tuwasiliane

Friday, February 19, 2016

NANI NI NANI,KATI YA SIMBA NA YANGA KESHO TAIFA

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena hapo kesho kwa jumla ya michezo sita kuchezwa.
Macho na masikio ya wapenda soka yatakua yakisubiri kwa hamu Dabi ya kariakoo kati ya Wekundu wa msimbazi Simba Sport Klabu, dhidi ya timu ya wananchi Dar Young Afrikans Yanga, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la taifa Jijini Dar Es Salaam.
Michezo mingine itayaopigwa hapo kesho Mgambo Jkt wataonyeshana ubavu na Tanzania Prisons, Stand United wao watawalika Jkt Ruvu.
Mbeya City wao watakua nyumbani Sokoine kukupiga na Wanalambalamba Azam FC , huku wanalizombe Majimaji wakikipiga na wakata miwa wa Mtibwa Sugar .Toto Africans ya Mwanza, wao watawalika jirani zao kutoka mkoani Kagera, Kagera Sugar.
TAKWIMU MUHIMU ZA MECHI YA SIMBA NA YANGA NI KAMA IFUATAVYO Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 45, katika michezo 19 wakati Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 katika michezo 18, iliyocheza na Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 katika michezo 17.
Katika pambano la mzunguko wa kwanza lililopigwa Septemba 26 uwanja wa taifa Yanga wakiwa wageni walishinda mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Amissi Tambwe aliyewahi kuichezea Simba na Malimi Busugu akitokea benchi mapema kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Simon Msuva mchezaji bora na mfungaji bora msimu uliopita.
Mashabiki wa Simba watakwenda uwanjani Jumamosi wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi na hiyo imetokana na timu yao kushinda mechi sita mfululizo zilizopita chini ya kocha Jackson Mayanja ambaye ndiyo amechukua nafasi ya Dylan Kerr, aliyefukuzwa mwezi uliopita,.Mwenendo huo pamoja na kupanda hadi nafasi ya kwanza kutoka ya tatu waliachwa na kocha Kerr, ndiko kumefufua matumaini ya timu hiyo kushinda mchezo wa Jumamosi lakini pia kubeba ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu huu.
Kuelekea mchezo huo Yanga wanaoonekana kuwa na kikosi bora wamekuwa kimya kanakwamba wameingiwa na hofu baada ya kelele na tambo za wapinzani wao Simba wanaoranda mitaani wakijitapa kulipa kisasi cha mabao 2-0, walichofungwa kwenye mzunguko wa kwanza.
Kimtazamo ukiviangalia vikosi vya timu zote mbili Yanga wanaonekana kuwa bora zaidi ya Simba kuanzia kucheza kitimu hata uwezo wa mchezaji mmoja mmoja nap engine kimya chao ndiyo silaha yao kujua wanaingiaje kwenye mchezo huo wa Jumamosi na kupata ushindi kama walivyofanya mchezo uliopita.
Lakini pengine kimya cha mashabiki wa Yanga kimetokana na hofu waliyonayo baada ya timu yao kufanya vibaya katika mechi mbili za ligi zilizopita dhidi ya Coastal Union ambayo walifungwa bao 2-0 na kutoka sare ya 2-2 na Tanzania prisons huku wakionyesha kiwango kibovu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Bado haija julikana ingawa mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wenye ushindani mkubwa kwa pande zote mbili hasa ukizingatia namna ambavyo wachezaji wakila upande pamoja na makocha wao walivyopania kupata matokea ya ushidi.
Timu hizo mbili zimekuwa na upinzani mkubwa tangu zilipoanzishwa miaka ya 1935 kwa Yanga na Simba mwaka 1936,kitu ambacho kimechangia kuwepo uhasama mkubwa wakimichezo kila upande ukihitaji ufalme ndani ya uwanja huku zikitofautishwa na Barabara katika makazi yao.Kutokana na ukongwe zilizokuwa nazo timu hizo ndizo zinaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi kila kona ya Tanzania na nchi za nje na wakati zinapokutana mambo mengi hutokea wakati mwingine hufikia hata watu kupoteza maisha endapo timu yake inapoteza mchezo na kama ni kiongozi akibainika ndiyo amechangia timu yake kupoteza mchezo huenda akawa na wakati mgumu pengine hata kuchomewa nyuma yake ama gari lake.
Hiyo ni kwa viongozi na wachezaji lakini mambo huwa mabaya zaidi kwa makocha na wachezaji mara nyingi timu hizo zinapokutana na moja wapo kupoteza mchezo lawama kubwa huwaangukia wachezaji au makocha na kama ni kocha basi hukufukwa kazi na huwa haijalishi kuwa mchezo huo ni wakirafiki au mashindano.
Hali huwa mbaya zaidi kwa wachezaji ambapo wengi wao huwa wanahusishwa na kupokea rushwa kutoka upande wa pili na inapotokea hiyo hata kama anajua kiasi gani atajikuta anawekwa benchi hadi mkataba wake utakapokwisha na kufungashiwa virago vyake.

Timu hizo mbili ndizo zinaongoza hata kwa mafanikio na Yanga ndiyo wanaongoza kwa kubeba mara nyingi ubingwa wa ligi ya Tanzania mara 25 wakifuatiwa na Simba mara 18 idadi hiyo inadhihirisha pia kwamba timu hizo zimekutana mara nyingi zaidi na Yanga ndiyo ilishinda michezo mingi ingawa miaka ya karibuni Simba wamekuwa wakiinyanyasa sana Yanga.
Pamoja na mapinduzi yaliyoletwa na klabu ya Azam FC, lakini BADO Simba na Yanga zimbaki na nguvu yao kubwa kiasi hata cha kuwanyima mashabiki Azam licha ya kuwa na kila kitu ikiwemo kumiliki uwanja wao wa kisasa na vitu vingine vingi ikiwemo Hosteli.Rekodi nzuri kwa Simba katika mapambano yake na Yanga ni kupata ushindi wa mabao mengi kama ilivyofanya mwaka 1977 iliweza kuifunga Yanga mabao 6-0 na Mei 6 mwaka 2012 iliipa tena kipigo cha aibu cha mabao 5-0,uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Simba imekuwa makini kwa kutumia vizuri madhaifu yawapinzani wao inapo wakuta wamechoka na kufunga mabao mengi yanayowapa rekodi nzuri kwenye historia za timu hizo.

Takwimu za Goal za miaka mitano iliyopita kuanzia 2009 zinaonyesha Simba na Yanga zimekutana mara 11 ikiwa ni mechi maalumu pamoja na zile za Ligi Kuu ya Tanzania bara.

Katika idadi hiyo Simba inaongoza kwa kushinda mara nne na Yanga ikipata ushindi mara tatu na mara nne zikienda sare lakini kizuri kwa Yanga ni kuwa na bahati ya kupata ushindi inapokutana na Simba mwezi Oktoba.

Oktoba 16 mwaka 2010 pambano la Ligi Kuu Tanzania bara lilifanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Jeryson Tegete dakika ya 70.

Yanga ilifanya tena hivyo Oktoba 29/2011 kwa kuifunga Simba safari hii ikiwa uwanja wa taifa Dar es Salaam mfungaji akiwa Mzambia Davis Mwape dakika ya 75,na msimu uliofuata kidogo vijana wa Msimbazi waligoma kufanywa wateja baada ya kukutana Oktoba 3/2012 na kutoka sare ya 1-1 na Yanga Simba wakitangulia kufunga kupitia kwa Amri Kiemba dakika ya tatu na Yanga ikasawazisha dakika ya 64 kupitia kwa Said Bahanuzi. 

Oktoba 20,2013,Simba iligoma kwa mara nyingine kufungwa na Yanga kwenye mwezi huo baada ya kulazimisha sare ya mabao 3-3 huku yenyewe ikitoka nyuma ka mabao matatu yaliyofungwa kipindi cha kwanza na Yanga.

Wafungaji wa Yanga katika mechi hiyo walikuwa ni Mrisho Ngasa aliyefunga bao la kwanza dakika ya 14 na Mganda Hamisi Kiiza aliyefunga mara mbili dakika ya 35,47 Mabao ya Simba yalifungwa na Beatram Mwombeki dakika ya 53Joseph Owino dakika ya 5 na Mrundi Gilbert Kaze dakika ya 83 mechi hii ikiwa maalumu ikipewa jina la Nani Mtani Jembe.

Ushindi pekee iliyowahi kuupata Simba inapocheza na Yanga ndani ya miaka mitano iliyopita ilikuwa ni Oktoba 31 ambapo iliweza kuifunga Yanga bao 1-0 mfungaji akiwa Mussa Hassani Mgosi dakika ya 26.

Katika takwimu hizi zilizowekwa na Mtandao wa Goal kila timu inacho cha kujivunia katika pambano hilo la Jumamosi Simba imekuwa na kipindi kizuri katika miaka mitano iliyopita wakati Yanga ikifurahi kukutana na Simba mwezi Oktoba kwa sababu imekuwa na bahati nao.

Lakini wakato Goal inakuwekea rekodi hizo timu husika kwa sasa zipo katika maandalizi kabambe kujiandaa na pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka.

Yanga ambao ndiyo wenyeji wa pambano hilo licha ya kufurahia kucheza mwezi Oktoba lakini wanajivunia matokeo yao ya ushindi katika mechi mbili zilizopita dhidi ya JKT Ruvu na Cercle de Joachim ya Mauritius ambayo yanawapa ari ya kuingia kwa nguvu kwenye mchezo huo na kutaka kuendeleza ubabe kwa wapinzani wao hao Simba.Ikumbukwe timu hiyo haijafanya vizuri katika misimu miwili iliyopita ambapo msimu wa 2012/13 ilimaliza nafasi ya tatu na msimu wa 2013/14 ikamaliza nafasi ya nne na msimu huu imetumia fedha nyingi kwa ajili ya kusajili wachezaji wenye majina na viwango vya juu ili kuweza kushinda taji hilo na mipango yao inaelekea kufanikiwa baada ya sasa kuongoza ligi hiyo na kuziacha nyuma Yanga na Azam.
Tusubiri kipyenga cha Mwamuzi Jonesia Rukyaa ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha pambano na 90 zitamalizika kwa timu gani ikiwa na furaha.

1 comment:

  1. What solid post this is for me and usually posts some really exciting stuff like this.spanish teacher tarifa

    ReplyDelete