

MIAMBA ya soka ya Zambia, Zanaco na Power Dynamos wanatarajia kuja nchini kwa ziara ya kimichezo ambapo watavaana na Simba na Yanga.
Timu hizo zinakuja nchini kwa mwaliko wa Klabu ya Michezo ya Kemramba ya Musoma, Mara na Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (Kifa) na zikiwa hapa zitacheza mechi mbalimbali za kirafiki jijini na mikoani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Charles Changarawe, Zanaco watakuwa wa kwanza kuwasili Desemba 29 wakiwa na wachezaji watano wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.
Changarawe ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Kifa ambao wanaratibu ziara ya Dynamos
alisema timu hizo zimepangiwa kuvaana na Simba na Yanga kabla ya mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza.
Mkurugenzi huyo alisema Desemba 31 miamba hao watakutana na vinara wa Ligi Kuu Simba jijini kabla ya kuvaana na Yanga siku inayofuata.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya timu ya Zanaco, watavaana na Toto Afrika ya Mwanza jijini humo Januari 8 na pia kucheza Arusha, Musoma, na Mbeya kabla ya kurejea Zambia Januari 18.
Dynamos ambao wanatarajia kuwasili nchini Januari 5 watavaana na Simba Januari 7 na
siku inayofuatia watakutana na Yanga kabla ya kuanza ziara za mikoani ukiwepo mkoa wa
Arusha, Mwanza, Sinyanga na Musoma, Mbeya na kurejea kwao Januari 24.
No comments:
Post a Comment