tuwasiliane

Monday, December 31, 2012

Breaking News:Kocha Mpya Simba atua Dar


Kocha Mkuu wa Simba Patrick Lieweg, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Jackson Odoyo          Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Lieweg, amewasili nchini mchana huu tayari kwa safari ya kwenda Zanzibar kuungana na timu hiyo Katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza kesho visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Habarimpya.com muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, alisema kwamba amekuja kuifundisha Simba na kuipatia ubingwa.
"Kwanza nimekuja kwa furaha baada ya kusikia kwamba Simba ndiyo mabingwa, watetezi wa Ligi Kuu, na katika msimu huu wanashika nafasi ya pili, hiyo ni nzuri kwangu kwa sababu nafahamu kwamba kufundisha timu bingwa lakini katika msimamo inashika nafasi ya pili inachangamoto nyingi, kwa sababu ya presha ya wachezaji,uongozi pamoja na mashabiki kuwa juu,pili ninafahamu juu ya ushindani uliopo katika soka la Afrika"alisema Lieweg na kuongeza:
"Hivyo nitakwenda Zanzibar kuungana na timu ila siendi kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mashindano hayo, kwa sababu nimechelewa kufika,ila ninakwenda Zanzibar katika mashindano hayo kwa ajili ya kuandaa kikosi cha ushindi,kwa sababu mbele yangu ninakabiriwa na mashindano ya Ligi pamoja na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika".
Kocha huyo rais wa Ufaranza alisema kwamba kikubwa kwake ni mazoezi, nakuifahamu timu kusoma uwezo wa mchezaji mmoja mmoja katika timu, na kwamba anaamini kwamba atapata ushirikiano mzuri sana kutoka kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo.
Kuhusu presha ya mashabi kutaka ushindi katika kila mechi alisema kwamba,hiyo ni kawaida ya mashabiki wote duniani lakini katika mashindano hayo angependa kupewa muda wa kuisoma timu kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia ushindi.
Akizungumzia fomesheni atakayoitumia katika timu hiyo alisema kwamba ingawa anafomesheni zake kama kocha lakini,kwanza angependa kuonana na uongozi wa timu hiyo, ili ajue sera za timu, kwa sababu kila timu inasera zake hivyo wakishamwambia sera zao ndipo atakapochagua fomesheni ya kutumia.

Walimu 25,000 kuajiriwa mwakani

SERIKALI inatarajia kuajiri walimu 25,000 wa sekondari mwakani ili kupunguza uhaba wa walimu katika shule za sekondari za Serikali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) Stephen Wasira, alisema hayo juzi wakati akihutubia mikutano ya hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti wilayani humu.
Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini ikiwemo upungufu wa walimu ambao sasa umegeuka kuwa mzigo kwa wazazi na walezi ambao wanachanga fedha za kuwalipia mishahara walimu wa kujitolea wanaofundisha shule hizo.

Alisema mbali na kuwapunguzia mzigo huo wazazi, Serikali pia itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa shule hizo ikiwa ni pamoja na kujenga hosteli na kuweka huduma za maji na umeme hasa kwa shule za vijijini ili walimu na wanafunzi wapate huduma hizo kwa urahisi.
“Tutaongeza walimu na kuboresha mazingira ya elimu. Januari mwakani walimu 25,000 wa Shule za Sekondari wataajiriwa na kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu mashuleni,” alisema Wasira.

Kuhusu madai mbalimbali ya walimu, Wasira alisema Serikali inayatambua na kuyafanyia kazi kwa kuwa ni watu muhimu katika kuboresha elimu nchini.
Alikiri kwamba Serikali ilichelewa kuyatatua baadhi ya madai hayo kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya uchumi na kusema hata hivyo inaendelea kuyatatua kadiri hali inaporuhusu.
Katika hatua nyingine, Wasira aliwasisitizia umuhimu wa wazazi na walezi kuwasomesha watoto wao bila ubaguzi akisema elimu haina mbadala maishani huku akiwataka wajenge uhusiano mzuri na walimu katika kufuatilia na kusimamia maendeleo ya watoto wao na kukuza taaluma ya mtoto.

