipa jina la Mpenzi Chocolate.

Uzinduzi huo ulifanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo ulienda sambamba na kusherehekea miaka mitano tangu bendi hiyo ianzishwe.

Sunday, December 25, 2011

25 DEC. Ghetto Diva adondosha 'DICTATION


Ghetto diva anasema "u gatta pay attention to this,hizi flow zafanya watu wadate na dictation zangu dunia nzima zatanda.

So write it down! "nimerecord hii track juu ya beat ya producer mosco wa majengo arusha,vocals na Mixing kasimamia defxtro pande za noizmekah.com.

So ma fans wote wa hiphop wajue GD bado niko hai kimziki ni mkimbizano na maisha hapa na pale tuko pamoko, shout out kwa mahomiez freelodaz pande za masaki,media personel zote TZ na EastAfrica kiujumla i Love y'All...

25 DEC.MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA


UCHAGUZI MKUU WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA/TANZANIA FILM FEDERATION-TAFF ULIOFANYIKA TAREHE 22/12.2011


1. Simon Mwakifwamba --Rais
2. Suleiman Ling’ande - Mjumbe
3. Wilson Makubi - Mjumbe
4. Mike Sangu - Mjumbe
5. Christian Kauzeni- Mjumbe
6. Makame Bajomba- Mjumbe
7. Emmanuel Myamba- Mjumbe
8. Deosonga Njelekela- Mjumbe
9. John Kallaghe- Mjumbe
10. Ally Baucha- Mjumbe
11. Maureen Mvuoni- Mjumbe
12. Mwanaharusi Hela- Mjumbe

Uchaguzi ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa BASATA na kusimamiwa na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) chini ya maofisa wake Anjelo Luhala na Omary Mayanga.

Kwa mujibu wa Katiba ya TAFF ,nafasi ya Katibu na mweka hazina ni nafasi ambazo zinateuliwa na Raisi wa shilikisho vivyohivyo wajumbe wanatakiwa wawe kumi na mbili ambapo kumi wanakuwa wakuchaguliwa kwa kula na wawili wa kuteuliwa na Raisi wa TAFF

Uongozi uluoingia madarakani utafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu TAFF-Tanzania Film Federation ni shirikisho lenye mjumuisho wa vyama tisa(9),ambavyo ni

1. TASA-Tanzania Scriptwriter Association
2. TCA-Tanzania Cameraperson Association

3. TDFAA-Tanzania Drama and Film Artist Association
4. TAFIDA-Tanzania Film Directors Association

5. TAFEA-Tanzania Film Editors Association

6. TALOMA-Tanzania Location Manager Association
7. TAFDA-Tanzania Film Distributor Association

8. TAFPA-Tanzania Film Producer Association
9. TAMPTA-Tanzania Motion Picture Teachers Association

Twatarajia kuwa mtaweka mbele kauli ya Uongozi ni dhamana na miaka mitatu sio mingi sana kama hamna mipango mizuri na pia miaka mitatu ni mingi sana kwa mtu aliyekuwa na mikakati
mizuri yenye kueleweka.

25 DEC. WASOMI UDOM WAKUTWA NA MISOKOTO YA BANGI


JUMLA ya wanafunzi 10 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi, wengine wakikutwa wanaivuta.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Fulgence C. Ngonyani amethibitisha kuwa wanafunzi hao walikamatwa Desemba 20, mwaka huu, majira ya saa 11.00 jioni katika maeneo ya Kitivo cha Elimu chuoni hapo baada ya kufanyika msako wa kuwasaka wanafunzi wahalifu.

Alisema katika msako huo jumla ya wanafunzi 10 walikamatwa wakivuta dawa za kulevya aina ya bangi katika maeneo ya kitivo hicho.

Kaimu kamanda aliwataja waliokamatwa katika maeneo ya kitivo cha elimu kuwa ni Joseph Jona (27), Mwakasitu Ikwisa (29), Chabae Mussa (25), Hamisi Issaka (25), Shaban Said (25), wanafunzi kitivo cha Elimu mwaka wa tatu na Stambuli Rahim (22), mwanafunzi wa kitivo cha
Elimu mwaka wa pili.

Alisema kuwa, mbali na wanafunzi hao sita, wanafunzi wengine wanne (4) walikamatwa
Desemba 15, mwaka huu katika kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha kwa kosa la uvutaji
wa bangi ambao walipekuliwa katika eneo la tukio na kukutwa na misokoto 16 ya bangi.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mutongore Filbert (27), mwanafunzi mwaka wa tatu, Samwel Seiboko (24), Ahmed Abdulaziz (20) na Nkembo Boniface (24), mwaka wa tatu wa shahada ya
uhasibu.

Alisema kuwa, wanafunzi hawa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kaimu Kamanda alisema kuwa, msako huo ni endelevu katika vitivo vyote ili kuhakikisha vitendo kama hivyo vinakoma katika eneo lote la chuo cha UDOM.

Katika hatua nyingine, Kaimu kamanda aliwataka madereva na watumiaji wote wa barabara kuwa waangalifu kwa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Pia, aliwatakia wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwani Jeshi la Polisi linawahakikishia wananchi wote kuwa ulinzi utaimarishwa ili kuwawezesha kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu.

“Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma anawaasa wakazi wote wa Dodoma kutumia haki ya kusherehekea vema sikukuu ya Krismasi na wananchi wakumbuke wajibu wa kuhakikisha kwamba usalama unadumishwa na kutii sheria zote,” alisema.

