tuwasiliane

Friday, February 19, 2016

Mwambusi: Simba lazima wafe kesho

Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm (kulia) na Msaidizi wake Juma Mwambusi
Mechi ya Simba dhidi ya Yanga ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kila timu ikijigamba kuwa itamfunga mwenzake, Mwambusi anasemaje?
Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema haoni sababu ya kikosi chao kupoteza mchezo wa  kesho Jumamosi dhidi ya Simba kutokana na maandalizi mazuri wanayoendelea kuyafanya pamoja na kurejea kwa wachezaji wao wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa majeruhi.
Mwambusi amekiambia chanzo kimoja kuwa, anajua kama mchezo huo utakuwa mgumu kwakua wapinzani wao Simba wangependa kuendeleza wimbi la ushindi kama walivyofanya huko nyuma lakini amewataka wafute wazo hilo kwani kikosi chao kipo imara zaidi ya wanavyo fikiria.
“Tunakijua kile ambacho kinawapa matumaini ya kushinda mchezo wa kesho Jumamosi lakini kama mabingwa watetezi tumejipanga kuepukana nazo na kushinda kama ilivyokua mzunguko wa kwanza na sisi tutaonyesha ubora wetu siku hiyo uwanjani,”amesema Mwambusi.
Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 43, katika michezo 18 iliyocheza na endapo itashinda mchezo huo itapanda hadi kileleni ikiwa na pointi 46, huku ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja na kama Simba wakishinda wataendelea kujitanua kileleni wakiwa na pointi 48.

No comments:

Post a Comment