tuwasiliane

Saturday, December 24, 2011

24 DEC, Sintah, Kajala wamaliza bifu

MSANII wa filamu Bongo, Husna Poshi ‘Dotnata’, juzikati aliingia tena kwenye kibarua kizito cha kuondoa bifu kati ya mastaa wa sinema, Christina Manongi ‘Sintah’ (pichani) na Kajala Masanja, Risasi Jumamosi ni shuhuda.

‘Mkutano’ wa usuluhishi ulifanyika Desemba 20, mwaka huu ndani ya Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dar es Salaam ambapo mastaa hao walikutana ‘laivu’ kwenye kikao cha maandalizi ya harusi ya Mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beats cha Star TV, Sauda Mwilima.

Katika kikao hicho, mastaa hao walinuniana kiasi cha kushindwa kusalimiana.

Hali hiyo ilimsukuma Dotnata kuwaita mara baada ya kikao na kuwasuluhisha ingawaje iliwachukua muda mrefu kwa wasanii hao kuchukua uamuzi huo.

Akizungumzia ishu hiyo kwa paparazi wetu, Dotnata alisema kuwa, katika kazi ya usuluhishi iliyowahi kuchukua muda mrefu ni pamoja na ugomvi wa mastaa hao.

“Nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu wote, namshukuru Mungu nimefanikiwa na wameahidi kutokwaruzana tena kwa chochote,” alisema Dotnata.
Paparazi: “Kwani ugomvi wao mkubwa ni nini?”
Dotnata: “Mh! Naomba hilo tuliache kwa sasa.”


SOURCE GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment