tuwasiliane

Tuesday, December 27, 2011

27 DEC. KHADIJA KOPA ALIVYOPAGAWISHA MASHABIKI UGIRIKI


MALKIA wa mipasho (taarab) nchini, Khadija Kopa, aliwapeleka ‘mbaya’ mashabiki wa Tanzania waishio katika jiji la Athens, Ugiriki, alipoangusha vitu vya uhakika katika ukumbi wa Axum.

Mashabiki waliofurika ukumbi huo ni pamoja na wananchi wa Afrika Mashariki ambao ni kutoka Kenya na Uganda.

Moja ya vivutio vya burudani hio alikuwa ni kijana anayechipukia kwa miondoko hiyo ya ‘rusha roho’ ajulikanaye kwa jina la muziki kama Michael Jackson ambaye jina lake halisi ni Juma Ramadhani. Msanii huyo alishirikiana na ‘mdada’ mmoja wa nguvu ambaye aliweza kuzimiliki vyema nyimbo za malkia mwingine wa taarabu nchini Bongo, Aisha Ramadhani aka Mashauzi.

Ilikuwa ni burudani tosha licha ya kwamba nchi yenyewe ya Ugiriki imekumbwa na matatizo ya kiuchumi, ambapo uchumi wake unatishia kuyumbisha maisha ya wananchi wake.

No comments:

Post a Comment