Saturday, December 29, 2012

SIMBA 0 TUSKER 3 FULL TIME

Tusker wakishangilia mbele ya mashabiki wa Simba 


SIMBA SC imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko, tayari Tusker walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse Were dakika ya 37 na 45.
Mabao yote yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo iliongozwa na beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji anafunga akiwa amebaki anatazamana na kipa.
Simba ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu iliyokuwa inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki warefu wa klabu hiyo bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa Yanga, Joseph Shikokoti. 
Kipindi cha pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba pamoja na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo na Kiggi Makassy na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza kupata hata bao la kufutia machozi. 
Nassor Masoud aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na kutoka nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza. 
Simba SC; William Mweta, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita, Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,  
SOURCE; BIN ZUBERY

Mancini na Redknapp matatani

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA, limewaandikisa barua makocha Harry Redknapp na Roberto Mancini kuhusiana na shutuma zao dhidi ya marefa.
Kocha wa QPR, Redknapp, alimshutumu refa wa mechi yao siku ya Jumatano ambapo walishindwa kwa magoli mawili kwa moja na West Brom.
Naye kocha wa Manchester City Roberto Mancini, aliwashutumu maafisa walisimamia mechi yao dhidi ya Sunderland, kwa kukosa kutoa adhabu baada ya nyota wake Pablo Zabaleta kufanyiwa madhambi kabla ya Adam Johnson kufunga bao la ushindi la Sunderland.
Makocha hao wawili sasa huenda wakachukuliwa hatua za kinidhamu na FA.
Makocha hao wawili sasa wameamriwa kuwasilisha ripoti zao kuhusu matamshi waliyoyatoa baada ya mechi zao.

Ferguson azozana na Pardew

Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki.
Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.
Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.
'' Allan Pardew ndiye kocha ambaye mara nyingi huwazomema marefa kwa takriban karibu mechi zote'' alisema Ferguson.
Pardew alipigwa marufuku ya kutohudhuria mecho mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumsukuma mmoja wa wasimamizi wa mechi yao mwezi Agosti.
Ferguson alimzomea refa wa mechi hiyo Mike Dean, naibu wake Jake Collin na Neil Swarbrick, mwanzo wa kipindi cha pili ya mechi yao ya ligi kuu ya Premier kupinga goli la pili la Newcastle.
Dean aliidhinisha kuwa Papiss Cisse, hakuwa ameotea wakati Jonny Evans alipojifunga kunako dakika 28.
Pardew hakufurahiswa na uamuzi wa FA wa kutomuadhibu kocha huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka sabini.

RIDHIWANI KIKWETE APONDA MFUMO WA UENDESHAJI YANGA ASEMA AFADHALI WA SIMBA

Ridhiwani akihutubia Waandishi asubuhi ya leo Kiromo Hotel


MWENYEKITI wa Kamati ya Kusaidia timu za soka za vijana za taifa, Ridhiwani Kikwete, amesema mfumo wa uendeshwaji wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam ni mbovu kwa sababu unategemea mfuko wa mtu mmoja.
 
Akizungumza wakati anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani, Kikwete alisema kwamba Yanga inahitaji kubadilika kutoka mfumo huo.
 
Kikwete alisema ni afadhali mfumo wa uendeshwaji wa Simba SC, ambao desturi yao ni kuchangishana.
“Nilijaribu kufanya uchunguzi wa mfumo wa uendeshwaji wa klabu ya Yanga, nikashangazwa ni mfumo mbaya, kwa sababu unategemea mfuko wa mtu mmoja, afadhali Simba wao huwa wanachangishana,”alisema.
 
Ingawa hakumtaja mtu ambaye mfuko wake unategemewa Yanga, lakini wazi ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
Kwa ujumla katika hotuba yake, Kikwete alisema haridhishwi na mfumo wa uendeshwaji wa soka ya Tanzania na kwamba unahitaji mabadiliko.
Kikwete aliushauri uongozi wa TASWA upiganie nafasi ya uwakilishi ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusisitiza juu ya umuhimu wa waandishi nchini kutambua haki zao.
 
Lakini pia Kikwete aliwaasa waandishi kuepuka uandishi wa kinazi wa Simba na Yanga na badala yake kuzama ndani zaidi katika kuripoti, sambamba na kuripoti michezo yote, badala ya kuegemea kwenye soka pekee.
 
“Vyombo vya habari lazima viwe na wataalamu tofauti wa kuripoti michezo tofauti, huyu akiegemea kwenye soka, mwingine aegemee kwenye mchezo mwingine, ili kuhakikisha tunafikisha ujumbe vema kwa jamii,” alisema mtoto huyo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
 
Ridhiwani ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, NEC akiiwakilisha Wilaya ya Bagamoyo alisema kwamba ipo haja ya TASWA kuendesha semina kadhaa za kuelimisha Waandishi wa Habari kuweza kuripoti michezo mbalimbali nchini.  
 
Aidha, katika mkutano huo, wanachama walielimishwa kuhusu uanzishwaji wa Saccos na kuridhia kuanza kwa mchakato wa kuundwa kwa chama cha ushirika wa akiba na mikopo kwa Taswa. Walipendekezwa wajumbe waunde timu ya mpito.
Katibu wa TASWA, Amir Mhando kulia na Katibu Msaidizi, George John wakisikiliza hotuba ya Ridhiwani

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Alfred Lucas kushoto na Jaba kulia wakisikiliza hotuba ya Ridhi

Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akijadiliana jambo na Katibu wake, Mhando

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Grace Hoka, Kapinga na Zena Chande wakisikiliza kwa makini hotuba ya Ridhiwani

Salehe Ally na Mohamed Akida kushoto

Kutoka kulia Mkandemba, Eric Mkuti na Abdallah Majura

Wakongwe, kutoka kulia Mwina Kaduguda, Willy Chiwango na Salim Said

Kutoka kulia Mgaya Kingoba, Alfred Lucas na Ibrahim Bakari

Kutoka kulia Thom Chilala, Angela Msangi na Somoe Said

Kwa raha zao, Pinto na Ridhi

Kutoka kulia Bon Wambura, Ben Kisaka

Ibrahim Bakari na Dina Ismail

Boss Masoud na Zai Kibwana

Frank Sanga kushoto              source bin zubery     

Friday, December 28, 2012

MESSI ATOSA DILI LA MAANA

Lionel Messi turned down a blockbusting move to an unknown Russian club after a bid of £205million triggered his release clause.
The club, thought to be Anzhi Makhachkala, then offered a blockbusting £460,000-a-week deal to the Argentine superstar, a massive £24m a year after tax, according to The Sun.
How much??? Even £460,000 a week couldn't tempt Messi to leave Barca
How much??? Even £460,000 a week couldn't tempt Messi to leave Barca
Barcelona were obliged to accept the massive offer but a gobsmacked Messi quickly rejected the move after discussions with Barca president Sandro Rosell and his family.
The three-time World Player of the Year, who scored a record breaking 91 goals this calendar year, then pledged his future by signing a new deal with the Catalan giants.
Record-breaker: The deal would've eclipsed the world record fee of £80m rivals Real Madrid paid for Cristiano Ronaldo
Record-breaker: The deal would've eclipsed the world record fee of £80m rivals Real Madrid paid for Cristiano Ronaldo


Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2254006/Lionel-Messi-turns-460-000-week-leave-Barcelona.html#ixzz2GLG7wgEe
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook

WACHEZAJI WANAOENDA NA YANGA UTURUKI JUMAPILI HAWA HAPA

Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa  5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza 
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu:  Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya
SOURCE; SHAFFIH DAUDA

