tuwasiliane

Tuesday, July 31, 2012

31 JUL. NGASA ASILIMIA 90% MSIMBAZI MSIMU UJAO


HABARI AMBAZO BLOG HII IMEZIPATA KUWA SIMBA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUMNASA WINGA WA AZAM FC, MRISHO NGASA BAADA YA KUTOA DAU LA SHILING MILION 25, WAKATI YANGA IMETOA MILION 20.

AZAM WENYEWE WANATAKA TIMU AMBAYO ITAKAYOFIKA DAU KUBWA KUWAUZIA NGASA NA KESHO NDIO WAMESEMA MWISHO,KWA MAANA HIYO SIMBA NDIO WANAONEKANA WAMESHAMNASA NGASA KWA ASILIMIA 90

31 JUL.SIMBA KUWATEMA LINO MASOMBO,SHAMTE NA KINJE


SIMBA imewatema nyota wake watatu akiwamo beki Lino Masombo baada ya kuboronga kwenye mashindano ya Kombe la Kagame.

Habari ambazo Chanzo chet kimezinasa zinaeleza uongozi wa Simba ulikaa wikiendi iliyopita na kufikia uamuzi huo mgumu.

Masombo anayeaminiwa alichukuliwa kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga, ndiye anayeongoza orodha ya kutimuliwa akiwa na Salum Kinje na Haruna Shamte.

Kinje alisajiliwa kutoka AFC Leopards ya Kenya wakati Shamte alirudishwa kikosini baada ya kutolewa mkopo kuchezea Villa Squads kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu uliopita.

Masombo alisajiliwa kutoka Motema Pembe ya Congo, hata hivyo ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye Kombe la Kagame.

"Jamaa wamepigwa panga baada ya kuonyesha kiwango cha chini katika michuano ya Kagame," alisema mtu mmoja, ambaye yuko karibu na uongozi wa klabu hiyo.

Pamoja na kuwatimua wachezaji hao, nyota wengine Uhuru Selemani, Danny Mrwanda na Kanu Mbiyavanga wamepewa onyo kali kwa kucheza chini ya kiwango.

Mmoja wa wachezaji wanaotakiwa kutimuliwa, Kinje aliiambia Mwanaspoti kuwa anaendelea na mazoezi.
Hata hivyo, uongozi wa Simba kupitia kwa Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga alisema: "Upo uwezekano wa wachezaji walionekana katika michuano ya Kagame wasiwepo katika usajili wetu kutokana na sababu mbalimbali.

"Wapo wachezaji waliocheza mashindano yale kwa mapatano bila mkataba, tunaweza kumalizana nao lakini siwezi kuwataja majina."

Simba ilitolewa katika robo fainali ya Kombe la Kagame ilionyesha udhaifu mkubwa katika beki yake.

Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, alishindwa kupata kombinesheni nzuri na alilazimika kuwabadilisha mara kwa mara, Shomari Kapombe, Obadia Mungusa, Juma Nyosso, Masombo na Shamte.

Klabu hiyo ilipata pigo zaidi baada ya Amir Maftah kuumia.

Monday, July 30, 2012

30 JUL. EXCLUSIVE; MGOMO WA WALIMU WAANZA RASMI


TAARIFA AMBAZO BLOG HII IMEZIPATA KUTOKA MIKOA MBALIMBALI KUWA ULE MGOMO AMBAO ULIPANGWA KUFANYWA NA WALIMU NCHI NZIMA UMEANZA RASMI. BLOG HII IMEWASILIANA NA WALIMU AMBAO WAPO KATIKA MIKOA YA MBEYA, SIMIYU, GEITA NA PWANI NI KWAMBA WALIMU WAMEGOMA KWENDA KAZINI KABISA

MKOANI SIMIYU KUNA BAADHI YA WALIMU WAMEWEZA KWENDA SHULE LAKINI HAWAJAINGIA DDARASANI ILI KUUNGANA NA WALIMU WENZAO AMBAO WAPO KWENYE MGOMO WA KUTOKWENDA SHULE KABISA.

BLOG HII ILIWEZA KUWASILIANA NA BAADHI YA WALIMU WALIOPO MKOANI MBEYA WAO WAMESEMA HAWAJAENDA KABISA KAZINI.BAADHI YA WALIMU AMBAO WALIENDA KAZINI HAWAKUFUNDISHA BALI WALIWATANGAZIA TU WANAFUNZI ANAYETAKA KUBAKI SHULE ABAKI ASIYETAKA ARUDI NYUMBANI

KUTOKA MKOANI PWANI BLOG HII IMEPATA TAARIFA KUWA KUNA BAADHI YA MAENEO AMBAYO WALIMU WALIOENDA SHULE WALIWEZA KUCHAPWA NA WATU WASIOJULIKANA, HALI ILIYOPELEKEA WALIMU WENGI KURUDI NYUMBANI.

JIJINI MWANZA PIA HALI ILIKUWA KAMA MIKOA MINGINE KWANI WALIMU WA BAADHI YA SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI HAWAKUFIKA KABISA KATIKA SHULE HIZO


BLOG HII ITAENDELEA KUWAPA MATUKIO AMBAYO ITAKUWA INAYAPATA KUHUSIANA NA MGOMO HUU

Sunday, July 29, 2012

29 JUL.NGORONGORO HEROES 1 NIGERIA 2


TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imeanza vibaya kampeni za kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika nchini Algeria mwakani, baada ya kufungwa na Nigeria mabao 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, Nigeria, Flying Eagles walioonekana kutumia wachezaji waliozidi umri, walikuwa mbele kwa mbele kwa mabao 2-0 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya pili, yote yakitiwa kimiani na mshambuliaji wa Enugu Rangers, Achaji Gero katika dakika ya pili na 44.

Kipindi cha pili, Ngorongoro walibadilika na kucheza vizuri, wakiwazidi wapinzani wao kumiliki mpira na kasi ya mchezo na hatimaye wakafanikiwa kupata bao la kufutia machozi, lililofungwa na Atupele Green dakika ya 50, akimalizia krosi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.

Ngorongoro wangeweza kupata mabao zaidi, kama wangecheza soka ya chini, lakini kutia krosi za juu kwenye lango la Nigeria ilikuwa ni kuwatesa washambuliaji wao wafupi, Atupele na Simon Msuva.

Kwa matokeo hayo sasa, Ngorongoro wanahitaji ushindi wa angalau wa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano Nigeria wiki mbili zijazo, ili kusonga mbele

Baada ya mchezo huo, kocha wa Ngorongoro Heroes, Mdenmark Jakob Michelsen alisema kwamba ataongeza nguvu katika kikosi chake kwa kuwaita wachezaji wawili wanaocheza nje, kiungo Adam Nditi wa Chelsea na Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), sambamba na nyota wengine waliokwenda Ujerumani n TSU kwenye michuano ya Fallerhof.

Huu unakuwa mchezo wa tatu mfululizo Ngorongoro inafungwa nyumbani tangu Michelsen apewe timu hiyo akirithi mikoba ya Kim Poulsen, ambaye amepandishwa timu ya wakubwa, Taifa Stars.

Awali, Ngorongoro walifungwa mechi mbili za kirafiki na Rwanda mwezi huu, moja Chamazi 2-0 na nyingine Taifa, 2-1.

Katika mchezo, kikosi cha Ngorongoro kilikuwa; Barwany Khomein, Omega Seme, Jamal Mroki, Issa Rashid, Ruhana Samir, Yarouk Ramadhan, Kheri Salum/Jerome Lambele, Frank Damayo, Simon Msuva, Atupele Green na Ramadhan Singano.
Flying Eagles; Samuel Okani, Hassan Abubakar, Ahiyu Mohamed, Ikechukwu Okine, Chizoba Amaefule, Agboyi Oubokha, Moses Orkuma, Chidi Osochukwu, Yahaya Adam/Harrison Egbune, Achaji Gero na Aminu Omar/Uchw Agbo.

