Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea
muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho
Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake
kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa
kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.
Chanzo cha habari kilicho karibu na
mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari
amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya
kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita na
klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.
"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza
mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha
ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."
Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000.
source; shaffihdauda
No comments:
Post a Comment