tuwasiliane

Thursday, June 20, 2013

Thamani ya Kiemba Sh500 mil

 

Wakati Simba ikiendelea kusotea pesa za kuuzwa Emmanuel Okwi klabu ya Etoile du Saleh ya Tunisia, klabu hiyo imesema mpango wake wa kumpiga bei kiungo, Amri Kiemba kwenda Raja Casablanca ya Morocco utatimia iwapo klabu hiyo itakubali kutoa siyo chini ya Sh500 milioni.

Raja Casablanca imepiga hodi Msimbazi kutaka kumsajili Kiemba baada ya kuvutiwa naye wakati walipomwona akiichezea Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Morocco zaidi ya wiki moja iliyopita.
Akizungumza na chanzo chetu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspope alisema, kiwango hicho cha fedha ndiyo thamani ya sasa ya Kiemba.
“Tayari tumezungumza na Raja Casablanca na kweli wameonyesha nia ya kumtaka Kiemba, lakini kwetu hakuna namna yoyote ya kumtoa bila Sh500 milioni kuwekwa mezani,” alisema Hanspope.
“Nilipokwenda kwao (Morocco) Rais wa klabu alikuwa Uturuki, tunasubiri arejee ili tuwatumie mchanganuo mzima wa mauzo ya Kiemba,” alisema.
Hanspope, alisema angependa kuona klabu yake inafanya biashara ya kuwauza wachezaji kwa faida. Tunatakiwa kuwalipa makocha, kuingia mikataba na wachezaji, mambo yote haya yanahitaji pesa. Hatuwezi tena kufanya biashara isiyo na faida kwa upande wetu,” alisema zaidi bosi huyo.

source; mwananchi

No comments:

Post a Comment