29 JUL. WABUNGE WALA RUSHWA WAKUBWA HAWA HAPA

WAKATI wabunge wakitoa tuhuma nzito dhidi ya wenzao wanaodaiwa kujihusisha na ufisadi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imebainishwa kuwa wabunge wenye tabia hiyo ni watano, watatu kutoka chama tawala CCM na wawili upinzani.

Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zimeeleza kuwa baadhi ya wabunge hao wanatoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, huku wengine wakitoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao wamedaiwa kuwa wamekuwa wakitumia nafasi zao za ubunge na ujumbe wa kamati kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi ndani ya shirika hilo la umma.

Gazeti hili limefanikiwa kupata majina ya wabunge hao, ambayo leo hatutayataja kwa sababu za kitaaluma.

Baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni juzi na jana walisema kuwa, wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini hawapendi kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.

Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa jana na Mbunge Vita Kawawa wa Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa, Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.

“Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa kifungu cha 55 (3)f mbunge au waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe. Sasa naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo," Kawawa alisema.

Aliliomba pia Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati nyingine zilizolalamikiwa kwa rushwa. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge.

Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono Spika wa Bunge, Anne Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.

"Ninakubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na zingine ambazo zitatajwa kwenye tuhuma hizo. Nalipeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, halafu kama ni kutajwa (wabunge hao), basi tutapata mwongozo wa kamati hiyo." alisema Spika Makinda na kuongeza:

"Nasema kwa dhati kabisa, kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge hili. Wabunge mkae vizuri. Kama kuna baadhi yetu wanaenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi, tutawezaje kuisimamia Serikali?"

Mbunge Zedi
Baada ya Spika kutangaza kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Seleman Zedi alisema kuwa ameshtushwa na uamuzi huo na anasubiri uamuzi wa Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge.

"Nimeshtushwa sana na uamuzi huo, lakini tusubiri Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge," alisema Zedi.

Waziri Muhongo
Akihitimisha hoja ya wizara yake bungeni jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa baadhi ya wabunge ambao wanashiriki kwenye vikao vya uamuzi vya Tanesco kama wajumbe, wamekuwa wakilihujumu shirika hilo kwa njia mbalimbali ikiwamo kufanya nalo biashara.

"Shirika liliwahi kulipa Pauni za Uingereza 50,000 kwa ajili ya kununua vipuri, lakini kilicholetwa nchini ni masanduku ya misumari,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza;

“Hata katika nguzo za umeme kuna biashara inaendelea. Tunajua kuwa nguzo hizo zinazalishwa Iringa na kupelekwa Mombasa kisha kurudishwa nchini kwa maelezo kwamba zimetoka Afrika Kusini."

Waziri Muhongo alisema kuwa mbali na ufisadi huo, baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini wamewahi kuliuzia shirika hilo matairi ya magari kwa bei kubwa, bidhaa ambayo hata hivyo alisema haina ubora unaokubalika.

"Baadhi ya wabunge wanafanya biashara na Tanesco; niseme tu kuwa, hii siyo sahihi. Lakini niombe kwamba mjadala huu tuufunge kwa sababu, tayari tumekabidhi suala hilo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)" alisema Waziri Muhongo.

Waziri Muhongo pia alizungumzia jinsi baadhi ya watu na kampuni zinavyoiibia Tanesco kupitia mita za Luku ambapo aliwataja watu hao kuwa ni pamoja na Shule za St. Mary's zinazodaiwa Sh10.5 milioni, Access Bank, Tawi la Tabata Matumbi Sh13.8 milioni na Hoteli ya Akudo Paradaise ya Kariakoo inayodaiwa Sh25.5 milioni.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa wadaiwa hao hutumia umeme kinyume na utaratibu,wahusika wote walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi baada ya kufanyika kwa uchunguzi.

“Baada ya kufanya uchunguzi na kubaini kuwapo kwa watu wanaotumia umeme bila kulipia na kuisababishia Tanesco hasara, tumeamua kuwachukulia hatua ikiwamo kuwafikisha polisi,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza:

“Inaonyesha wazi kwamba wizi wa umeme wa Luku umekuwa ukifanyika mara kwa mara na kwamba baada ya kuwakamata hawa, uchunguzi utaendelea na wengine watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.”

Jenista Mhagama

Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama alisema kuwa, amepokea kwa masikitiko taarifa hizo za wabunge wa CCM kuingia katika tuhuma hizo, lakini akasema namna nzuri ya kushughulikia tatizo hilo ni vyombo vya dola kufanya uchunguzi makini ili kujiridhisha na kisha hatua za kisheria kufuatwa.

"Ni taarifa mbaya kwa kweli, lakini mimi niiombe Serikali itusaidie kufanya uchunguzi ili ukweli ubainike na hatua zichukuliwe," alisema Mhagama.

Mbunge Silinde
Naye Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde alisema: "Kwa kuwa tumesikia, kama kambi tutafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo. Tutakaa kikao cha kuamua nini cha kufanya. Pia tutatoa tamko juu ya mwenendo mzima wa hizi tuhuma na Bunge kwa ujumla.”

Zitto
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma ambayo imeunganishwa kwenye tuhuma hizo, Zitto Kabwe, alisema tuhuma hizo anazisikia, lakini anaziona kama siasa za majitaka kwa sababu zinarushwa bila ushahidi wowote.

"Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini. Mimi binafsi sijahongwa na mtu yeyote wala mimi sijamtetea mtu isipokuwa natetea taratibu kufuatwa," alisema.

Zitto alibainisha kuwa anaamini tuhuma hizo zimetokana na hasira za yeye kupinga posho za wabunge na sasa wameona hilo ndilo eneo la kumkomoa.

"Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza:

"Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'.”

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini(Chadema) alishauri pia Spika wa Bunge kutumia Kamati ya Maadili kuchunguza tuhuma hizo kwa kuwa hazipaswi kuachwa zikapita hivihivi.

John Cheyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo alisema anasikitika kuona Bunge ambalo kimsingi ni kitovu cha uadilifu limeanza kuvamiwa na mafisadi.

"Very unfortunate, (bahati mbaya sana) Bunge ambalo ni kilele cha uadilifu, nyumba ya waheshimiwa, ambako kunatarajiwa high level of intergrity (uadilifu wa hali ya juu), kuanza kutumika kama perpets (vibaraka) wa mafisadi," alisema.

Cheyo aliongeza: "Ninalaani sana kitendo hicho, lakini niwaambie viongozi wapya wa Wizara ya Nishati na Madini kuwa, waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na nguvu yao ni wabunge wengi wema, ambao watawaunga mkono. Wasikate tama," alisema.

Mjadala ya wabunge

Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda aliliomba Bunge kufanya uchunguzi ili kuwabaini wabunge wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Alisema baadhi ya wabunge wanatumia nafasi zao vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuiyumbisha Serikali.

“Namwomba Spika na timu yake yote ikaona kuna haja ya kufanya uchunguzi kwa wabunge ili kuweza kuwabaini wanaotumia nafasi zao vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ilikuiyumbisha Serikali ,” alisema Shibuda

Mbuge Kangi

Naye Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora alitaka Waziri wa Nishati na Madini awataje wabunge aliowatuhumu ili kuonyesha usawa hasa baada ya kuwataja kwa majina watuhumiwa wengine katika ufisadi wa Tanesco na wale wanaoliibia umeme shirika hilo la umma.

"Tunaomba waziri asema kwa nini asiwataje hao wengine wakati tayari ametutajia kina Freddy na Veronica William Mhando na taasisi za St Mary? " alihoji.

Hoja hiyo ya Lugora ilitupwa na Spika wa Bunge Anne Makinda aliyesema kuwa jambo hilo lina taratibu zake.

Kamata
Vicky Kimata (Viti Maalumu) nusura amwage machozi bungeni juzi jioni, alipozungumza kwa uchungu kupinga hatua ya wabunge hao kujihusisha na ufisadi, huku akieleza kuwa nchi imefika pabaya.

