tuwasiliane

Saturday, December 24, 2011

24 DEC. MILOVAN APATA KIBALI CHA KUFANYIA KAZI


KOCHA wa Simba ya Dar es Salaam, Milovan Cirkovic, amepata kibali cha kufanya kazi nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa hatua hiyo ni furaha kwa mashabiki wa Simba kuomba sasa apewe ushirikiano wa kutoka.

“Klabu inapenda kutumia nafasi hii kushukuru Idara ya Uhamiaji, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla kutokana na ushirikiano wa hali ya juu uliooneshwa katika kipindi cha kushughulikia suala hili.

“Kwa taarifa hii, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wanatoa wito kwa wadau, mashabiki na vyombo vya habari kumpa nafasi Milovan ili sasa apate fursa ya kuutumia ujuzi wake wa hali ya juu kwenye kuimarisha soka la Tanzania,” alisema Kamwaga.

Alieleza kuwa leseni yake ya ukocha alionayo Milovan ndiye atakuwa kocha wa kiwango cha juu zaidi anayefanya kazi nchini kwa sasa.

Wakati huohuo, Kamwaga alisema mechi ya Simba na timu ya Eskom ya Malawi iliyokuwa ifanyike Jumapili sasa itachezwa Jumatatu ijayo.

“Mabadiliko haya yametokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam ambazo zimeathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu, wakiwamo wapenzi wa kandanda na pia Uwanja wa Taifa wenyewe ambako mechi ilipangwa kuchezwa.

“Simba pia inapenda kutoa salamu za pole kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na mvua hizo za Dar, Mara na Mbeya na iko pamoja na wote walioguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine,” alisema

No comments:

Post a Comment