tuwasiliane

Saturday, December 24, 2011

24 DEC .Taifa Stars yaitwa Misri


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imealikwa kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Misri Februari mwakani.

Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Angetile Osiah alisema wamepokea barua ya mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Misri (EFA) juzi na wamejibu kuthibitisha kukubali mwaliko huo.

Alisema Misri imeomba kucheza mechi hiyo kati ya Februari 19 na 20 ama 23 na 24, lakini alisema wao wamewaandikia kuomba wacheze kati ya Februari 23 na 24.

Osiah alisema shirikisho la nchi hiyo litagharamia gharama zote za timu ya taifa kuanzia tiketi, malazi na gharama nyingine za mechi hiyo.

Alisema mechi hiyo ya kirafiki ni fursa nzuri kwa timu ya taifa kujiandaa na mashindano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Tanzania inayoshika nafasi ya 137 na Misri inayoshika nafasi ya 31 kwa ubora wa viwango vya
shirikisho la soka la kimataifa (Fifa) zote zimeshindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika
zikatakazofanyika kwenye nchi za Gabon na Guinea Ikweta mwakani.

Wakati huo huo, TFF imekataa mwaliko wa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kutaka timu ya
soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kucheza na timu ya soka ya Zanzibar kwenye maadhimisho ya sikukuu ya Mapinduzi ZanzibarJanuari 2 mwakani.

Akitoa msimamo huo jana, Osiah alisema Kilimanjaro Starshaitacheza mchezo huo kwa
sababu wachezaji wake wengi wanaounda timu hiyo watakuwa kwenye timu za Azam, Simba na
Yanga ambazo pia zitashiriki mashindano hayo.

Pia Osiah alisema hata Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Charles Boniface atakuwa na timu ya soka ya taifa ya wanawake(Twiga Stars) ambayo inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika dhidi ya Namibia mwakani.

Januari mwaka huu, Taifa Stars ilikuwepo jijini Cairo Misri kwenye mashindano ya Nchi za
Bonde la Mto Nile iliyoshirikisha saba, ambapo Taifa Stars mchezo wa ufunguzi ilifungwa mabao 5-1 na wenyeji

No comments:

Post a Comment