'Watanzania tumefikia hapo! Watu wanatengeneza mgawo wa umeme ili kujipatia hela, Jamani...jamani.. Hammwogopi hata Mungu!"

Said Mussa Zuberi alipendekeza itungwe sheria ya kuwanyonga mafisadi na wahujumu uchumi kwa kuwa matendo hayo pia ni uuaji.

"Katika taifa letu tuna wadudu sijui tuwaite mchwa ambao wanaharibu yaliyotengenezwa kwa maslahi yao. Nawashauri wananchi kwa kuwa sasa tuko kwenye suala la Katiba, wasisahau kupitisha sheria ili watu wahujumu uchumi tuwaue, tena kwa risasi.
SOURCE; GAZETI LA MWANANCH

29 JUL.CWT: Mgomo wa walimu upo palepale

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesisitiza kuwa, mgomo wake uliopangwa kuanza leo upo palepale.
Hatua hiyo ya CWT imekuja siku moja baada ya Serikali kutangaza kuwa mgomo huo ni batili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba ameitaka Serikali kuacha vitisho dhidi ya walimu.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwalazimisha walimu kujaza fomu zinazowataka kuorodhesha majina yao na shule wanazofundisha na kueleza kama wanaunga mkono mgomo huo au la.CWT imesema walimu wanatakiwa kushiriki mgomo huo kwa kuwa ni halali na umeitishwa na chama hicho kwa kufuata taratibu zinazotakiwa.

Mukoba alisema, Baraza la CWT lilitoa notisi ya saa 48 kuanzia jana (juzi) saa 8 mchana, ambayo inamalizika leo saa 8 mchana, kisha kutangaza rasmi kuwa utekelezaji wa azma yao ya kugoma unaanza kesho.

“Walimu wataanza mgomo rasmi Jumatatu (kesho), kwa kubaki nyumbani bila ya kwenda kazini hadi watakapotaarifiwa vinginevyo na Rais wa CWT,” alisema Mukoba.

Alisema kuwa, wanachama waliopiga kura kuamua kuwepo kwa mgomo walikuwa 183,000 ambapo kati yao 153,000 waliunga mkono azimio hilo wakiwa sawa na asilimia 95.7 ya wanachama, hivyo kuhalalisha mgomo huo.
Hata hivyo, Mkoba alisema kuwa mgomo huo hautahusiana na zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 26, mwaka huu ambapo aliwataka walimu kushiriki kikamilifu.

“Walimu wanahakikishiwa kuwa mgomo hautaathiri utumishi wao kwa kuwa umezingatia sheria, ingawa tunategemea kuwapo kwa vitisho na propaganda nyingi kutoka kwa waajiri wetu,” alisema Mukoba.Mukoba alieleza kuwa mgogoro uliotangazwa na walimu kupitia CWT ulishindikana kusuluhishwa na msuluhishi aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

"Nawataka walimu wote nchini kuungana na kuhakikisha kuwa mnashiriki zoezi hili lenye lengo la kumshinikiza mwajiri wetu (Serikali) kusikiliza madai yetu," alisema.

Alhamisi wiki hii CWT ilitangaza mgomo wa walimu nchi nzima kupinga Serikali kushindwa kuwatimizia madai yao ya siku nyingi ikiwamo ongezeko la mishahara.

Madai ya walimu
Madai ambayo walimu wamekuwa wakiitaka Serikali kuyatafutia ufumbuzi ni pamoja na ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa Sayansi asilimia 55, asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya sanaa na posho kwa walimu wanaoishi katika mazingira magumu.Mgogoro kati ya CWT na Serikali umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa, ambapo licha ya ahadi ya kulipwa madai hayo, fedha zimekuwa hazikidhi ukubwa wa tatizo na kusababisha madeni kurundikana.

Hata hivyo, Serikali juzi ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Paniel Lyimo ikieleza kuwa walipokea notisi kutoka CWT kuwataarifu juu ya mgomo utakaofanyika kesho nchi nzima.
“Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za kujadili na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha masilahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala kwa maelewano kwa kutumia vyombo na ngazi mbalimbali,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa shauri hilo liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na kwamba juzi mchana pande zote mbili zilifika Mahakamani na Mahakama ikaamuru pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo Jumanne.

