tuwasiliane

Monday, December 31, 2012

Breaking News:Kocha Mpya Simba atua Dar


Kocha Mkuu wa Simba Patrick Lieweg, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Jackson Odoyo          Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Lieweg, amewasili nchini mchana huu tayari kwa safari ya kwenda Zanzibar kuungana na timu hiyo Katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza kesho visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Habarimpya.com muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, alisema kwamba amekuja kuifundisha Simba na kuipatia ubingwa.
"Kwanza nimekuja kwa furaha baada ya kusikia kwamba Simba ndiyo mabingwa, watetezi wa Ligi Kuu, na katika msimu huu wanashika nafasi ya pili, hiyo ni nzuri kwangu kwa sababu nafahamu kwamba kufundisha timu bingwa lakini katika msimamo inashika nafasi ya pili inachangamoto nyingi, kwa sababu ya presha ya wachezaji,uongozi pamoja na mashabiki kuwa juu,pili ninafahamu juu ya ushindani uliopo katika soka la Afrika"alisema Lieweg na kuongeza:
"Hivyo nitakwenda Zanzibar kuungana na timu ila siendi kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mashindano hayo, kwa sababu nimechelewa kufika,ila ninakwenda Zanzibar katika mashindano hayo kwa ajili ya kuandaa kikosi cha ushindi,kwa sababu mbele yangu ninakabiriwa na mashindano ya Ligi pamoja na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika".
Kocha huyo rais wa Ufaranza alisema kwamba kikubwa kwake ni mazoezi, nakuifahamu timu kusoma uwezo wa mchezaji mmoja mmoja katika timu, na kwamba anaamini kwamba atapata ushirikiano mzuri sana kutoka kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo.
Kuhusu presha ya mashabi kutaka ushindi katika kila mechi alisema kwamba,hiyo ni kawaida ya mashabiki wote duniani lakini katika mashindano hayo angependa kupewa muda wa kuisoma timu kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia ushindi.
Akizungumzia fomesheni atakayoitumia katika timu hiyo alisema kwamba ingawa anafomesheni zake kama kocha lakini,kwanza angependa kuonana na uongozi wa timu hiyo, ili ajue sera za timu, kwa sababu kila timu inasera zake hivyo wakishamwambia sera zao ndipo atakapochagua fomesheni ya kutumia.

No comments:

Post a Comment