Donald Ngoma
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Singida United, Atupele Green anaamini kuwa Donald Ngoma ndiye mshambuliaji aliyekamilika katika Ligi Kuu Bra kuliko straika yeyote kwa sasa.

Atupele amejiunga na Singida United akitokea klabu ya JKT Ruvu iliyoshuka daraja msimu uliopita, amemwagia sifa Ngoma kuwa  ni straika mwenye kila kitu tofauti na washambuliaji wengi hapa nchini, ana nguvu, kasi, uwezo mkubwa wa kupiga mashuti kadhalika ni mzurikwenye kucheza mipira ya juu.

Akifanya mahojiano na gazeti la michezo la Mwanaspoti, Atupele amesema katika ushindani huo anawatoa Okwi, Luizio, Ajibu kwa sababu nyota hao si washambuliaji wa kati wengi upenda kutokea pembeni

"Kati ya mastraika wote wa Simba na Yanga, hakuna anayeweza kumzidi Ngoma, yule mtu ana kila kitu. Nacheza nafasi hiyo ya straika, hivyo ninachokizungumza nakimaanisha" alisema hivyo Atupele Green.
Donald Ngoma alijiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Fc Platnumz inayoshiriki Lig Kuu ya nchini Zimbabwe, misimu hiyo miwili amefunga zaidi ya magoli 30 katika mashindano yote.