Kauli ya WizaraNaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipoulizwa jana kuhusu uamuzi wa walimu kuendelea na mgomo, alisema hawezi kuzungumzia hilo yuko safarini kuelekea Mbeya.

“Siwezi kuzungumza nipo safarini kuelekea Mbeya na hatuwezi kuelewana hivyo, mtafute Waziri atazungumzia,” alisema Mulugo.

Hata hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipopigiwa simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokewa.

Walimu Bunda Kutoka Bunda, Ahmed Makongo anaripoti kuwa siku moja baada ya CWT, kutangaza mgomo wa walimu usiokuwa.

Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Bunda, Francis Ruhumbika aliwataka walimu wote wilayani humo kushiriki kwenye mgomo huo bila kwenda kwenye vituo vyao vya kazi, baada ya notisi ya masaa 48 kumalizika.

Akizungumza na mjini Bunda jana, Ruhumbika pia amewataka walimu wote wilayani humo, kutokukubali kusaini fomu yoyote itakayoletwa na viongozi wa Serikali, itakayowataka walimu wanaounga mkono au wasioutaka mgomo kusaini fomu hiyo.

Arusha Kutoka Arusha Peter Saramba, anaripoti kuwa CWT Wilaya za Arumeru na Manispaa ya Arushawametangaza kuunga mkono tamko la mgomo usio na mwisho uliotangazwa na Baraza Kuu la Taifa la chama hicho.Wakitoa tamko mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi za CWT Mkoa wa Arusha jana, Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Arumeru, Elifas Ole Saitabauna Martin Godfray kutoka Manispaa ya Arusha walisema hakuna njia nyingine ya kusimamisha mgomo huo isipokuwa Serikali kutekeleza madai yao. “Sisi ngazi ya wilaya na mkoa tunaunga mkono mgomo huo na tunawataka walimu wasiogope vitisho, atakayetishiwa atoe taarifa mara moja kwa uongozi wa eneo lake,” alisema Ole Saitabau.
SOURCE; GAZETI LA MWANANCHI

29 JUL.SAID BAHANUZI NDIO MFUNGAJI BORA WA KAGAME CUP


WAFUNGAJI KAGAME 2012:

Said Bahanuzi Yanga SC 6

Taddy Etikiama AS Vita 6-1 - Moja la penati

Hamisi Kiiza Yanga SC 5

John Bocco Azam FC 5

Suleiman Ndikumana APR 3

Abdallah Juma Simba SC 3

Leonel St Preus APR 2

Didier Kavumbagu Atletico 2

Feni Ali URA 2

Robert Ssentongo URA 2

29 JUL.NGOROGORO HEROES VS NIGERIA LEO


TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na vijana wenzao wa Nigeria, Flying Eagles katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Menmark Jakob Michelsen na Nahodha wa timu hiyo, kiungo Omega Seme wamesema timu yao iko tayari kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.

Michelsen amesema timu yake imepata mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Rwanda, lakini pia aliishuhudia Flying Eagles ikicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) uliofanyika Julai 24 mwaka huu jijini Kigali.
Timu iko vizuri na wachezaji kama Frank Domayo, Simon Msuva na Ramadhan Singano ambao pia wanachezea timu A (Taifa Stars), hivyo uzoefu wao ni muhimu kwa mechi ya kesho.

“Nigeria ni mabingwa watetezi wa michuano hii kwa hiyo tunatarajia upinzani mkubwa, lakini tumejiandaa kwa hilo. Nigeria ni nchi yenye mfumo mzuri wa timu za vijana, na sisi tunaelekea huko huko” amesema Michelsen.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Flying Eagles, John Obuh amesema haijui vizuri Ngorongoro Heroes lakini anaiheshimu kutokana na ukweli kuwa inacheza raundi ya pili baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.

“Sina mchezaji yeyote anayecheza mpira wa kulipwa nje ya Nigeria, lakini tumekuja kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza raundi ya mwisho na hatimaye tucheze fainali mwakani,” amesema Obuh aliyefuatana na nahodha wake Samuel Okan ambaye ni mlinda mlango.

Katika mechi hiyo, itakayochezeshwa na refa Moses Osano, akisaidiwa na Peter Keireni na Elias Wamalwa, Thomas Onyango mezani, viingilio vitakuwa Sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A ni sh. 10,000.
Osano atasaidiwa na Peter Keireini na

Saturday, July 28, 2012

28 JUL.YANGA BINGWA KAGAME CUP 2012


YANGA YA TANZANIA IMEWEZA KUUTETEA UBINGWA WAKE WA KOMBE LA KLAB BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA AZAM FC GOLI 2-0

GOLI LA KWANZA LA YANGA LILIFUNGWA NA HAMIS KIIZA DK 44 YA KIPINDI CHA KWANZA BAADA KUTOKEA UZEMBE WA MABEKI WA AZAM KUJICHANGANYA,GOLI LA PILI LILIFUNGWA NA SAIDI BAHANUZI DK YA 45 YA KIPINDI CHA PILI.

KATIKA MCHEZO WA AWALI WA KUSAKA MSHINDI WA TATU TIMU YA VITA YA CONGO DRC IMEWEZA KUFANIKIWA KUCHUKUA NAFASI YA TATU BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA APR YA RWANDA GOLI 2-1

28 JUL.KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA DHIDI YA AZAM FC KWENYE FAINALI YA KAGAME CUP 2012


1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1

2.Stephano Mwasika - 3

3.Oscar Joshua - 4

4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23

5.Kelvin Yondan - 5

6.Athuman Idd 'Chuji' - 24

7.Rashid Gumbo - 16

8.Haruna Niyonzima - 8

9.Said Bahanunzi - 11

10.Hamis Kiiza 'Diego' - 20

11.David Luhende - 29

Subs:
1.Yaw Berko - 19

2.Ladislaus Mbogo - 28

3.Juma Seif 'Kijiko' - 13

4.Idrisa Rashid - 12

5.Shamte Ally - 15

6.Nizar Khalfan - 7

7.Jeryson Tegete - 10

Head Coach: Tom Saintfiet

Ass Coach : Fred Felix Minziro

Goalkeeper Coach: Mfaume Athuman

Team Doctor : Dr Suphian Juma

Kit Manager : Mahmoud Omary (Mpogolo)

Massagist : Jacob Onyango

Team Manager : Hafidh Saleh

28 JUL.FAINALI YA KAGAME LEO, YANGA VS AZAM F.C




KISASI cha milioni nane! Hivi ndivyo unavyoweza kulielezea pambano la fainali ya Kombe la Kagame baina ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Azam FC kuanzia saa 10:00 jioni leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao utatanguliwa na ule wa baina ya Vita ya Congo na APR ya Rwanda kwa ajili ya kusaka mshindi wa tatu, unatarajiwa kuwa mkali na msisimko mkubwa.

Yanga itaingia na hasira ya kutaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 na Azam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Machi 10.

Pamoja na Yanga kutaka kulipa kisasi cha mabao hayo, pia ina uchungu na wachezaji wake kufungiwa na klabu kutakiwa kulipa faini ya Sh milioni nane kutokana na vurugu za mechi ile hivyo kuzidisha hasira za kushinda mchezo huu.

Yanga imeingia fainali baada ya kuifunga APR bao 1-0 wakati Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuichapa AS Vita mabao 2-1.

KUKUTANA
Timu hizo zinakutana mara ya tatu mwaka huu, mara ya kwanza zilipambana kwenye Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mapema Januari na Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3- 0.

Kisha zikakutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Azam kushinda mabao 3-1.

KISASI
Mchezo huo pia utakuwa wa visasi kutokana na tukio lililotokea kwenye pambano la Machi 10 kwani wachezaji wa Yanga wakiongozwa na beki Stephano Mwasika walimpiga mwamuzi, Israel Nkongo.

