Humphrey Mieno yupo kwenye rada za Azam pia |
BEKI mmoja
matata wa Tusker ya Kenya, anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kwa ajili hya
kusaini mkataba wa kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa
Azam FC, Nassor Idrisa alisema jana kwamba, beki huyo mzuri atafichuliwa
leo baada ya kusaini mkataba, ila kwa
sasa wanaendelea kuweka kapuni jina lake.
Tayari Azam
imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini
mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony
alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao
makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa
kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony
alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi
wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex
Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
SOURCE; BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment