tuwasiliane

Saturday, June 29, 2013

Moyes ataka kumsajli Baines

 
Klabu ya Everton, imekata ombi lililowasilishwa na Manchester United la kutaka kumsajili mlinda lango wake Leighton Baines kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili.

Kocha mpya wa Manchester David Moyes ambaye alisajiliwa hivi majuzi kutoka kwa klabu hiyo ya Everton alitaka kumasjili mchezaji huyo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Siku chache tu baada ya kusajiliwa kama kocha wa Manchester United Moyes, alitangaza wazi wazi kuwa nia yake kuu ni kumsajili mechaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na minane.

Ripoti zinasema Manchester United inajianda kuwasilisha ombi lingine baada ya kuongeza fedha za kumsajili.
Hata hivyo, wasimamizi wa Everton, wamesema kuwa hawana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.

Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez kwa upande wake amesema anataka mchezaji huyo ambaye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita kusaini mkataba mpya.

Uamuzi huo wa Moyes wa kutaka kumsajili, Baines, huenda ukahujumu nafasi ya mcheza kiungo wa Manchester United Patrice Evra mwenye umri wa miaka thelathini na miwili.

Thursday, June 27, 2013

THE GIRL OF MY DREAM


ZINEDINE ZIDANE ATEULIWA KOCHA MSAIDIZI WA REAL MADRID - ATAMBULISHWA PAMOJA NA CARLO ANCELOTTI


Real Madrid wamemtambulisha rasmi kocha wao mpya Carlo Ancelotti na pia wametangaza kwamba Zinedine Zidane na Paul Clement watakuwa ndio makocha wasaidizi.

Ancelotti alitambulishwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na raisi wa klabu hiyo Florentino Perez mapema leo mchana.
 
Ancelotti atasaini rasmi mkataba wa miaka mitatu na Madrid July 3 akitokea Paris St Germain.

Wednesday, June 26, 2013

Ancelotti prefers Suarez to Cavani at Madrid


Suarez Real Madrid
New Real Madrid Carlo Ancelotti wants Luis Suarez to join him at the Bernabeu. The Italian sees the Liverpool striker as a cheaper option to Edinson Cavani.

 Source: Daily Star

Done Deal;Arsenal yakamilisha dili la £22m kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuain


 Higuain Arsenal Double Deal


Arsenal yakaribia kuthibitisha kumsajili mshambuliaji waf Real Madrid Gonzalo Higuain kwa £22million, Chanzo chatu kinajua.
Muanjentina huyo amekuwa gumzo katika tetesi za usajili katika kipindi hiki cha kiangazi , kwani amekuwa akigombaniwa na Arsenal and Juventus tangu awekwe sokoni na miamba  ya Spain
.
Mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 25 ana rekodi nzuri ya ufungaji kwani ameweza kufunga magoli, 122  katika michazo 266 , he has found himself somewhat out of favour in recent times, and looks to be part of a summer clear-out at the Bernabeu as they look to re-shape their squad for a renewed challenge on La Liga next season.
Other players such as Karim Benzema, Luka Modric and Angel Di Maria could also leave the club as they look to raise cash for some big-name transfer targets this summer, which include Tottenham’s £85million-valued winger Gareth Bale, and £50million Uruguayan strike pair Edinson Cavani and Luis Suarez, of Napoli and Liverpool respectively.
Arsenal have looked to capitalise on Higuain’s availability, as they are still in need of a top class striker to replace Robin van Persie, who left the club in a shock move to Manchester United last summer. Olivier Giroud and Lukas Podolski have done reasonably well to replace the Dutchman, but Arsene Wenger is still keen to bring in a more clinical finisher to be first choice upfront, and has also been linked strongly with Fiorentina frontman Stevan Jovetic for the last few months.
A move for the Montenegro forward looks to have fallen through, with the likes of Chelsea and Manchester City also keen on him, and this has seen Arsenal move quickly to wrap up a deal for Higuain.
The move should now be finally confirmed as the Spanish giants have now officially appointed PSG’s Carlo Ancelotti as their new manager, and the Italian is expected to give the move the green light as he looks to put his own stamp on the squad he inherits from Jose Mourinho.
Higuain will become Arsenal’s record signing at £22million, and signals a strong change in approach in the transfer market from Wenger, who had previously focused on bringing in lesser-known young players on the cheap, though these methods did not bring success to the Gunners, who have not won a trophy since the FA Cup in 2005.
The arrival of Higuain, following another big-name deal last year in Santi Cazorla, will show a real statement of intent from Arsenal to get themselves back into the thick of a serious title challenge, and with some signs of improvement defensively in 2012/13, a more regular goal-scorer could be just what the Gunners need to get themselves closer to their title rivals.

Rooney afikiria kutimkia Barcelona

Mshambuliaji wa Manchester United  Wayne Rooney afikiria kwenda Barcelona iwapo atataka kuondoka  Old Trafford. Rooney amesema kuwa Machampioni wao wa Spain ndio chaguo lake la kwanza na anataka kufanya mazungumzo na boss wake mpya David Moyes.
Source: The Sun

Tuesday, June 25, 2013

Cruyff: Barcelona inabidi imuuze Messi kwa kuwa tayari wana Neymar

 Cruyff: Barcelona should sell Messi now they have Neymar
The Netherlands legend believes the Catalans have created a potential conflict of interest within the squad by signing the Brazil starlet to play alongside the Argentine
Barcelona icon Johan Cruyff feels the Catalans should consider cashing in on Lionel Messi now they have brought Neymar on board.

The Liga champions signed Neymar in a deal worth €57 million earlier this summer and Cruyff envisages problems following the former Santos star's arrival.

Neymar "With Neymar on board, I would have planned for the possibility of selling Messi. Some would agree with me and others would not," Cruyff told Marca.

"Neymar's arrival could cause problems. Just look at free kicks for example. Neymar is very good at taking them. And Messi has already shown he is great, too. Who's going to take them...

"Or the fact that Neymar and Barcelona are with Nike while Leo is with Adidas. These are situations that could cause problems.

"You are talking about a team, its players, the things around it. There are too may things at stake. That's why it's so difficult to manage such a top class squad.

Lionel Messi "Neymar is talented, but we will have to wait and see how he gets along with the rest of the squad. I would not have taken the risk of bringing in Neymar."

Messi has a contract with Barcelona until June 2018, while Neymar recently inked a five-year deal, too.

Juventus yakubali kumsajiliTevez kutoka Manchester City

Juventus have agreed a deal with Manchester City to sign striker Carlos Tevez. The Argentine will cost €9 million (£7.6m) potentially rising to €12m (£10.2m)
Source: Sky Sport Italia

Mzee Mandela bado yuko hali mahututi

 
Rais mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.
Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

.MSHIRIKI WA TANZANIA AFANYA MAPENZI NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER

 

Mshiriki wa  kiume   wa  Tanzania, Nando  ametutia  aibu  baada  ya  uvumilivu  kumshinda  na  kuamua  kufanya  tendo la  ngono  hadharani  akiwa 
katika  jumba  la  big  brother. hatutaweka  video hiyo kutokana na  kuwa kinyume na maadili mema kwa jamii yetu ya kitanzania

Hali ya wasiwasi kuhusu afya ya Mandela

 

Wananchi wa Afrika Kusini hii leo wamekuwa na wasiwasi baada ya rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kutangaza kuwa hali ya afya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri sana.
Asubuhi waliamkia kwenda kazini wasijue taarifa watakazopokea hii leo baada ya rais Zuma kutoa taarifa hiyo.

Taarifa kutoka ikulu ya rais zilisema Jumapili jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni.
Afisaa mmoja mkuu alisema kuwa raia wa Afrika Kusini wasiwe na matumaini kupita kiasi.
Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94,alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.

Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.

Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu.
Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela 

KAPOMBE KUWA MWAFRIKA PEKEE FC TWENTE YA UHOLANZI MSIMU UJAO, ASUBIRIWA KWA HAMU ENSCHEDE

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Shomary Kapombe anaweza kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee Mwafrika kwenye kikosi cha FC Twente ya Ligi Kuu ya Uholanzi msimu ujao, iwapo atapasi majaribio yake katika timu hiyo hivi karibuni. 

FC Twente imeandika katika tovuti yake kwamba wakati wowote kuanzia sasa, Kapombe anayetumika kama beki wa kushoto siku hizi, atakuwa huko kwa majaribio. 

Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992 aliibukia katika klabu ya Polisi Morogoro kabla ya kujiunga na Simba SC miaka mitatu iliyopita ambako anatarajiwa kumalizia Mkataba wake Desemba mwaka huu.

Twente imejiridhisha klabu yake imekubali kumpa ruhusa kwenda kufanya majaribio nchini humo. “Tumepewa ruhusa kumuita kwa majaribio Ulaya na tunamtakia mafanikio,”imesema taarifa katika tovuti ya Twente, ambayo kwa sasa haina mchezaji Mwafrika kwenye kikosi chake cha kwanza.

Kapombe mwenyewe ameonyesha nia thabiti ya kucheza Ulaya na amekuwa akikataa ushawishi wa timu nyingine za Tanzania zinazotaka kumng’oa Simba SC kama Yanga na Azam FC ili kusikilizia nafasi ya Ulaya.

FC Twente maskani yake yako Enschede, ikicheza Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie na ilianzishwa mwaka 1926. Hawa ni mabingwa wa Kombe la KNVB na Johan Cruijff Schaal mwaka 2011, na wamekuwa mabingwa wa Eredivisie msimu wa 2009–2010.

Timu hiyo, inayotumia Uwanja wa nyumbani wa De Grolsch Veste tangu 1998,  pia imeshika nafasi ya pili mara tatu Eredivisie na walikuwa pia washindi wa pili wa Kombe la UEFA msimu wa 1974–1975 na kwa ujumla wametwaa Kombe la KNVB mara tatu.

Tanzaniaans International Shomari Kapombe op proef bij FC Twente

Tanzaniaans International Shomari Kapombe op proef bij FC Twente

FC Twente krijgt binnenkort waarschijnlijk de Tanzaniaan Shomari Kapombe op proef. Kapombe is een linksback die momenteel uitkomt voor Simba SC dat in eigen land Ă©Ă©n van de twee topclubs is. De melding wordt gedaan door Tanzania Soccer. Kapombe is zesvoudig international en wist Ă©Ă©n keer te scoren voor Tanzania. Hij zal ook bij andere clubs stages af gaan werken.
Shomari Kapombe is geboren op 28 januari 1992 in Tanzania. Hij kwam enkele seizoenen gelden van de Tanzaniaanse club Police Morogoro Football Club over naar Simba SC. Hier heeft de back nog een contract tot eind december 2013.
Zijn club Simba SC geeft de jongeling toestemming om zijn geluk te gaan beproeven in het buitenland. “We hebben groen licht gegeven om stages te gaan lopen in Europa en wensen hem heel erg veel succes. We verwachten hem na de stages wel terug om aan de voorbereiding met Simba SC deel te nemen.”
Kapombe zelf is zeer gemotiveerd en ziet een carrière in Europa als een grote droom.

Sunday, June 23, 2013

MWALIMU SAID MPEMBENUE,AKAMILISHA NUSU YA UISLAM JANA



JANA ILIKUWA SIKU YA FURAHA KWA MWL SAIDI MPEMBENUE,BAADA YA KUFUNGA NDOA NA BI HADIJA KUNDUMU,SHEREHE YA HARUSI ILIFANYIKA KWNYE UKUMBI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO KILOSA
 

Friday, June 21, 2013

SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU ( MOSES MACHALI) AKIWA DODOMA JANA JIONI


Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana  jioni  mjini Dodoma.

Tukio hilo lilitokea jana jioni  wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita ....

Kitendo hicho  kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni ....

Baada ya kushuka,  vijana hao walimtolea  matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanza.

Shuhuda  aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema  Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.

Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu. 

source.the choice

Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.
"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO


Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo 
amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

Thursday, June 20, 2013

KIPONZO CHA LEO

Thamani ya Kiemba Sh500 mil

 

Wakati Simba ikiendelea kusotea pesa za kuuzwa Emmanuel Okwi klabu ya Etoile du Saleh ya Tunisia, klabu hiyo imesema mpango wake wa kumpiga bei kiungo, Amri Kiemba kwenda Raja Casablanca ya Morocco utatimia iwapo klabu hiyo itakubali kutoa siyo chini ya Sh500 milioni.

Raja Casablanca imepiga hodi Msimbazi kutaka kumsajili Kiemba baada ya kuvutiwa naye wakati walipomwona akiichezea Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Morocco zaidi ya wiki moja iliyopita.
Akizungumza na chanzo chetu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspope alisema, kiwango hicho cha fedha ndiyo thamani ya sasa ya Kiemba.
“Tayari tumezungumza na Raja Casablanca na kweli wameonyesha nia ya kumtaka Kiemba, lakini kwetu hakuna namna yoyote ya kumtoa bila Sh500 milioni kuwekwa mezani,” alisema Hanspope.
“Nilipokwenda kwao (Morocco) Rais wa klabu alikuwa Uturuki, tunasubiri arejee ili tuwatumie mchanganuo mzima wa mauzo ya Kiemba,” alisema.
Hanspope, alisema angependa kuona klabu yake inafanya biashara ya kuwauza wachezaji kwa faida. Tunatakiwa kuwalipa makocha, kuingia mikataba na wachezaji, mambo yote haya yanahitaji pesa. Hatuwezi tena kufanya biashara isiyo na faida kwa upande wetu,” alisema zaidi bosi huyo.

source; mwananchi

Wednesday, June 19, 2013

HUU NDO UKWELI KUHUSU KUWEPO KWA TAARIFA KUA SAIDA KAROLI KAFARIKI KATIKA AJALI YA MAJI ZIWA VICTORIA

 

Jana  kumekuwepo na taarifa kutoka kwa mwanahabari, Frederick Katulanda kupitia kundi pepe la majadiliano la MabadilikoTanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki aliyekuwa maarufu Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia leo hii katika ajali ya kuzama kwa boti.

Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.

Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.

Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”

source;udakuspecially

Mh. Sugu apata ajali akielekea Arusha. Gari lake lagongana uso kwa uso na basi la abiria

 sugu-joseph-mbilinyi

Kwa mujibu wa eddymoblaze blog na vyanzo vingine mbalimbali, mbunge wa Mbeya mjini, Mh. Joseph Mbilinyi “Sugu” amepata ajali ya barabarani wakati akielekea Arusha.
Ripoti hizo zinasema kuwa gari la Mh. Mbilinyi limegongana uso kwa uso na basi la abiria.
Ajali hiyo imetokea katika wilaya ya Hanang’, na taarifa hizo zinasema Sugu hajadhurika kwenye ajali hiyo.

Monday, June 17, 2013

TAIFA STARS NA IVORY COAST WAINGIZA MILLIONI 500,PAULSEN ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA UGANDA

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
 
 
wakati huo huo;
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

Sunday, June 16, 2013

http://www.fifa.com/worldcup/preliminaries/africa/standings/index.html








































SAFARI YA BRAZIL MWAKANI KWA TANZANIA,YAISHIA TAIFA


IVORY Coast imefanikiwa kusonga hatua ya pili na ya mwisho katika kuwanai tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Tanzania mabao 4-2 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi C kanda ya Afrika.

Kwa ushindi huo, Ivory Coast imetimiza pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa itasubiri kucheza na mmoja wa washindi wengine wa makundi mengine tisa ili kuwania kwenda Brazil mwakani.
Tanzania inabaki na pointi zake sita, huu ukiwa mchezo wa kwanza kufungwa nyumbani katika kampeni hizi na Morocco bila kuhusisha matokeo yake na Gambo, ina pointi tano.  
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mehdi Abid aliyesaidiwa na Hamza Hammou, Bauabdallah Omar wote kutoka Algeria, hadi mapumziko Ivory Coast tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-2.
Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mfungaji Amri Ramadhani Kiemba dakika ya kwanza tu aliyepokea pasi ya Mbwana Ally Samatta kufuatia mpira wa kurushwa na Erasto Edward Nyoni kusababisha kizazaa langoni mwa Tembo wa Abidjan.

Nyoni alirusha kama amepiga kwa mguu karibu kabisa na kibendera cha kona kufuatia beki Suleiman Bamba kumpitia Thomas Ulimwengu na kutoa nje na mpira ukaokolewa kabla ya kumkuta Samatta aliyempelekea mfungaji.

Ivory Coast wakasawazisha bao hilo dakika ya 15 kupitia kwa Lacina Traore baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa na Yaya Toure akafunga la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 23, nje kidogo ya eneo la hatari. Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Stars kupanga ukuta wao vibaya na kumpoteza maboya kipa wao, Juma Kaseja.

Stars ilirudi mchezoni na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 35 mfungaji Ulimwengu aliyeunganisha krosi maridadi ya Shomary Kapombe. Hata hivyo, Ivory Coast wakapata penalti rahisi baada ya Gervinho kujiangusha wakati anakabiliana na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Yaya Toure akaenda kumtungua Kaseja dakika ya 43.

Kipindi cha pili Stars ilikianza vizuri na kushambulia mara nyingi langoni mwa Ivory Coast, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen dakika ya 87 kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza mshambuliaji Vincent Barnabas yaliigharimu Tanzania kwa kufungwa bao la nne na kupotea kabisa mchezoni. Baada ya kutoka Kazimoto, aliyetekeleza majukumu yake vizuri leo, Ivory Coast wakatawala sehemu ya kiungo na kutengeneza bao la nne lililofungwa na Bonny Wilfred dakika ya 88.
Pamoja na kufungwa, Stars ilicheza soka safi ya kuvutia na mabao yote yalitokana na makosa – na si kuzidiwa uwezo. 

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk 85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto/Vincent Barnabas dk 87, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.
Ivory Coast; Boubakar Barry, Arthur Boca, Didier Zakora, Solomon Kalou/Sio Giovanni, Gervais Yao, Jean Jarques Gosso Gosso, Alain Aurier, Lacina Traore/Bonny Wilfred, Yaya Toure, Geoffrey Serey na Suleiman Bamba/Nori Koffi Christian. 

POLE YA DOCTA SLAA KWA WATU WA ARUSHA

 
Wana Arusha,

Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha.

Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile.

Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi.

TAIFA STARS KUWA NA MABADILIKO KIDOGO LEO

 
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameweka wazi kuwa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ atacheza badala ya Aggrey Morris wakati Mwinyi Kazimoto akiziba pengo la Mrisho Ngassa.

Morris atakosa mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania mchujo wa Fainali za Kombe la Dunia Brazili 2014.
Beki huyo wa kati anayekipiga na klabu ya Azam FC anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye pambano la marudiano dhidi ya Morocco mjini Marrakesh. Stars ikilala mabao 2-1.
Kwa upande wa Ngassa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano alizopewa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ivory Coast. Stars ikilala mabao 2-0 na ya pili akilimwa pambano la Morocco. Stars ikifungwa mabao 2-1.
Kim alikiambia chanzo chetu jana jijini Dar es Salaam kuwa nafasi ya Morris atacheza Cannavaro wakati akilazimika kumtumia Kazimoto kucheza nyuma ya Thomas Ulimwengu, huku Amri Kiemba akicheza winga ya kulia.
“Nafasi ya Morris atacheza Cannavaro. Pia, nitambadilisha Kazimoto kucheza nyuma ya Ulimwengu wakati Kiemba atacheza pembeni, winga ya kulia.” alisema Kim na kuongeza.
“Nafikiri kukosekana kwao hakuwezi kuathiri timu kufanya vizuri.” alisisitiza.

BOMU LAJERUHI NAKUUA WAFUASI WA CHADEMA ARUSHA,UCHAGUZI WASOGEZWA MBELE





. Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.

Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.
Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.

Watu walioshuhudia tukio hilo walikiambia chanzo chetu kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.
Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.
Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani.

Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.

Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki.

Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo.


Miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo la mlipuko wa bomu ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Selian.

Mbowe akizungumza katika hospitali ya Selian jana aliwataka wanachama wa chama hicho watulie kwa sababu tukio hilo ni kubwa na lina mambo mengi ndani yake.

Alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha kuwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo wanapata matibabu kwanza.
Mbowe aliwataka watu wote waliopotelewa na ndugu kufika katika hospitali zote za mji wa Arusha kutambua ndugu zao waliojeruhiwa.

Alisema Chadema itagharimia matibabu ya watu wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Mbowe alisema chama chake kwa sasa hakiwezi kutoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo la bomu kwa sababu wanafuatiliwa na baadhi ya askari polisi na maofisa wa Usalama wa Taifa.

Katika hospitali ya Selian, Mganga wa zamu, Dk Ekenywa alisema kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 25 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.
Waandishi wa habari walishuhudia baadhi ya wanachma wa Chadena pamoja na viongozi wao akiwamo Mbowe wakitoa damu kwa ajili ya majeruhi.

Awali Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alihitimisha kampeni kwa chopa katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli na kukumbana na mkutano wa kampeni wa CCM uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Edward Lowassa.
Viongozi hao, walifanya mikutano katika kata hiyo na kila chama kilitamba kushinda leo na kuwaondoa wananchi na hofu za kutokea vurugu.

Mbowe licha ya kufanya mkutano huo, pia alifanya mikutano katika Kata ya Kaloleni Uwanja wa Soweto mjini Arusha na mamia ya wakazi wa Arusha wa kata zote nne na mkoani Manyara, katika kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaofanyika katika kata mbalimbali nchini.
Uchaguzi mdogo wa kata nne za Jiji la Arusha na Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli, unatarajiwa kufanyika leo.

Uchaguzi wa Kata ya Makuyuni, unafanyika kuziba nafasi ya Diwani wa CCM, Abdilah Warsama aliyefariki dunia, kata nne za Jiji la Arusha, uchaguzi unafanyika kutokana na waliokuwa madiwani wa Chadema kufukuzwa uanachama kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.

Vyama vilivyosimamisha wanaogombea udiwani ni CCM, Chadema na CUF. Kwa upande wa CCM ni Emanuel Meliali (Kaloleni), Emmannuel Laizer (Elerai), Edna Jonathan Sauli (Kimandolu) na Victor Mkolwe (Themi) .

Chadema wanaogombea ni Melance Kinabo “Kaburu” (Themi), Emmannuel Kessy (Kaloleni), Jeremiah Mpinga (Elerai) na Rayson Ngowi (Kimandolu).

Kwa upande wa CUF waliosimamishwa kugombea ni Abbas Mkindi Darwesh (Kaloleni) John Bayo (Elerai) na Lobora Ndarvoi (Themi).

Kampeni

Kampeni za uchaguzi huo, mdogo, zilikuwa na upinzani mkubwa na kwa Jiji la Arusha, wakati Chadema, ilikuwa ikiongozwa na mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema, CCM iliwatumia vigogo wake wote wa juu wa chama hicho.

Vigogo hao waliokuwa Arusha ni Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba, Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdalah Bulembo.

Wengine waliokuwa Arusha ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwanri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen Wassira na wabunge kadhaa wakiongozwa na mbunge wa Simanjiro, Christopha ole Sendeka.

Kata ya Makuyuni

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema jana kuwa chama hicho, kina uhakika wa ushindi katika Kata ya Makuyuni na kata nne za Arusha.

“Tumefanya kampeni kwa amani na utulivu na nina imani ya ushindi mkubwa hasa hapa Makuyuni,” alisema Nangole.

Mbowe katika kata hiyo, jana alifanya mkutano mfupi baada ya kutua kwa chopa, akitokea mkoani Manyara


Sha
Mbowe aliwataka wakazi wa kata hiyo, wasiwe na hofu wajitokeze kupiga kura leo. Kwa upande wa Lowassa, ambaye ameweka kambi katika kata hiyo, pia alitoa wito kwa wakazi wa kata hiyo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura leo.

Kwa pamoja viongozi hao ambao walipishana muda mfupi, Mbowe akianza kupita na baadaye Lowassa kuhitimisha mkutano, kila mmoja alitamba chama chake kushinda leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nape alisema chama hicho kina imani na ushindi leo na alipongeza kampeni kuwa za amani.

“Tuna imani polisi wataimarisha ulinzi leo,” alisema Nape.

Nape jana jioni, alitarajiwa kuhitimisha kampeni mkoani Manyara.

Lema akizungumza katika mikutano jana, alisema wana imani Chadema itaibuka na ushindi katika kata zote.
 Wakati huohuo taarifa ambazo blog hii imezipata hivi punde, tume ya Taifa ya uchaguzi imeahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike leo katika kata 4 za jiji la Arusha hadi tarehe 30/06/2013 kutokana na machafuko yaliyotokea jana

Saturday, June 15, 2013

BREAKING NEWZ; WAFUASI WAWILI WA CHADEMA WAKATWA MAPANGA,KILOSA

Habari ambazo blog hii imezipata kutoka kijiji cha Miyombo kuwa wafuasi wawili wa Chama cha demokrasia na maendeleo wamekatwa mapanga usiku wa kuamkia leo hali zao sio nzuri. kutokana na maandalizi wa uchaguzi wa udiwani katika kata ya miyombo utakaaofanyika kesho hali ya vurugu imeripotiwa kutokea katika vijiji mbalimbali vya kata hiyo. tunafanya mawasiliano na kamanda wa polisi wa wilaya ya kilosa ili aweze kuthibitisha hili,.

endelea kufuatilia www.heavytalio.blogspot.com kwa habari zaid

Mtikila ashinda kesi ya 'ugombea huru' Mahakama ya Haki za Binadamu Africa

 Picha:Mtikila PNG.PNG



Arusha. Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.
Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa. 

MBWANA SAMATTA AENDELEA KUWAFUNIKA MASTAA WOTE TP MAZEMBE - ULIMWENGU NAE HAYUPO NYUMA

SAMATTA remains the key man
Kwa mujibu wa takwimu zilizotlewa na klabu ya TP Mazembe. kwa kutumia vigezo vya: Kucheza mechi, Pasi zilizozaa matunda na Mabao - mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu hiyo Ally Mbwana Samatta ameongoza kwa kipindi cha takribani miezi 2, April na May.

MECHI/MUDA WALIOCHEZA
Kwa kuzingatia muda wa kucheza, hakuna aliyeweza kutimiza michezo 13 ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mwezi May wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza walicheza mechi zote saba, wakati katika kuleta utofauti KASUSULA na SAMATTA walicheza mechi zote sita. Katika dakika walizocheza Samata tayari alikuwa anashika nafasi ya 3 nyuma ya Richard KISSI Boateng na Kasongo Kabiona.

Dakika walizocheza kwa namba: 1. KIDIABA na KASUSULA dakika 900.
3. SAMATTA 873
4. BOATENG 79
5. KABIONA 720
6. SINKALA 655
7. KIMWAKI na HICHANI 630
9. MPUTU 610
10. ASANTE 518
11. KALABA 512
12. ILONGO 475, 13. NKULUKUTA 447, 14. KABANGU 430, etc.

Mabao - Samatta anaongoza
Hakuna shabiki yoyte wa TPM anayeweza kushangazwa na mshambuliaji huyu wa kibongo kushika nafasi ya kwanza. SAMATTA amefunga mabao 6 ndani ya miezi mwili, akifuatiwa na Bokanga aliyefunga 5, Awako na Tresor Mputu wamefunga mabao 4 kila mmoja huku mshambuliaji mwingine wa kibongo Thomas Ulimwengu akifunga mabao 2.


Pasi za mabao: MPUTU anaongoza ...
Tresor MPUTU ameendelea kuwa mfalme wa pasi za mwisho ndani ya TP Mazembe. Lakini Samata hayupo mbali - anashika nafasi ya pili. 
Waliongoza: 1. MPUTU pasi 6 , 2. SAMATTA pasi 5, 
3. BOATENG 2, 6. ASANTE, BOKANGA, KABANGU, KASONDE, ADJEI, NKULUKUTA, ULIMWENGU kila mmoja alitoa pasi 1 ya goli.

ONYESHO LA JIDE NI KUFURU, HAKUNA PA KUKANYAGA, BURUDANI MURUWA

Lady Jaydee akimba wimbo mambo ya Fedha na Mh. Sugu

ONYESHO la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13 katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo katika eneo la maegesho ya magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu.
Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake.







Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo.
Kufika saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi.
Saa 5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado, Yeye, Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy katika awamu ya kwanza.
Baada ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani.
Jide alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu, lakini alisisimua mashabiki ile mbaya.

Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide.
Kutoka hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na kuurusha umati ile mbaya.

Wakati Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie.   

Nature kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake Ngwair apumzishwe kwa amani peponi.

Ndipo Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala, Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage. 
Wanaume walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa 
akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia.

Ikawadia zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee, baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi, Nikusaidiaje na Kamili Gado.

Watu kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa kukanyaga’.
Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa.
ssource; BIN ZUBERY

Friday, June 14, 2013

BREAKING NEWS; SERIKALI SASA YARUHUSU SIMBA NA YANGA ZIENDE SUDAN KUCHEZA KAGAME

SERIKALI imeziruhusu klabu za Simba SC, Yanga SC za Dar es Salaam na Super Falcons ya Zanzibar kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma asubuhi ya leo kusema wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.

Makalla amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko yanayoedelea Sudan.

Kufuatia tamko la Serikali kuziruhusu klabu hizo sasa ziende Sudan, sasa ni juu yao ya klabu hizo kuamua kwenda au kutokwenda.
Lakini Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Mkenya Nicholas Musonye amekwshatishia atazichukulia hatua kali klabu hizo zisipokwenda.

Juzi Serikali kupitia Makalla ilitoa tamko la kuzuia klabu za Tanzania kutokwenda Sudan kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo. 
Kufuatia tamko hilo, jana Yanga, ambao ni mabingwa watetezi kwa miaka miwili mfululizo, walitangaza kuvunja kambi yao hadi wiki mbili baadaye, wakati Kombe la Kagame linaanza kutimua vumbi Juni 18, mwaka huu.

Yanga wamepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na Vital 'O' ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda.

Katika michuano hiyo inayotarajiwa kufikia tamati Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.

Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo Juni 20 kwa kumenyana na Express, wakati Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-mereikh

TFF YATOA NOTISI YA MKUTANO MKUU


Boniface Wambura, I
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa notisi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho utakaofanyika Julai 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam ukiwa na ajenda moja ya marekebisho ya Katiba.

Notisi hiyo imetolewa juzi (Juni 12 mwaka huu). Rais ameitisha Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(1) ya Katiba ya TFF baada ya kupata maagizo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa barua yake ya Aprili 29 mwaka huu.

Ajenda rasmi na taarifa nyingine zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(4) ya Katiba ya TFF. Wanachama wa TFF ambao ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu wanatakiwa kutuma majina ya wajumbe halali.

