SERIKALI
imeziruhusu klabu za Simba SC, Yanga SC za Dar es Salaam na Super
Falcons ya Zanzibar kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla amefanya Mkutano na
Waandishi wa Habari mjini Dodoma asubuhi ya leo kusema wameruhusu klabu
hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo
kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla
amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba
timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko
yanayoedelea Sudan.
Kufuatia tamko la Serikali kuziruhusu klabu hizo sasa ziende Sudan, sasa ni juu yao ya klabu hizo kuamua kwenda au kutokwenda.
Lakini
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
Mkenya Nicholas Musonye amekwshatishia atazichukulia hatua kali klabu
hizo zisipokwenda.
Juzi
Serikali kupitia Makalla ilitoa tamko la kuzuia klabu za Tanzania
kutokwenda Sudan kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.
Kufuatia
tamko hilo, jana Yanga, ambao ni mabingwa watetezi kwa miaka miwili
mfululizo, walitangaza kuvunja kambi yao hadi wiki mbili baadaye, wakati
Kombe la Kagame linaanza kutimua vumbi Juni 18, mwaka huu.
Yanga
wamepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja na Ports ya Djibouti,
Express ya Uganda na Vital 'O' ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi,
Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman ya
Somalia na APR ya Rwanda.
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kufikia tamati Julai 2, mwaka huu mjini
Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na
wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan
na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo Juni 20 kwa kumenyana na Express, wakati Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-mereikh
No comments:
Post a Comment