Pia aliwataka wenye kumbi za starehe na burudani kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa, vilevile wananchi wanaaswa wanapokwenda kwenye nyumba za ibada na kumbi za starehe kuhakikisha nyumba zao zipo katika hali ya usalama kwa kufunga milango, madirisha au kuwaacha baadhi ya watu kwa ulinzi wa makazi

25 DEC. Zanaco, Dynamos kucheza na Simba, Yanga



MIAMBA ya soka ya Zambia, Zanaco na Power Dynamos wanatarajia kuja nchini kwa ziara ya kimichezo ambapo watavaana na Simba na Yanga.

Timu hizo zinakuja nchini kwa mwaliko wa Klabu ya Michezo ya Kemramba ya Musoma, Mara na Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (Kifa) na zikiwa hapa zitacheza mechi mbalimbali za kirafiki jijini na mikoani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Charles Changarawe, Zanaco watakuwa wa kwanza kuwasili Desemba 29 wakiwa na wachezaji watano wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Changarawe ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Kifa ambao wanaratibu ziara ya Dynamos
alisema timu hizo zimepangiwa kuvaana na Simba na Yanga kabla ya mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza.

Mkurugenzi huyo alisema Desemba 31 miamba hao watakutana na vinara wa Ligi Kuu Simba jijini kabla ya kuvaana na Yanga siku inayofuata.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya timu ya Zanaco, watavaana na Toto Afrika ya Mwanza jijini humo Januari 8 na pia kucheza Arusha, Musoma, na Mbeya kabla ya kurejea Zambia Januari 18.

Dynamos ambao wanatarajia kuwasili nchini Januari 5 watavaana na Simba Januari 7 na
siku inayofuatia watakutana na Yanga kabla ya kuanza ziara za mikoani ukiwepo mkoa wa
Arusha, Mwanza, Sinyanga na Musoma, Mbeya na kurejea kwao Januari 24.

25 DEC.SETTLE SOUNDERS YAMPOTEZEA NGASA


HATIMA ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu ya Azam FC, Mrisho Ngasa kujiunga na timu ya Seattle Sounders ya Marekani ipo mashakani kutokana na kutoeleweka kinachoendelea sasa baada ya kukatika kwa mawasiliano.

Akizungumza na Mwandishi wa blogu hii, Katibu Mkuu wa timu ya Azam FC, Nassoro Idrissa alisema pamoja na Ngassa kufanya majaribio na kuchezea mechi ya kihistoria dhidi ya Manchester United, mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote.

Idrissa alisema baada ya Ngassa kurejea nchini na kupewa ahadi ya kurudi tena Marekani, hawajapata taarifa tena kama.

Alisema kwa sasa Seattle Sounders inaendelea na usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya msimu ujao na walitarajia kuona Ngassa anakwenda huko ili kukamilisha zoezi hilo au kwa majaribio kabla ya hatua nyingine.

“Kwa sasa hatufahamu lolote kuhusiana na hatima ya Ngassa, hakuna mawasiliano yoyote na kwa vile Ngassa ni mchezaji wetu, basi ataendelea kuichezea timu yetu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano mengine,” alisema Idrissa.

Alisema kuwa bado wana matarajio mchezaji wao kuichezea timu hiyo au nyingine kwani ni miongoni mwa wachezaji wenye vipaji na hazina kubwa kwa timu yao na timu ya Taifa.

“Sisi halituumizi na si tatizo kwetu, kwanza hatujatumia gharama yoyote katika mchakato mzima. Lakini nisema kwamba hatukauwa na kipingamizi, tutajadiliana nao kuwaeleza matakwa yetu, ikishindikana ataendelea kuwa Azam,” alisema.

Mratibu wa majaribio hayo, Rahim Kangezi alisema kuwa anasubiri mawasiliano kutoka kwa timu hiyo japo si kiongozi wa Azam FC.

“Mimi ni kiongozi wa African Lyon, sitahusika na makubaliano yoyote kuhusiana na usajili wa Ngassa, sijui kimekwama nini, ila najua usajili bado mpaka Machi mwakani,” alisema Kangezi.

Alisema kuwa endapo Seattle Sounders watamwita Ngassa kwa majaribio, itabidi apitie utaratibu wa kimataifa wa kupimwa afya yake kabla ya kusaini.

25 DEC. I WISH U ALL MARRY X MASS

Saturday, December 24, 2011

24 DEC. KENNY DALGLISH AMTETEA SUAREZ


Anfield boss refuses to see how the club's t-shirt defence of the Uruguayan could have offended people after the player received an eight-game ban for using racist language


The Reds' squad warmed up in t-shirts bearing the Uruguayan's image at Wigan on Wednesday to show support for their top scorer, who had been found guilty of racially insulting Manchester United defender Patrice Evra a day previously.

The FA ruling was met with a strongly worded statement from Liverpool that vehemently defended the striker, with some critical of the club's actions.

"The statement couldn't have caused anyone any trouble," Dalglish told reporters.

"I don't think the players have caused any trouble with the FA either by their statement or support by their T-shirts. If we are not in any trouble we will leave it at that before we do get in any trouble.

"[Suarez has] been quite emotional and very grateful, I don't think it is ever a disappointment when the people you work for give you their undivided support and I think that is the least he deserves."

Liverpool are yet to receive a written version of Suarez's judgement, which will include the evidence used to reach the decision, and once they have the document, the club will have 14 days to lodge an appeal.

Dalglish continued: "Most of the people have had their say, we've had our say but we will wait for the judgement and take it from there, but it won't be tomorrow [Saturday].

"The club have issued the statement, the players have issued their statement visually and verbally, but we have to wait for the written report because no-one knows [what it contains].

"At this moment in time I don't think the club are permitted to go into any further detail than they have done."

24 DEC, Sintah, Kajala wamaliza bifu

MSANII wa filamu Bongo, Husna Poshi ‘Dotnata’, juzikati aliingia tena kwenye kibarua kizito cha kuondoa bifu kati ya mastaa wa sinema, Christina Manongi ‘Sintah’ (pichani) na Kajala Masanja, Risasi Jumamosi ni shuhuda.

‘Mkutano’ wa usuluhishi ulifanyika Desemba 20, mwaka huu ndani ya Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dar es Salaam ambapo mastaa hao walikutana ‘laivu’ kwenye kikao cha maandalizi ya harusi ya Mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beats cha Star TV, Sauda Mwilima.

Katika kikao hicho, mastaa hao walinuniana kiasi cha kushindwa kusalimiana.

Hali hiyo ilimsukuma Dotnata kuwaita mara baada ya kikao na kuwasuluhisha ingawaje iliwachukua muda mrefu kwa wasanii hao kuchukua uamuzi huo.

Akizungumzia ishu hiyo kwa paparazi wetu, Dotnata alisema kuwa, katika kazi ya usuluhishi iliyowahi kuchukua muda mrefu ni pamoja na ugomvi wa mastaa hao.

“Nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu wote, namshukuru Mungu nimefanikiwa na wameahidi kutokwaruzana tena kwa chochote,” alisema Dotnata.
Paparazi: “Kwani ugomvi wao mkubwa ni nini?”
Dotnata: “Mh! Naomba hilo tuliache kwa sasa.”


SOURCE GLOBAL PUBLISHERS

24 DEC. MAKOCHA WAKIGENI KUPATA VIBALI KUTOKA CAF



MAKOCHA wa kigeni wanaofundisha timu za Yanga, Simba na Azam sasa wanatakiwa kuomba kibali toka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kuendelea kuzinoa timu zao.Yanga na Simba zinafundishwa na Waserbia, Kostadin Papic na Milovan Cirkovic, huku Azam ikifundishwa na Stewart Hall raia wa Uingereza.

Katika sheria mpya ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), inaeleza makocha wote wa kigeni ni lazima wapate kibali maalum cha kufanya kazi toka CAF.

Akizungumza na gazeti hili, Mkufunzi wa CAF na Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Shirikisho la Soka la Zambia, Honour Janza alisema hivi sasa CAF ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha leseni wanazotoa kwa makocha Afrika zinatambuliwa na UEFA.

Pia wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) ili kudhibiti makocha kutoka Ulaya na Marekani kumiminika Afrika kwa kuweka sheria ambazo watalazimika kuzifuata na kupata vibali cha CAF.

"Kuna kasumba ya nchi nyingi za Afrika kuchukua makocha toka Ulaya, mpango wa CAF sasa ni kuhakikisha makocha wa Afrika wanapata fursa ya kufundisha nchi yoyote duniani na ndio maana tunazungumza na FIFA ili leseni zetu zitambuliwe na UEFA.

"Kwa makocha ambao wapo tayari hapa Tanzania hata kama wana leseni ya daraja B (UEFA) ni lazima wafanye utaratibu wa kuomba kibali CAF ili waweze kuendelea na ajira zao, sheria hii inafanyiwa kazi ikikamilika itaanza kutumika mara moja," alisema Janza.

"Hali kadhalika kwa makocha wa Tanzania na Afrika kwa jumla mpango huu utasaidia makocha wenye leseni za CAF kwenda kufundisha soka popote duniani, kikubwa ninachowaasa makocha wa Tanzania wasijifunge hapa nchini tu watoke wasake ajira kila mahali wawe na moyo wa kujituma na kujiendeleza kila wakati."

Janza alisema hayo wakati akifunga kozi ya siku nne ya makocha kwenye Uwanja wa Taifa.Alisema zaidi: "Kocha ni lazima aende na wakati kwa kujua mbinu mpya za kufundisha soka kwa kusoma.

"Kama mnataka maendeleo makocha wasijifunge, mfumo wa ufundishaji mpira unabadilika kila siku, ni lazima wasome kozi za muda mfupi, mitandao na wajue CAF wanachofanya kwa wakati,"alisema Janza.

"Maendeleo ya soka hutokana pia na uwapo wa makocha bora, hivyo ni lazima makocha wajue sheria 17 za mchezo wenyewe na mbinu mpya ili kukuza uelewa wa soka la kisasa."

Alisema nchi nyingi za Afrika zimelala ndio maana soka lao limedumaa tofauti na Ulaya na kwamba CAF wamegundua hilo na ndio maana wametoa mapendekezo ya kutaka mabadiliko

24 DEC. MILOVAN APATA KIBALI CHA KUFANYIA KAZI


KOCHA wa Simba ya Dar es Salaam, Milovan Cirkovic, amepata kibali cha kufanya kazi nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa hatua hiyo ni furaha kwa mashabiki wa Simba kuomba sasa apewe ushirikiano wa kutoka.

