Tusker wakishangilia mbele ya mashabiki wa Simba |
SIMBA SC
imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo
huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko, tayari Tusker
walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse Were dakika ya 37 na
45.
Mabao yote
yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo iliongozwa na
beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji anafunga akiwa amebaki
anatazamana na kipa.
Simba
ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu iliyokuwa
inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki warefu wa klabu hiyo
bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa Yanga, Joseph Shikokoti.
Kipindi cha
pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya
54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba pamoja
na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema,
Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo na Kiggi Makassy
na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje,
Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza
kupata hata bao la kufutia machozi.
Nassor Masoud
aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na kutoka nafasi yake
ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza.
Simba SC; William Mweta, Haruna Shamte, Paul
Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita, Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah
Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng,
Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick
Onyango, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk, SOURCE; BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment