
HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamethibitisha kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi litaloanza Januari 2 huko Zanzibar.
Yanga iliyokuwa kisuasua kuhusu ushiriki wake kwenye michuano hiyo kwa kutoa sababu mbalimbali kabla ya jana kuthibisha hilo. Katibu Mkuu wa Yanga, Celestin Mwesigwa alisema ni lazima kwa timu yake kushiriki kwenye michuano hiyo ya mapinduzi.
Mwesigwa alisema awali walishindwa kutoa maamuzi kwa kuwa barua ya mwaliko ya kushiriki michuano hiyo ilichelewa kuwafikia."Tulipokea barua ya mwaliko kutoka ZFA (Shirikisho la Soka Zanzibar) Jumamosi na leo 'jana' imejadiliwa hivyo timu yetu itashiriki mashindano hayo," alisema Mwesigwa.
Timu hiyo ni miongoni mwa timu nane zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayoanza Januari 2 hadi12 siku ya kilele cha sikukuu hiyo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyotokea miaka 49 iliyopita.
Timu zitakazoshiriki mashindano hayi ni pamoja na mabingwa watetezi Simba, Azam na Yanga zote za Tanzania Bara, nyingine ni Jamhuri ya Pemba, Mafunzo, Miembeni United, Super Falcon na Kikwajuni zote za Visiwani.
No comments:
Post a Comment