“Klabu inapenda kutumia nafasi hii kushukuru Idara ya Uhamiaji, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla kutokana na ushirikiano wa hali ya juu uliooneshwa katika kipindi cha kushughulikia suala hili.

“Kwa taarifa hii, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wanatoa wito kwa wadau, mashabiki na vyombo vya habari kumpa nafasi Milovan ili sasa apate fursa ya kuutumia ujuzi wake wa hali ya juu kwenye kuimarisha soka la Tanzania,” alisema Kamwaga.

Alieleza kuwa leseni yake ya ukocha alionayo Milovan ndiye atakuwa kocha wa kiwango cha juu zaidi anayefanya kazi nchini kwa sasa.

Wakati huohuo, Kamwaga alisema mechi ya Simba na timu ya Eskom ya Malawi iliyokuwa ifanyike Jumapili sasa itachezwa Jumatatu ijayo.

“Mabadiliko haya yametokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam ambazo zimeathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu, wakiwamo wapenzi wa kandanda na pia Uwanja wa Taifa wenyewe ambako mechi ilipangwa kuchezwa.

“Simba pia inapenda kutoa salamu za pole kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na mvua hizo za Dar, Mara na Mbeya na iko pamoja na wote walioguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine,” alisema

24 DEC.AT Sio Mzanzibari...!!


Msanii AT, amesema ameshtushwa sana na kauli ya baaraza la sanaa la kisiwani huko, kwamba yeye sio raia wa Tanzania visiwani na kuanzia sasa kwa sababu msanii huyu kwa sasa anaishi Tanzania Bara, itabidi awe analipia anapokwenda kufanya shoo zake Zanzibar.

AT amesema yeye ni mzaliwa wa Zanzibar, amezaliwa Mwembeladu Unguja na watu wote wanamfahamu akisisitiza kuwa amedhalilishwa sana kwa kuvuliwa uraia na watu wasio na mamlaka ya Uhamiaji.

Msanii huyu alikumbana na maswahiba ya kushushwa jukwaani hivi karibuni huko Unguja alipokuwa akifanya onyesho, na imefahamika kuwa, hata video ya msanii huyu inayojulikana kama ya bao la kete, imefungiwa kuchezwa katika vituo vya televisheni visiwani humo kutokana sababu ziliyoelezwa kuwa ni za kimaadili.

24 DEC. Joh Makini Kumnunulia Cherehani Muhanga Wa Mafuriko Dar...



"Mweusi" mkali wa Hip-Hop Tanzania Joh Makini ameguswa na mafuriko yanayoendelea kuikumba Dar-es-Salaam na wakazi wake na kutoa sifa kwa kituo cha Televisheni cha EATV kwa kuwa karibu na wananchi kwa kuwapatia taarifa za umakini kwa kila kinachoendelea kuhusiana na mafuriko hayo.

Kufuatia EATV kuonesha muhanga mmojawapo wa mafuriko mama wa makamo fundi cherehani aliyepoteza mali zake ikiwemo cherehani, EATV imeandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa Joh Makini amesema atamnunulia mama huyo cherehani mpya.

24 DEC .Taifa Stars yaitwa Misri


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imealikwa kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Misri Februari mwakani.

Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Angetile Osiah alisema wamepokea barua ya mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Misri (EFA) juzi na wamejibu kuthibitisha kukubali mwaliko huo.

Alisema Misri imeomba kucheza mechi hiyo kati ya Februari 19 na 20 ama 23 na 24, lakini alisema wao wamewaandikia kuomba wacheze kati ya Februari 23 na 24.

Osiah alisema shirikisho la nchi hiyo litagharamia gharama zote za timu ya taifa kuanzia tiketi, malazi na gharama nyingine za mechi hiyo.

Alisema mechi hiyo ya kirafiki ni fursa nzuri kwa timu ya taifa kujiandaa na mashindano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Tanzania inayoshika nafasi ya 137 na Misri inayoshika nafasi ya 31 kwa ubora wa viwango vya
shirikisho la soka la kimataifa (Fifa) zote zimeshindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika
zikatakazofanyika kwenye nchi za Gabon na Guinea Ikweta mwakani.

Wakati huo huo, TFF imekataa mwaliko wa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kutaka timu ya
soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kucheza na timu ya soka ya Zanzibar kwenye maadhimisho ya sikukuu ya Mapinduzi ZanzibarJanuari 2 mwakani.

Akitoa msimamo huo jana, Osiah alisema Kilimanjaro Starshaitacheza mchezo huo kwa
sababu wachezaji wake wengi wanaounda timu hiyo watakuwa kwenye timu za Azam, Simba na
Yanga ambazo pia zitashiriki mashindano hayo.

Pia Osiah alisema hata Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Charles Boniface atakuwa na timu ya soka ya taifa ya wanawake(Twiga Stars) ambayo inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika dhidi ya Namibia mwakani.

Januari mwaka huu, Taifa Stars ilikuwepo jijini Cairo Misri kwenye mashindano ya Nchi za
Bonde la Mto Nile iliyoshirikisha saba, ambapo Taifa Stars mchezo wa ufunguzi ilifungwa mabao 5-1 na wenyeji

Friday, December 23, 2011

23 DEC.SUGU ASEMA,VINEGA LAZIMA TUTASHINDA


Toka ukurasa wake wa Facebook, Mbunge wa Mbeya Mjini na kiongozi wa VINEGA anasema haya....Kwa niaba yangu na Vinega wote wa Anti-Virus napenda kutoa shukrani kwa sapoti mnayotupa kutoka kila pande ya dunia...from Kenya to Japan,South Africa to China,India to Iran and all Europe and America...we r winning this war because of you..its now all about vinega movement worldwide baby..from the bottom of my heart i say god bless y'all and keep supporting...!!!

23 DEC. LEO NI SIKU YA KUZALIWA YA MBWANA SAMATA


LEO NI SIKU YA KUZALIWA YA MCHEZAJI WA KULIPWA WA TP MAZEMBE NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA,KAMA MDAU WASPOTI NA MTAKIA MAISHA MEMA,AKAZE ILI SIKU MOJA AJE KUCHEZEA KLABU KUBWA KM MAN CITY

23 DEC. Yaya Toure Mchezaji bora


Mcheza kiungo wa klabu ya Manchester City na pia Timu ya Taifa ya Ivory Coast,Yaya Toure amechaguliwa kua mchezaji bora wa soka na Shirikisho la soka ya Afrika(CAF)


Mchezaji huyo mashuhuri alipitia mchujo wa ushindani na Seydou Keita kutoka Mali anayechezea klabu ya Barcelona na Andre Ayew wa Ghana pia klabu ya Olympique Marseille.

Toure, mwenye umri wa miaka 28, alichaguliwa na Makocha wa Timu za Mataifa ya Afrika kutoka nchi wanachama wa CAF.

Mwenyewe Yaya Toure alisema baada ya kutangazwa kua mchezaji bora kua, ''Hii ndio zawadi kubwa ambayo ningeweza kuipokea katika maisha ya uchezaji wangu soka.''

Inakumbukwa kua Yaya Toure ndiye aliyefunga bao pekee la klabu yake ilipoibwaga Stoke City katika fainali ya Kombe la FA mnamo mwezi Mei.

Toure aliyekua amebubujika kwa furaha alisema kua anajivunia tuzo hio na ni siku kuu kwake, na kuongezea kua ana imani hilo litaipa Timu yake ya Ivory Coast msukumo wakati wakiazimia kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika hapo mwakani.

Ushindi wa Toure ulihitimisha furaha ya nchi yake ya Ivory Coast ambayo ilikua tayari inasherehekea mshindi wa zawadi ya Refa bora wa CAF iliyomwendea Noumandiez Doue.

Mchezaji chipukizi aliyejitokeza ni mchezaji mchanga anayechezea klabu ya Tottenham, Souleyman Coulibaly aliyeshinda zawadi ya mchezaji bora mdogo mwenye kipaji. Oussama Darragi wa klabu ya Esperance akachaguliwa ,chezaji bora anayecheza soka yake barani Afrika kama mchezaji bora wa mwaka.

Kocha wa mwaka alikua Harouna Doula aliyeiongoza Timu ya Taifa ya Niger hadi kufuzu kwa fainali za fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huku Botswana nayo ilitajwa kama mojapo ya Timu zilizofuzu kwa mara ya kwanza kabisa.

Timu ya Wanawake ya Cameroon ilitajwa kua Timu bora ya soka ya wanawake huku Mwanamke bora miongoni mwa wachezaji waliotia fora akiwa Perpetual Nkwoche wa Nigeria.

Thursday, December 22, 2011

22 DEC. Papic:Kikosi changu chahitaji dozi zaidi


Aliweza kukiri kwamba timu yake bado haijafikia kiwango wanachokitaka na kwamba hali hiyo ndiyo iliyowafanya wazidiwe na kulala 2-0, kwenye mechi yao ya kirafiki dhidi ya Azam iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa hapa Jijini.

Si mwingine bali ni yule Kocha wa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kostadin Papic kwamba mechi hiyo imempa picha kwamba bado wachezaji wake hawajafikia kiwango cha kukabiliana na ushindani dhidi ya timu zenye maandalizi ya kutosha.

Alisema kikosi chake chahitaji dozi zaidi ya mazoezi ili wafikie katika ubora wanaouhitaji.

Ndani ya mechi hiyo watoto wa Jangwani waliburuzwa kwa kasi ya ajabu, kwa pasi maridadi za Azam katika muda mwingi wa mechi na hivyo.

Kwani hakukuwa na shabiki aliyeshangaa kuona wakipata kipigo kilichotokana na mabao hayo kutoa kwa washambuliaji hao wa zamani yaani Gaudence Mwaikimba aliyefunga la utangulizi katika kipindi cha kwanza na Mrisho Ngassa aliyeongeza jingine katika kipindi cha pili.

Papic, alisema kuwa mechi hiyo imempa picha kwamba bado wachezaji wake hawajafikia kiwango cha kukabiliana na ushindani dhidi ya timu zenye maandalizi ya kutosha, hivyo wanahitaji 'dozi' zaidi ya mazoezi ili wafikie katika ubora wanaouhitaji.

Yanga na Azam watakutana tena mwezi ujao visiwani Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakayoanza Januari 2.

22 DEC. Fid kurelease tatu za kuaga mwaka!


Anayeaminika kushikilia taji la mkali wa vina mpaka dakika hizi, namzungumzia Fareed Kubanda a.k.a Ngosha The Don anatarajia kuachia video tatu kabla ya mwisho wa mwaka huu ikiwa ni zawadi ya mwaka mpya.

