tuwasiliane

Friday, December 28, 2012

WACHEZAJI WANAOENDA NA YANGA UTURUKI JUMAPILI HAWA HAPA

Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa  5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza 
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu:  Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya
SOURCE; SHAFFIH DAUDA

No comments:

Post a Comment