
TIMU za Simba na Yanga zimewasilisha usajili wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya mashindano ya kimataifa mwakani, huku wachezaji Artif Amour wa Yanga na Ulimboka Mwakingwe wa Simba majina yao yakiwa hayapo.
Artif Amour mchezaji chipukizi aliyeripotiwa kukulia kwenye timu ya watoto ya Arsenal, ambayo timu yake ya wakubwa inashiriki Ligi Kuu England ni moja ya wachezaji waliopambwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa wana uwezo mkubwa, lakini jina lake halipo kwenye orodha ya Yanga iliyowasilishwa TFF.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alithibitisha jana kuwa wamewasilisha majina 28 TFF ili yatumwe makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya ushiriki wa Ligi ya
Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itacheza na Zamalek ya Misri hatua ya awali.
“Tumewaacha Artif na Zuberi Ubwa, lakini wengine wote yameenda hata Rashid Gumbo ambaye baadhi ya magazeti yaliandika ameachwa, jina lake tumelipeleka,” alisema Sendeu.
Wachezaji ambao majina yao yamewasilishwa TFF kuombewa usajili Yanga kwa mujibu wa chanzo chetu ni Nadir Haroub, Shadrack Nsajigwa, Kigi Makasy, Jerry Tegete, Chacha Marwa,
Juma Seif, Bakari Mbegu, Abuu Ubwa, Shamte Ally, Nurdin Bakari, Hamis Kiiza na Keneth Asamoah.
Wengine ni Yaw Berko, Idrisa Rashid, Haruna Niyonzima, Shaaban Hassan, Said Mohammed, Rashid Gumbo, Pius Kisambale, Godfrey Taita, Oscar Joshua na Stephano Mwasika, Omega Seme, Godfrey Bonny, Ibrahim Job, Salum Telela na Athumani Idd. Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kwenye taarifa yake jana kuwa Simba na Yanga tayari zimewasilisha usajili wao na kwamba Simba iliwasilisha wachezaji 24 na Yanga 28.
“Mwisho wa kufanya usajili ni Desemba 31 mwaka huu na kila klabu inaruhusiwa kusajili hadi wachezaji 30. Hata hivyo Agosti mwakani kutakuwa na usajili wa dirisha dogo kwa timu
ambazo hazikumaliza nafasi zote 30,” alisema Wambura ambaye hakutaja majina yaliyowasilishwa TFF.
Hata hivyo, akizungumza baadaye jana na gazeti hili, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wamewasilisha wachezaji 25 na kwamba kulitokea tatizo la kiufundi, hivyo jana
walipeleka barua TFF kurekebisha hali hiyo.
“Ni majina 25 tuliyopeleka, kuna tatizo lilijitokeza, tayari tumeliweka sawa, “ alisema Kamwaga ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina yaliyopelekwa TFF wala walioachwa.
Lakini habari zilizopatikana kutoka ndani ya klabu ya Simba zilieleza kuwa wachezaji Rajabu Isihaka na Ulimboka Mwakingwe majina yao hayamo kwenye usajili huo wa CAF.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ndani ya Simba, orodha kamili iliyotumwa TFF kwa ajili ya kupelekwa Caf ni makipa: Juma Kaseja, Ally Mustapha na William Mweta.
Mabeki ni Nassoro Said, Derick Walulya, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Juma Jabu, Victor Costa, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Obadi Mungusa na Hassan Khatib ambaye amepandishwa
kutoka kikosi cha pili cha Simba.
Viungo; Mwinyi Kazimoto, Machaku Salum, Uhuru Selemani, Patrick Mafisango na Haruna Moshi.
Abdalla Seseme, Frank Senkule, Ramadhan Singano na Jonas Mkude wametoka kikosi cha pili.
Washambuliaji ni Gervas Kago, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na Edward Cristopher aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili.
No comments:
Post a Comment