Fid anaweka wazi kuwa maandalizi ya kurelease Video hizo yamekamilika na wakati wowote kuanzia sasa ataanza kuzisambaza kwenye vyombo husika.

Mipini anayotarajia kurelease ni pamoja na ‘Lelewe mitaa’, ‘Juhudi za wasiojiweza’, pamoja na ‘Neno’.

22 DEC.SUAREZ ASEMA LAZIMA AKATE RUFAA


Liverpool striker Luis Suarez will appeal against his Football Association punishment for racially abusing Patrice Evra, according to his lawyer.

Alejandro Balbi, who is also Suarez’s agent, said his player was “convinced” the punishment would be reversed.

Suarez was handed an eight-game ban and £40,000 fine after he used “insulting words in reference to Manchester United defender Evra’s colour”.

“It seems to us absolutely out of proportion,” Balbi said.

“He [Suarez] is firmly convinced this hard sanction can be reversed.”

Speaking at a news conference in Uruguay capital Montevideo, Balbi said that it would be Liverpool’s lawyers who made the appeal to the FA.

Suarez, who denied the allegations, has 14 days to launch his appeal against the decision. Should he do so, there is a possibility length of the ban could be increased.

SOURCE: BBC Sport

Wednesday, December 21, 2011

21 DEC.Shukrani toka kwa C-pwaa! I


I would like to thank you all for your support my people, and special thanks to all Websites, Bloggers, Twitters, BBM'ers, Facebook, within 48 hours we have 0ver 5990 views on Youtube!

Haijawahi kutokea kibongo!Lets share the link an hit a Million views! Yes we can!

21 DEC.K-LYN ATAMANI KURUDI KWENYE GAME


Former Miss Tanzania, ambaye pia ni mwanamuziki ktk anga hizi za Bongo, namzungumzia mwanadada Jackquline Ntuyabaliwe ‘K-LYNN’, amesema anatamani kurudi katika game lakini anashindwa kutokana na kubanwa na kazi nyingi anazojishughulisha nazo kwa sasa.

Kwa mujibu wa mwanadada huyo mrembo anaamini mashabiki wake wamemmiss na wanamuhitaji ili aweze kutoa tena burudani lakini anawaomba waendelee kumsubiri kidogo akiwa anajiandaa na ujio wake mpya atakaokuja nao.

K-Lynn anasema kuna uwezekano mkubwa mwakani akarudi kwenye game huku akiwa na staili mpya ambayo inaweza kumtoa zaidi, “ninaweza kurejea katika game kwani muziki bado upo katika damu,” alimalizia.

21 DEC. John Terry kufikishwa mahakamani


Nahodha wa Timu ya Taifa ya England John Terry anakabiliwa na mtihani wa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji mwenzake Anton Ferdinand wakati wa mchuano wa Ligi kuu.


Inasemekana kua John Terry alitumia lugha ya ubaguzi wakati wa pambano kati ya klabu ya Chelsea na Queens Park Rangers iliyomalizika kwa ushindiwa QPR mnamo tarehe 23 Oktoba.

Huduma inayohusika na mashtaka(CPS) inasema kua Bw Terry anakabiliwa na mashtaka ya ukiukaji wa sheria ya ubaguzi wa rangi hadharani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameapa kujitahidi kwa ala kulla hali kukabili madai hayo.

Polisi imemhoji mchezaji huyo wa Chelsea kwa tahadhari tangu mwezi Novemba na faili kuhusu suala hilo kutumwa kwenye huduma za mashtaka mwanzoni mwa mwezi huu wa Disemba.

Alison Saunders, Mwanasheria mkuu wa jiji la London, amesema kua ameishauri Polisi ya mji mkuu kumfungulia mashtaka John Terry kwa matamshi yake ya kuchukiza kinyume cha sheria inayohusu ubaguzi wa rangi.

Chama cha mpira, FA kiliahirisha upelelezi wake kikisubiri uwamuzi wa Huduma ya mashtaka ukamilike.

Kutokana na hatua ya hivi sasa Bw.Terry anatarajiwa kufika mbele ya Koti ya Mahakama ya London ya magharibi ifikapo tarehe 1 Febuari.

Akipatikana hatia atatozwa hadi pauni za Uingereza 2,500.

Uwamuzi juu ya kesi ya John Terry unatokea siku moja baada ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Luis Suarez kuhukumiwa kifungo cha kukosa mechi nane za Ligi kwa kumtukana beki wa klabu ya Manchester United - Patrice Evra

21 DEC.Man United yalalamikia mgao wa tikiti


Manchester United imelalamika kwa Chama cha Kandanda cha England -FA- kuhusiana na mgao wao wa tikiti kwa mpambano wa Kombe la FA mzunguko wa tatu mwezi Januari dhidi ya Manchester City.

Chini ya taratibu za FA, Manchester United wana haki ya kupata mgao wa asilimia 15 ya uwezo wa viti 47,805 katika uwanja wa Etihad, ambao ni sawa na tikiti 7,100.

Hata hivyo, Manchester City imetoa tikiti 5,500, ikiwa ni asilimia 11 tu, hii ni kutokana na sababu za usalama uwanjani.

Manchester United ina mgawanyo maalum kutoka kwa FA, kutokana na uwezo wa uwanja wake wa Old Trafford wenye viti 76,000, kutoa asilimia 11 ya tikiti kwa timu ngeni, sawa na tikiti 8,500.

Mashateni hao Wekundu wanadai wapatiwe mgao wao kamili kwa ajili ya pambano hilo, litakaloanza saa saba mchana siku ya Jumapili tarehe 8 mwezi wa Januari.

Manchester City, ambao kwa sasa wanashikilia usukani wa Ligi Kuu ya England, watawakaribisha mahasimu wao hao wakubwa Manchester United katika mtanange huo wa Kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1955.

Timu hizo zilikutana katika hatua ya nusu fainali mwaka jana kwenye Kombe la FA uwanja wa Wembley, ambapo Manchester City waliibuka washindi kwa bao 1-0 , baadae wakailaza Stoke katika fainali na kufanikiwa kushinda mashindano makubwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 35.

Manchester City iliwaadhibu Man United walipokutana mara ya mwisho kwa mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye uwanja wa Old Trafford.

Tuesday, December 20, 2011

20 dec.mtanzania apata timu uingereza


CHAMA cha Mpira wa Miguu Uingereza (FA) kimetuma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kumuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mchezaji Douglas Didas Masaburi ili ajiunge na klabu ya nchini humo.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kuwa Masaburi mwenye umri wa miaka 21 anaombewa ITC ili ajiunge na klabu ya Coventry Spartans akiwa mchezaji wa ridhaa. Coventry Spartans iko katika Ligi Daraja la Pili ya Midland.

“Mchezaji huyo anaombewa ITC kutoka katika klabu ya New Rule Power. TFF inafanyia kazi
maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika,” alisema Wambura.

Wakati huohuo, Wambura alisema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Zambia kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia.

Mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani.

Mwamuzi ni Gladys Lengwe wakati waamuzi wasaidizi ni Patience Mumba na Mercy Zulu.

“Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Bookanang Lekgowe kutoka Botswana wakati kamishna
wa mechi hiyo kutoka Afrika Kusini atakuwa Smith Hilton Fran,” alisema.

Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Nasra Mohamed ilianza rasmi mazoezi Desemba 19 kwa ajili ya mechi hiyo.

20 DEC.SERIKALI YA BOTSWANA YAKATAA KUNUNUA HAKI YA KUONESHA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA


Mashabiki wa kandanda nchini Botswana wamenyimwa nafasi ya kuishuhudia timu yao taifa ikishiriki mashindano yajayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Botswana kugoma kununua haki ya kutangaza kutoka kampuni ya Ufaransa ya SportFive.

Serikali imesema gharama ya Pula milioni 15 sawa na dola za Marekani milioni 1.98 haziingii akilini.

Msemaji wa serikali ya Botswana Dokta Jeff Ramsaya ameiambia BBC kwamba kiwango cha Pula milioni 15 kuweza kupata haki ya kuangalia timu yao ya taifa ikishiriki katika mashindano hayo kimeonekana ni kikubwa sana.

Hatua hiyo imekuja baada ya majadiliano kuvunjika kati ya SportFive na Televisheni ya taifa (Btv), ambayo inaitegemea serikali kwa fedha.

"Kwa sasa tunakabiliwa na matatizo ya fedha katika bajeti yetu, kwa kweli tulitenga kiasi cha fedha katika bajeti na kiwango hiki hatukukiweka," Ramsay alieleza.

Aliongeza kueleza ana matumaini mashabiki wengi wa kandanda wataweza kufuatilia michuano hiyo kupitia televisheni za kulipia zinazoonesha mashindano hayo kwa kutumia mitambo ya setelaiti.

Ramsay ameongeza kusema serikali tayari imewekeza kiasi cha fedha kwa kuiandaa timu yao ya taifa inayoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo.

Serikali ya Botswana inagharamia mazoezi ya siku kumi ya timu hiyo iliyopiga kambi nchini Afrika Kusini katika kituo cha michezo cha Royal Bafokeng Sports mjini Rustenburg.

Baada ya kumaliza kambi huko Rustenburg, timu ya taifa ya Botswana maarufu Zebras ama Pundamilia itaelekea nchini Qatar tarehe 26 mwezi huu, ambapo watafanya mazoezi katika chuo cha Aspire Academy kwa gahrama za serikali.

Botswana wapo katika kundi D pamoja na Ghana, Mali na Guinea.

Wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola mwaka 2010, Btv iliamriwa kusimamisha kutangaza fainali hizo baada ya kushindwa kukosa haki ya kuonesha -huku kampuni ya SportFive ikielezea kwamba Btv walionesha mechi ya ufunguzi kinyume na sheria.

Monday, December 19, 2011

19 DEC. Kiongozi Korea Kaskazini afariki dunia


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-il amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo katika umri wa miaka 69, vyombo vya habari vya serikali vimetangaza.

Mamilioni ya raia wa Korea Kaskazini ‘wamegubikwa na huzuni isiyoelezeka’, Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema. Watu wameonekana wakilia katika mji mkuu Pyongyang.

Mwanae Kim Jong-un ameelezewa na KCNA kama "mrithi mkuu " ambaye wakorea kaskazini hawana budi kumuunga mkono na kuwa nyuma yake.

