
MAKOCHA wa kigeni wanaofundisha timu za Yanga, Simba na Azam sasa wanatakiwa kuomba kibali toka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kuendelea kuzinoa timu zao.Yanga na Simba zinafundishwa na Waserbia, Kostadin Papic na Milovan Cirkovic, huku Azam ikifundishwa na Stewart Hall raia wa Uingereza.
Katika sheria mpya ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), inaeleza makocha wote wa kigeni ni lazima wapate kibali maalum cha kufanya kazi toka CAF.
Akizungumza na gazeti hili, Mkufunzi wa CAF na Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Shirikisho la Soka la Zambia, Honour Janza alisema hivi sasa CAF ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha leseni wanazotoa kwa makocha Afrika zinatambuliwa na UEFA.
Pia wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) ili kudhibiti makocha kutoka Ulaya na Marekani kumiminika Afrika kwa kuweka sheria ambazo watalazimika kuzifuata na kupata vibali cha CAF.
"Kuna kasumba ya nchi nyingi za Afrika kuchukua makocha toka Ulaya, mpango wa CAF sasa ni kuhakikisha makocha wa Afrika wanapata fursa ya kufundisha nchi yoyote duniani na ndio maana tunazungumza na FIFA ili leseni zetu zitambuliwe na UEFA.
"Kwa makocha ambao wapo tayari hapa Tanzania hata kama wana leseni ya daraja B (UEFA) ni lazima wafanye utaratibu wa kuomba kibali CAF ili waweze kuendelea na ajira zao, sheria hii inafanyiwa kazi ikikamilika itaanza kutumika mara moja," alisema Janza.
"Hali kadhalika kwa makocha wa Tanzania na Afrika kwa jumla mpango huu utasaidia makocha wenye leseni za CAF kwenda kufundisha soka popote duniani, kikubwa ninachowaasa makocha wa Tanzania wasijifunge hapa nchini tu watoke wasake ajira kila mahali wawe na moyo wa kujituma na kujiendeleza kila wakati."
Janza alisema hayo wakati akifunga kozi ya siku nne ya makocha kwenye Uwanja wa Taifa.Alisema zaidi: "Kocha ni lazima aende na wakati kwa kujua mbinu mpya za kufundisha soka kwa kusoma.
"Kama mnataka maendeleo makocha wasijifunge, mfumo wa ufundishaji mpira unabadilika kila siku, ni lazima wasome kozi za muda mfupi, mitandao na wajue CAF wanachofanya kwa wakati,"alisema Janza.
"Maendeleo ya soka hutokana pia na uwapo wa makocha bora, hivyo ni lazima makocha wajue sheria 17 za mchezo wenyewe na mbinu mpya ili kukuza uelewa wa soka la kisasa."
Alisema nchi nyingi za Afrika zimelala ndio maana soka lao limedumaa tofauti na Ulaya na kwamba CAF wamegundua hilo na ndio maana wametoa mapendekezo ya kutaka mabadiliko
No comments:
Post a Comment