tuwasiliane

Saturday, June 15, 2013

MBWANA SAMATTA AENDELEA KUWAFUNIKA MASTAA WOTE TP MAZEMBE - ULIMWENGU NAE HAYUPO NYUMA

SAMATTA remains the key man
Kwa mujibu wa takwimu zilizotlewa na klabu ya TP Mazembe. kwa kutumia vigezo vya: Kucheza mechi, Pasi zilizozaa matunda na Mabao - mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu hiyo Ally Mbwana Samatta ameongoza kwa kipindi cha takribani miezi 2, April na May.

MECHI/MUDA WALIOCHEZA
Kwa kuzingatia muda wa kucheza, hakuna aliyeweza kutimiza michezo 13 ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mwezi May wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza walicheza mechi zote saba, wakati katika kuleta utofauti KASUSULA na SAMATTA walicheza mechi zote sita. Katika dakika walizocheza Samata tayari alikuwa anashika nafasi ya 3 nyuma ya Richard KISSI Boateng na Kasongo Kabiona.

Dakika walizocheza kwa namba: 1. KIDIABA na KASUSULA dakika 900.
3. SAMATTA 873
4. BOATENG 79
5. KABIONA 720
6. SINKALA 655
7. KIMWAKI na HICHANI 630
9. MPUTU 610
10. ASANTE 518
11. KALABA 512
12. ILONGO 475, 13. NKULUKUTA 447, 14. KABANGU 430, etc.

Mabao - Samatta anaongoza
Hakuna shabiki yoyte wa TPM anayeweza kushangazwa na mshambuliaji huyu wa kibongo kushika nafasi ya kwanza. SAMATTA amefunga mabao 6 ndani ya miezi mwili, akifuatiwa na Bokanga aliyefunga 5, Awako na Tresor Mputu wamefunga mabao 4 kila mmoja huku mshambuliaji mwingine wa kibongo Thomas Ulimwengu akifunga mabao 2.


Pasi za mabao: MPUTU anaongoza ...
Tresor MPUTU ameendelea kuwa mfalme wa pasi za mwisho ndani ya TP Mazembe. Lakini Samata hayupo mbali - anashika nafasi ya pili. 
Waliongoza: 1. MPUTU pasi 6 , 2. SAMATTA pasi 5, 
3. BOATENG 2, 6. ASANTE, BOKANGA, KABANGU, KASONDE, ADJEI, NKULUKUTA, ULIMWENGU kila mmoja alitoa pasi 1 ya goli.

No comments:

Post a Comment