TFF inapenda kuwakumbusha wanachama wake kutuma majina ya wajumbe halali ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano huo. Ni vizuri kuhakikisha kuwa jina linalotumwa ni la mjumbe halali wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya TFF.

Fastjet kutoa huduma za bei nafuu

 

Shirika la ndege, linalotoa huduma za usafiri wa ndege kwa bei nafuu Fastjet, limepata kibali cha kuanzisha safari za ndege za kimataifa za bei nafuu, kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini, Zambia na Rwanda.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na Stelios Haji-Ioannou, ambaye ni mmiliki wa shirika la ndege la Easyjet, lililo na makao yake barani ulaya.

Shirika hilo limetangaza kuwa litaanzisha safari za ndege katika mataifa hayo kwa bei nafuu huku abiria wakilipa dola mia moja pekee.
Kwa sasa shirika hilo linahudumia wasafiri nchini Tanzania pekee.

Raia wengi na hasa wafanya biashara wamefurahishwa na tangazo hilo, wakisema kuwa itapunguza gharama za usafiri na hivyo kuimarisha biashara katika kanda hiyo.

Nchini Kenya, shirika la ndege la Kenya Airways ambalo ni moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika, limepata pigo kubwa baada ya kupata hasara kubwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa shirika hilo lilipata hasara ya zaidi ya dola milioni mia moja kabla ya kutozwa ushuru, kiwango ambacho ndicho mbaya zaidi tangu mwaka wa 2009.
Shirika hilo lilikuwa maarufu sana kwa abiria wanaosafiri magharibi, mashariki, kusini na katika mataifa ya Afrika ya kati.

BREAKING NEWZ;Pellegrini ateuliwa kuwa bosi mpya Manchester City

Manchester City confirm Pellegrini appointment

The Chilean has signed a three-year deal to succeed Roberto Mancini at the Etihad Stadium after a protracted departure from Malaga, and will begin his duties on June 24
Manchester City have confirmed Manuel Pellegrini as the club's new manager on a three-year deal.

Pellegrini succeeds the sacked Roberto Mancini, having guided Villarreal to the Champions League semi-finals and Malaga to the last eight in their debut campaigns in Europe's elite competition.





Last week Goal revealed Pellegrini had flown into Manchester to finalise negotiations, and City have now confirmed he will begin his duties on June 24.

Pellegrini told the club's official website: "I am delighted to accept this hugely exciting opportunity.

"The club has a clear vision for success both on and off the pitch and I am committed to making a significant contribution.

"Everything is in place for Manchester City to continue to be successful and I am excited to be able to work with such a talented squad, the executive team and the board to deliver for fans who are renowned for their steadfast support."

City chairman Khaldoon Al Mubarak added: "Manuel is a hugely experienced and successful manager with a proven track record."

BAADA YA KUMSAINISHA JUZI - SIMBA SASA NJIANI KUMUUZA AMRI KIEMBA KWENDA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO

 
Siku moja baada ya Simba kumwongezea mkataba Amri Kiemba, klabu hiyo ya Msimbazi inatarajia kumpiga bei kiungo huyo mwenye kiwango kilichosimama kwenye mstari kwa timu ya Wydad Ac Casablanca ya Morocco.


Mpango wa kumuuza Kiemba umekuja baada ya mashushushu wa timu hiyo ya Morocco kuridhishwa na kiwango alichoonyesha wakati akiichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani.
 
Katika mchezo huo, Stars ilifungwa mabao 2-1, huku Kiemba akifunga bao nzuri la kufutia machozi kwa kiki ya mwendo mrefu nje ya boksi la hatari.
Zakaria Hanspope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, amelithibitishia gazeti la Mwananchi jana kuwa, mazungumzo ya awali ya kuuzwa kwa kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga yako hatua za mwisho kukamilika.
 
“Ni kweli, mazungumzo ya awali yameshafanyika kati ya Simba na uongozi wa Wydad Ac Casablanca, leo tunamalizia tulipofikia,” alisema Hanspope.
“Niko Morocco kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Wydad Casablanca, natumaini tutafikia mahala pazuri Mungu akijalia,” alisema Hanspope.
Mmoja wa vigogo wa Kundi la Friends of Simba ndiyo aliyeushtua uongozi juu ya mpango huo, ambao nao waliharakisha kumsainisha mkataba mpya kabla ya kumuuza. Juzi, Simba ilimsainisha Kiemba mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh35 mil.

SOURCE: MWANANCHI