Rais wa shirikisho la mchezo wa
soka barani Afrika, CAF, Issa Hayatou, anaelekea kushinda awamu nyingine
ya kuliongoza shirikisho hilo bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu ujao.
Baada ya mkutano wa kamati kuu ya CAF
uliofanyika tarehe 10 Desemba mwaka huu, katibu mkuu wa shirikisho hilo
alilifahamisha kamati hiyo kuwa Hayatou, ndiye mgombea wa pekee katika
kiti cha urais.Afisa mkuu wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA Jacques Anouma, alikuwa ametangaza kuwa atawania kiti hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mjini Maraketch, nchini Morocco mwezi Machi mwaka ujao.
Anouma kutoka Ivory Coast alitoa tangazo hilo, licha ya kufahamu kuwa kwa mujibu wa sheria za CAF, hangeliruhisiwa.
Hayatou, mwenye umri wa miaka 66, aliongoza mikakati ya kubadili katiba ya CAF, ambayo sasa inaruhusu wanachama wake wa kamati kuu pekee walio na haki ya kupiga kura, kuwania kiti cha urais.
Hayatou adaiwa kubadili sheria kujinufaisha
Anouma ni mwanachama wa kamati kuu ya CAF, kwa kuwa yeye ni muakilisha wa bara la Afrika katika kamati kuu ya FIFA.Jina na Anoumaa linaaminika kuwasilishwa kwa kamati kuu ya CAF, kabala ya tarehe siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi, lakini kwa sasa haliko katika, orodhaa ya majina ya watu wanaowania viti mbali mbali, kwa mujibu wa orodha iliyochapishwa kwenye mtandao wa CAF.
Juhudi za Liberia za kutaka sheria hiyo kubatilisha ziligonga mwamba pale ombi lao lilipotupiliwa mbali na mahakama ya upatinishi ya michezo CAS, kwa misingi kuwa Liberia haikuwa imefuata sheria zote za CAF, kutatua mzozo huo.
Rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Liberia, Hassan Musa Bility, ambaye aliomgoza uasi huo, ni miongoni mwa wale watakaowania nafasi katika kamati kuu ya CAF.
Danny Jordaan, kutoka Afrika Kusini ambaye, kwa mujibu wa sheria za sasa hawezi kuwania kiti cha urais, atawania kuwa muakilisha wa kanda ya Afrika Kusini katika kamati kuu ya CAG.
No comments:
Post a Comment