tuwasiliane

Sunday, June 16, 2013

TAIFA STARS KUWA NA MABADILIKO KIDOGO LEO

 
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameweka wazi kuwa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ atacheza badala ya Aggrey Morris wakati Mwinyi Kazimoto akiziba pengo la Mrisho Ngassa.

Morris atakosa mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania mchujo wa Fainali za Kombe la Dunia Brazili 2014.
Beki huyo wa kati anayekipiga na klabu ya Azam FC anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye pambano la marudiano dhidi ya Morocco mjini Marrakesh. Stars ikilala mabao 2-1.
Kwa upande wa Ngassa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano alizopewa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ivory Coast. Stars ikilala mabao 2-0 na ya pili akilimwa pambano la Morocco. Stars ikifungwa mabao 2-1.
Kim alikiambia chanzo chetu jana jijini Dar es Salaam kuwa nafasi ya Morris atacheza Cannavaro wakati akilazimika kumtumia Kazimoto kucheza nyuma ya Thomas Ulimwengu, huku Amri Kiemba akicheza winga ya kulia.
“Nafasi ya Morris atacheza Cannavaro. Pia, nitambadilisha Kazimoto kucheza nyuma ya Ulimwengu wakati Kiemba atacheza pembeni, winga ya kulia.” alisema Kim na kuongeza.
“Nafikiri kukosekana kwao hakuwezi kuathiri timu kufanya vizuri.” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment