Manchester City inataka kuichukulia Arsenal hatua za kisheria baada ya kuzuia uhamisho wa Alexis Sanchez siku ya kufungwa dirisha la usajili wa majira ya joto.
Miamba hao wa Manchester inaaminika walifikia makubaliano ya paundi milioni 60 na Arsenal kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mapema Alhamisi asubuhi, lakini hakuna kilichofanyika.
Arsenal waliamua kubatilisha makubaliano hayo baadaye siku hiyo baada ya kumkosa Thomas Lemar, ambaye aliamua kubaki Monaco kwa msimu mwingine.
Kwa mujibu wa chanzo cha Chile El Murcurio, sakata hilo la uhamisho halijaisha bado kwani City wanataka maelezo ya kina ni kwa nini waligeuziwa kibao na wanataka kwenda mbele zaidi.
Habari nyingine tofauti imedai kuwa Sanchez hajafurahia tabia ya Arsenal kipindi chote cha majira ya joto na yupo tayari kufanya mgomo, ingawa Arsene Wenger alitia maji madai hayo akisisitiza Ijumaa kwamba mchezaji huyo bado ana mapenzi na klabu kwa asilimia mia moja.
No comments:
Post a Comment