Wednesday, December 26, 2012

YANGA YAKATWA NGEBE NA TUSKER

Kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan akifumua shuti katikati ya mabeki wa Tusker katika mchezo wa leo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

MABINGWA wa Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo ulikuwa mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.   
Wachezaji wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao,
 Ismail Dunga kulia
Hadi mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo, ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja ametoa sare.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda, Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC; George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,  

SOURCE; BIN ZUBERY

HATIMAYE WANAKILOSA WAFANIKIWA KUUNDA UMOJA WAO

hatimaye kikao cha wadau mbalimbali wa kilosa kimefanyika hii leo na kumalizika salama,maazimio ya kikao hicho ni kama ifuatavyo. wadau tumekubaliana kuanziasha asasi isiyo ya kiserikali inayoitwa WANAKILOSA,asasi hiyo itakuwa ikishughulikia mambo mbalimbali ya kijamii mfano,elimu,afya,kilimo nk.

pia tumekubaliana kutengeneza katiba ya kikundi, katika kutengeneza katiba ya kikundi tumeweza kuchagua viongozi wa mpito wa kikundi ambao ni kama ifuatavyo

myenyekiti ni Mriam kurameso, katibu ni Edwin Mwombeki,mhasibu ni pendo makata,na mtu wa kusaidia kutengeneza katiba ni Ramadhan Imiri,

pia kikundi tumekubaliana kuwa tarehe 1/1/2013 wanakikundi kwenda kutembelea wagonjwa kwenye hospital ya wilaya ya kilosa,katika kufanikisha hilo bwana edwin mwombeki ametoa mchango wa shilingi 20000,saed huwel ametoa shiling 10000,wanakilosa mbalimbali tunakaribisha michango myenu ili kufanikisha hilo, mnaweza kutuma michango yenu kwa muhasibu wetu pendo makata ambaye namba zake ni 0716 128913 au 0767813121 au 0787813121, kikao kingine cha wana kilosa kitafanyika tarehe 1/1/2013 pale pale golden folk hotel saa 11 jion, baada ya kutoka hospital

Wednesday, December 12, 2012

Hayatou kuchaguliwa bila kupingwa


Issa Hayatou
Issa Hayatou Rais wa CAF

Rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika, CAF, Issa Hayatou, anaelekea kushinda awamu nyingine ya kuliongoza shirikisho hilo bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu ujao.
Baada ya mkutano wa kamati kuu ya CAF uliofanyika tarehe 10 Desemba mwaka huu, katibu mkuu wa shirikisho hilo alilifahamisha kamati hiyo kuwa Hayatou, ndiye mgombea wa pekee katika kiti cha urais.
Afisa mkuu wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA Jacques Anouma, alikuwa ametangaza kuwa atawania kiti hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mjini Maraketch, nchini Morocco mwezi Machi mwaka ujao.
Anouma kutoka Ivory Coast alitoa tangazo hilo, licha ya kufahamu kuwa kwa mujibu wa sheria za CAF, hangeliruhisiwa.
Hayatou, mwenye umri wa miaka 66, aliongoza mikakati ya kubadili katiba ya CAF, ambayo sasa inaruhusu wanachama wake wa kamati kuu pekee walio na haki ya kupiga kura, kuwania kiti cha urais.

Hayatou adaiwa kubadili sheria kujinufaisha

Anouma ni mwanachama wa kamati kuu ya CAF, kwa kuwa yeye ni muakilisha wa bara la Afrika katika kamati kuu ya FIFA.
Jacques Anouma
Jacques Anouma mwanachama wa kamati kuu ya FIFA

