Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA,
limewaandikisa barua makocha Harry Redknapp na Roberto Mancini kuhusiana
na shutuma zao dhidi ya marefa.
Kocha wa QPR, Redknapp, alimshutumu refa wa
mechi yao siku ya Jumatano ambapo walishindwa kwa magoli mawili kwa moja
na West Brom.Naye kocha wa Manchester City Roberto Mancini, aliwashutumu maafisa walisimamia mechi yao dhidi ya Sunderland, kwa kukosa kutoa adhabu baada ya nyota wake Pablo Zabaleta kufanyiwa madhambi kabla ya Adam Johnson kufunga bao la ushindi la Sunderland.
Makocha hao wawili sasa huenda wakachukuliwa hatua za kinidhamu na FA.
Makocha hao wawili sasa wameamriwa kuwasilisha ripoti zao kuhusu matamshi waliyoyatoa baada ya mechi zao.
No comments:
Post a Comment