tuwasiliane

Sunday, June 16, 2013

POLE YA DOCTA SLAA KWA WATU WA ARUSHA

 
Wana Arusha,

Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha.

Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile.

Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi.

No comments:

Post a Comment