Licha ya kuwa yeye huhudhuria mikutano ya kamati kuu ya CAF, hana haki ya kushiriki katika zoezi lolote la kupiga kura.
Jina na Anoumaa linaaminika kuwasilishwa kwa kamati kuu ya CAF, kabala ya tarehe siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi, lakini kwa sasa haliko katika, orodhaa ya majina ya watu wanaowania viti mbali mbali, kwa mujibu wa orodha iliyochapishwa kwenye mtandao wa CAF.
Juhudi za Liberia za kutaka sheria hiyo kubatilisha ziligonga mwamba pale ombi lao lilipotupiliwa mbali na mahakama ya upatinishi ya michezo CAS, kwa misingi kuwa Liberia haikuwa imefuata sheria zote za CAF, kutatua mzozo huo.
Rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Liberia, Hassan Musa Bility, ambaye aliomgoza uasi huo, ni miongoni mwa wale watakaowania nafasi katika kamati kuu ya CAF.
Danny Jordaan, kutoka Afrika Kusini ambaye, kwa mujibu wa sheria za sasa hawezi kuwania kiti cha urais, atawania kuwa muakilisha wa kanda ya Afrika Kusini katika kamati kuu ya CAG.

BEKI LAKUFA MTU KUMWAGA WINO AZAM FC LEO

Humphrey Mieno yupo kwenye rada za Azam pia

BEKI mmoja matata wa Tusker ya Kenya, anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kwa ajili hya kusaini mkataba wa kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema jana kwamba, beki huyo mzuri atafichuliwa leo  baada ya kusaini mkataba, ila kwa sasa wanaendelea kuweka kapuni jina lake.
 
Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
 
Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
 
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
 
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno.  
SOURCE; BIN ZUBERY

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI NA KUPEWA MILLIONI 10 - AHAIDIWA NYINGENE MWISHO WA MSIMU

Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita  na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000.
source; shaffihdauda 

Saturday, December 8, 2012

OKWI AMALIZANA NA SIMBA,ALAMBA MKATABA MPYA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam, baada ya kusaini jana usiku katika hoteli ya Sheraton mjini hapa.
 
Okwi alisaini mbele ya Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ambaye ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.
 
Baada ya kusaini, Okwi alisema; “Nimefurahi kuongeza mkataba na klabu yangu na ninaahidi kuendelea kuitumikia kwa nguvu zangu zote,”alisema Okwi.
Kwa upande wake, Hans Poppe alisema kwamba anaamini kusaini na Okwi sasa kutawakata vilimilimi wapinzani wao, ambao walikuwa wanamuwania mchezaji huyo.
 
“Sisi tunajua yote yaliyokuwa yakiendelea kwenye Challenge, tunajua wapinzani wetu walimfuata Okwi huku, lakini huyu mchezaji ana mapenzi yeye mwenyewe na Simba SC,”alisema Hans Poppe.
Okwi aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 mjini hapa, alisajiliwa na Simba SC mwaka 2009 akitokea SC Villa      ya hapa, baada ya klabu hiyo kumkosa mshambuliaji mwingine Mganda, Brian Umony aliyewahiwa na SuperSport United ya Afrika Kusini.
 
Tangu msimu uliopita, Okwi amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Yanga au Azam na akiwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyoanza Novemba 24 na inafikia tamati kesho, ziliibuka habari za klabu hizo kumfuata kumsainisha mjini hapa.
Okwi jana alifunga bao moja kati ya matatu ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, yaliyozima ndoto za Tanzania Bara kurejea nyumbani na Kombe la Challenge.
 
Kwa matokeo hayo, Uganda itamenyana na majirani zao na wapinzani wao wakubwa, Kenya katika fainali Jumamosi, ambao katika mchezo wa kwanza waliitoa kwa mikwaju ya penalti 4-2 Zanzibar, kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika 120.
 
Zanzibar na Bara zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu siku hiyo hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Namboole.
Hadi mapumziko, Uganda walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya 11, baada ta kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na kipa wake, Hamza Muwonge na kufumua shuti kali la umbali wa mita 19, ambalo lilimshinda kipa Juma Kaseja.
 