Jirani wa Pyongyang wako katika hali ya tahadhari. Taarifa ambazo hazijathibitshwa kutoka Korea Kusini zinasema Korea Kaskazini imefanya majaribio ya nyuklia Jumatatu.

Shirika la habari la Yonhap mjini Seoul lillisema kombora la nyuklia la masafa mafupi lilitupwa pwani ya mashariki ya nchi hiyo maskini iliyojitenga na yenye kumiliki nyuklia Jumatatu lakini haikujulikana haraka iwapo jaribio hilo linahusiana na tangazo la kifo cha Kim Jong-il.

"Huu unaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko kwa Korea Kaskazini”"

William Hague, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza

Korea Kusini imeweka silaha zake kwa tahadhari baada ya tangazo hilo, ikisema nchi hiyo ilikuwa kwenye mgogoro unaofukuta. Serikali ya Japan imefanya mkutano wa dharura.

Uhusiano wa China na Korea Kaskazini na ubia katika biashara wameonyesha kushtushwa na habari za kifo hicho na kuahidi kuendeleza na kuimarisha "mchango wake was amani na utulivu katika rasi ya ukanda huu ."

Masoko ya hisa ya Asia yalishuka baada ya habari hizo kutangazwa.
Kilio cha sauti

Tangazo la kifo cha Kim Jong-il lilitolewa kwa kusomwa taarifa yenye hisia kupitia televisheni ya Taifa.

Mtangazaji, akiwa na mavazi meusi, alijitahidi kuzuia machozi wakati akisema alikufa kutokana na kufanya kazi za nguvu na kiakili kupita kiasi. The announcer, wearing black, struggled to keep back the tears as she

Baadaye shirika la habari la KCNA likaripoti kuwa alikufa kutokana na "maumivu makali ya kifua yanayoambatana na mshtuko wa moyo na kisha kuacha kusukuma damu (myocardial infarction)" saa mbili na nusu muda wa huko siku ya Jumamosi (23:30 GMT Ijumaa).

Wakati huo alikuwa kwenye gari moshi katika moja ya ‘safari zake za ulekezaji vijijini’, KCNA lilisema.

Shirika hilo la habari la serikali limesema mazishi yatafanyika Pyongyang tarehe 28 Disemmba na Kim Jong-un ataongoza kamati ya mazishi. Muda wa maombolezo kitaifa umetangazwa kuanzia tarehe 17 to 29 Disemba.

Picha kutoka ndani ya taifa hilo lenye tahadhari kubwa zimeonyesha watu mitaani Pyongyang wakilia baada ya taarifa za kifo hicho.

Wanachama wa chama tawala katika moja ya kijiji cha Korea Kaskazini walionyeshwa na televisheni ya Taifa wakipiga mesa na kulia kwa sauti, Shirika la habari la AFP limeripoti.

"Siwezi kuamini. Ataondokaje namna hii? Tunafanyeje sasa?" mmoja wa wanachama anayeitwa Kang Tae-Ho alinukuliwa akisema.

Mwingine, Hong Sun-Ok, alisema:"alijaribu kufanya kazi kwa bidii kufanya maisha yetu kuwa bora na ametuacha hivi tu."

KCNA linasema watu "walikuwa wakitetemeka kwa uchungu na kukata tamaa, " kwa kuondokewa namna hii, lakini wataungana nyuma ya mrithi wake Kim Jong-un.

19 DEC. DIAMOND ATOA TAHADHALI


Guyz u need to be very waangalifu coz kuna mtu anatumia jina langu kwenye facebook picha na vitu kibao akijifanya yeye ni Diamond.. mbaya zaidi anatukana, kutongoza na kuwatapeli watu kibao.. Diamond platnumz wa kweli ana Account moja tu! na account yake hauwezi kum Add coz ana too many friend request, so ukiona account imeandikwa Diamond Platnumz halaf. ukii Add inakubali jua huyo si wa kweli" Says Diamond Platnumz

19 DEC. CPwaa's New Music Video to be officially released this weekend


Greetings Ladies and Gentlemen, The 3 Tanzania Kilimanjaro Music Awards winner and Channel O nominated Artist from Tanzania, CP well known as CPwaa will release his most anticipated new music video this weekend of 17th -18th Dec 2011 officially for the first time on Internet through Social Network sites( Facebook, Twitter,MySpace), BBM, and Blogs.This primary release will be followed by a release of the video to all National and International TV stations worldwide effectively from 19th Dec 2011. This will be CPwaa's new song/video to be released after ACTION song/video which was released last year December.The King of Bongo Crunk " CPwaa" has been working on this project since July 2011 and has confirmed that the work is finally ready to go out as planned. Below are further details of the song and video. Song Title: "Hhmm....." Artist: CP a.k.a CPwaa Genre: AfroTechno Producer: Lucci Studio: ( Vocal and Mixing) MJ Records. Video Director: Adam Juma ( Visual Lab-Next level) Location: Sandton City, Johannesburg. South Africa. Guests Stars: Navio ( Uganda), Hanni( Ethiopia BBA Housemate 2011), XO(Nigeria), Tiffany ( Nigeria), Turas ( Ghana) and many more. The video will also be exclusively premiered on Channel O's " Volt Extra" with 30 minutes of behind the scenes,CPwaa's history,Biography, Music Videos and interviews. For the latest feeds on Cpwaa follow him on Twitter @Cpwaa or visit www.cpwaa.co.tz Thank you. TeamCPwaa