Baada ya bao hilo, Okwi aliumia na kutoka nje dakika ya 36 nafasi yake ikichukuliwa na Hamisi Kiiza.
Uganda ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi na kulitia misukosuko lango la Stars kwa takriban dakika 10 mfululizo, lakini baada ya hapo timu hizo zikaanza kushambuliana kwa zamu.
 
Timu zote zilikuwa zikishambulia kutokea pembeni, lakini Uganda ndio walioonekana kuzalisha mashambulizi ya hatari zaidi.
Kipa na Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza akilaumiana na mabeki wake kwa kufungwa bao la kutanguliwa.
Kipindi cha pili, Waganda walirudi na moto wao tena na kufanikiwa na kupata bao la pili dakika ya 51, safari hii Robert Ssentongo akimtungua Kaseja, baada ya mabeki wa Stars kudhani ameotea.
Pamoja na kufungwa bao la pili, Stars waliendelea kucheza kwa juhudi, ingawa Waganda waliendelea kutawala mchezo.
Mpira uliotemwa na Juma Kaseja kufuatia shuti la Moses Oloya, ulimkuta Ssentongo dakika ya 71 akaukwamisha nyavuni na kuipatia The Cranes bao la tatu. Kutoka hapo, hali ilikuwa mbaya kwa Stars.
Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, taa za Uwanja wa Mandela zilizimika, lakini baada ya jitihada za pamoja za FUFA, CECAFA na uongozi wa Uwanja, ziliwaka baada ya dakika saba na mchezo kuendelea hadi filimbi ya mwisho.

Anasaini

Anasaini

Anaweka dole gumba     HABARI KWA MSAADA WA BIN ZUBERY          

Walimu wakimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.

Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.

Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.

Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.

“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.

Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.

Mwalimu huyo alidai kuwa walimu wamekuwa wakitishiwa kuchomwa visu na nyumba zao kuchomwa moto, huku walimu wanne wa kike wakidhalilishwa kimapenzi kwa kupigwa mabusu na kutongozwa na wanafunzi.
“Wanafunzi wamefanya mtihani wa kidato cha pili chini ya ulinzi wa askari polisi wenye silaha kitu ambacho si cha kawaida,” aliongeza.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ofisa Elimu Sekondari, Adnan Mwenda alisema asingependa kuzungumzia tatizo hilo kwa kuwa siyo msemaji. Akashauri atafutwe mkurugenzi wa wilaya… “Unaweza kuzungumza mambo mengine yakakuletea matatizo,” alisema Mwenda kabla ya kuelekeza atafutwe mkurugenzi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alithibitisha walimu hao kuikimbia shule hiyo na kusema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, itakutana hivi karibuni kujadili suala hilo.
“Ni kweli shule hiyo imetelekezwa, walimu wamekimbia na wanafunzi hawaendi shule. Tatizo tunalifahamu na Mkuu wa Wilaya anafanya jitihada mbalimbali kurekebisha tatizo hilo,’ alisema.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruaruke, Hemedi Mpullu pia alithibitisha walimu hao kuitelekeza shule hiyo na kusema Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu ameagiza kufanyika kwa kikao cha dharura ili kupatikana mwafaka kati ya walimu hao, wanafunzi na wazazi.
“Mbunge wa Kibiti, Abdul Marombwa amepanga pia kufanya mkutano hapa Ruaruke ili kutafuta mwafaka,” alisema Mpullu.
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT), Wilaya ya Rufiji,  Manyama Lazaro alisema kuondoka kwa walimu hao, kumefanya shule hiyo ijifunge yenyewe, kwani wanafunzi nao sasa hawaendi shule.

“Wanafunzi wamefikia hatua ya kuwachora walimu wa kike wakifanya mapenzi na walimu wa kiume katika kuta za vyoo! Huu ni udhalilishaji mkubwa,” alisema.
Lazaro alieleza kuwa katika siku za hivi karibuni, wanafunzi hao walichoma moto nyumba tatu za walimu na Bodi ya Shule iliamua kuwa wanafunzi hao waitwe na wazazi wao ili walipe gharama za uharibifu.

source; gazeti la mwananchi

Thursday, December 6, 2012

XCLUSIVE; YAW BERKO ATUA FC LUMPOPO KWA MKOPO

Klabu ya Yanga wapo katika hatua za mwisho za kumtoa golikipa wao wa kimataifa kutoka Ghana Yew Berko kwenda klabu ya FC Lupopo ya Congo kwa mkopo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Yanga ni kwamba klabu hiyo wanampeleka Berko FC Lupopo ili waweze kupata nafasi ya kumuongeza Kabange Twite katika usajili wa dirisha dogo.

Berko jana alionekana akiwa katibu wa Yanga wakiwa katika ofisi za ubalozi wa Congo wakifuatilia taratibu mbalimbali za viza ya kwenda nchini Congo kwa ajili ya kujiunga na Lupopo.
Kabange Twite
Kabange Twite inasemekana ameshamalizana na Yanga na siku chache zijazo atakuja kujiunga na timu yake mpya ili kuanza kujipanga na msafara wa klabu hiyo kwenda nchini Uturuki kwa ajili kuajindaa na ligi kuu ya Tanzania bara. 

KILIMANJARO STARS VS UGANDA THE CRANES,ZANZIBAR HEROS VS KENYA NUSU FAINAL YA CHALLENGE LEO

TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa kumenyana na wenyeji, Uganda, The Cranes katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kuanzia saa 12:00 jioni.
 
 
Mchezo huo, utatanguliwa na mechi nyingine ya hatua hiyo kati ya Zanzibar na Kenya, ambayo, itaanza saa 10:00 jioni.     
Hii inakuwa mara ya pili mfululizo, Bara kukutana na Uganda katika Nusu Fainali ya michuano hii, kwani hata mwaka jana pia mjini Dar es Salaam, zilikutana katika hatua hiyo, Desemba 8, Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo, wenyeji wakiwa chini ya makocha wazalendo, walichapwa mabao 3-1 ndani ya dakika 120, Stars ikitangulia kupata bao mapema tu dakika ya 18, mfungaji Mrisho Khalfan Ngassa, lakini Nahodha wa The Cranes  Andy Mwesigwa akasawazisha dakika ya 56.
 
Mchezo ulipohamia katika dakika za nyongeza, Uganda walipata mabao mawili na kuwamaliza wenyeji, wafungaji Emmanuel Okwi dakika ya 102 na Isaac Isinde dakika ya  111 kwa penalti.
 
Kocha wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen ametahadharisha wanataka uchezeshaji wa haki kutoka kwa refa Mohamed El Fadil wa Sudan, ambaye pia aliwachezesha katika mechi dhidi ya Rwanda Robo Fainali.
“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni uchezeshaji wa haki kutoka kwa refa, maana tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,” alisema.
Poulsen alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa haki tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika michezo dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.
 
Kuhusu hali ya timu, Mdenmark huyo alisema hana majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia, si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.
Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stars, Sylvester Marsh amesema kama Uganda waliwafunga Tanzania Dar es Salaam mwaka jana, basi na wao watawafunga Kampala mwaka huu.
 
Kocha wa Uganda, The Cranes, Msoctland, Bobby Williamson alisema kwamba Stars ni timu nzuri, lakini haina uwezo wa kuifunga timu yake.
“Wana wachezaji wazuri, wenye vipaji, lakini bado timu yangu ni nzuri katika mashindano haya, tutawafunga,”alisema. 
 
Safu ya ushambuliaji ya Stars leo inatarajiwa kuongozwa na Mrisho Khalfan Ngassa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ ambao wanaongoza kwa mabao katika mashindano haya, kila mmoja akiwa na mabao matano.
Uimara zaidi wa Stars upo katika safu ya kiungo, ambako kuna watu mahiri kama Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar na Mwinyi Kazimoto.
Stars pia inajivunia safu imara ya ulinzi, chini ya Nahodha, kipa Juma Kaseja, mabeki Erasto Nyoni, Amir Maftah, Kevin Yondan na Shomary Kapombe ambao wameruhusu bao moja tu katika mechi nne zilizopita, tena la penalti, dhidi ya Burundi.
 
Bocco, aliyeimarika zaidi kiuchezaji, mwenye nguvu, anayeenda hewani na kuambaa vema na mpira, atasimama mbele ya mdomo wa goli la Korongo wa Kampala, wakati Ngassa atakuwa akishambulia kutokea pembeni.
Domayo, Kiemba na Sure Boy watakuwa wote wakikaba kwa bidii, wakati Kazimoto atakuwa akiiendesha timu, zaidi ya kuwatengenezea nafasi za kufunga Bocco na Ngassa.
Kiemba amekuwa akitumia mwanya wa timu kufanya mashambulizi ya kushitukiza kupanda kusaidia na ndiyo maana aliwafunga Rwanda, jambo ambalo linatarajiwa na leo pia.
Kazimoto mwenye mashuti makali hajafunga hata bao moja katika mechi nne zilizopita, lakini matarajio ya wengi atatikisa nyavu kuanzia leo baada ya kuizoea zaidi hali ya Kampala.
Uganda nao wana ukuta sugu, ambao haujaruhusu hata bao moja hadi sasa, ikiongozwa na kipa Hamza Muwonge, mabeki Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi na Isaac isinde, wakati safu ya kiungo ya kiungo inatarajiwa kuongozwa na Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito na Moses Oloya.
Safu ya ushambuliaji leo bila shaka dhamana watapewa, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na Brian Umony, wakati Emmanuel Okwi anaweza kuanzia benchi tena. Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali, Uganda wakicheza mbele ya malefu ya mashabiki wao na Bara wakijaribu kulipa cha Dar es Salaam  mwaka jana. 
Timu hizi zimekutana mara 12 katika Challenge tangu mwaka 1975, kila timu ikishinda mechi tano, sare mbili na Bara imefunga mabao 16, wakati imefungwa mabao 17.
Uganda; Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi, Henry Kalungi, Isaac Isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Tanzania; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Franko Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngassa.  
Mungu zibariki timu zetu, Bara na Zanziabr leo, ibariki Tanzania. Amin.
MATOKEO YA JUMLA STARS NA CRANES TANGU 1975:
                     P    W  D   L    GF GA      Pts
Uganda         12 5    2    5    17 16       17
Tanzania       12 5    2    5    16 17       17
REKODI YA STARS NA CRANES CHALLENGE TANGU 1974:
Desemba 8, 2011; Nusu Fainali, Dar es Salaam
Uganda 3–1 Tanzania (dakika 120)
Januari 9, 2009; Kundi A Uganda
Tanzania 1-2 Uganda
Desemba 11, 2001; Kundi B Rwanda
Tanzania 1-0 Uganda
Desemba 1, 1995; Kundi B Uganda
Tanzania 2-1 Uganda B
Desemba 10, 1994; Fainali Kenya
Tanzania 2-2 Uganda: (Tanzania ilishinda kwa penalti 4-3)
Desemba 10, 1992; Fainali Mwanza
Tanzania B(Kakakuona) 0-1 Uganda
Desemba 17, 1990; Nusu Fainali Zanzibar
Tanzania 1-1 Uganda (dakika 120, Uganda ilishinda penalti 6-5)
Desemba 1, 1984; Kundi A Uganda
Tanzania 1-1 Uganda
Novemba 20, 1983; Kundi A Kenya
Tanzania 1-1 Uganda
Novemba 17, 1982; Kundi A Uganda
Tanzania 0-1 Uganda
Novemba 9, 1979; Kundi A Kenya
Tanzania 5-3 Uganda
Desemba 10, 1974; Fainali Dar es Salaam                                    
Tanzania 1-1 Uganda (Tanzania ilishinda kwa penalti 5-3)