Walifanya hivyo baada ya kukasirishwa na kitendo cha mwamuzi huyo kumtoa kwa kadi nyekundu kiungo mchezeshaji, Haruna Niyonzima, katika dakika ya 13 ya mchezo huo. Niyonzima alitolewa baada ya kuzozana na mwamuzi.

Mapema Niyonzima alikuwa na kadi ya njano aliyopewa baada ya kucheza rafu na baadaye kuonyeshwa njano nyingine na hivyo nyekundu kufuata, kitendo hicho kilitafsiriwa na wachezaji wa Yanga kuwa mwamuzi alikuwa anaibeba Azam.

Ndipo ikaanzisha vurugu iliyofanya Nadir Haroub Cannavaro naye atolewe kwa kadi nyekundu.

Kutokana na tukio hilo Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) liliwafungia Mwasika na Jerry Tegete kutocheza mechi zote zilizosalia za ligi na faini ya Sh milioni mbili kwa kila mmoja wao.

Pia ilimfungia beki Cannavaro kutocheza michezo mitatu na faini ya Sh milioni moja huku pia ikiwafungia viungo Nurdin Bakari na Omega Seme kukosa mechi tatu na faini ya Sh milioni moja kila mmoja.

Yanga ina ghadhabu na tukio lile na wametamba lazima washinde ili kukata ngebe za Azam ambao ni maarufu kwa jina la Wana Lamba Lamba.

Azam nao baada ya kuitoa Simba kwenye robo fainali, inaamini itaendeleza rekodi yao ya kuishinda Yanga.

UBORA WA TIMU
TIMU zote zina ubora wa hali ya juu kuanzia ushambuliaji, viungo na hata safu ya ulinzi.

Lakini vita kubwa itakuwa kati ya washambuliaji watatu, John Boko Adebayor wa Azam, Said Bahanuzi na Hamis Kiiza wa Yanga ambao wote wana mabao matano na kila mmoja atataka kuongeza ili kuchukua Kiatu cha Dhahabu na kumzidi mshambulaiji wa AS Vita Etekiama Taddy mwenye mabao sita.

Adebayor ambaye alimtungua kipa Juma Kaseja mabao matatu Hat Trick, anatarajiwa kuongoza maangamizi sambamba na Kipre Tcheche na Mrisho Ngasa ambaye anaweza kuanza.

Katika mchezo uliopita wa nusu fainali dhidi ya AS Vita, Ngassa alipangwa kikosi cha kwanza na kuipeleka timu yake fainali licha ya kuwepo taarifa kuwa haelewani na kocha, Stewart Hall.

Yanga yenyewe itakuwa ikiwategemea washambuliaji wake pacha Bahanuzi na Kiiza ambao wameunda kombinesheni ya hatari katika michuano hiyo na kocha wao amewapa majukumu ya kuhakikisha Azam inalala na kuipa ubingwa tena timu yao.

Lakini kubwa jingine linalosubiriwa ni kuona ubora wa viungo wachezeshaji Niyonzima na Salum Abubakary Sure Boy wa Azam, ambao wamesababisha mjadala mkubwa miongoni mwa washabiki wa soka kuwa nani mkali baina yao.

Wote wamekuwa wakicheza soka la kiwango cha juu katika timu zao na kitendawili hicho kitateguliwa kwa yeyote atakayempoteza mwenzake uwanjani ndiye atakayeibuka mshindi.

Pia sifa kubwa ya timu hizo mbili ni ubora wa safu ya ulinzi hasa beki ya kati kwani wakati Yanga kuna 'Cannavaro' na Kelvin Yondani Vidic, Azam kuna Aggrey Morris na Said Morad.

Hivyo washambuliaji wa timu hizo wanahitaji akili za kiwango cha juu kuhakikisha wanazipenya ngome hizo na kwenda kufunga mabao.

KAULI ZA MAKOCHA
Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet amesema anafurahia ubora wa kikosi chake na jinsi wachezaji wake wanavyocheza soka kwa nidhamu na anaamini watazidi kuwafurahisha mashabiki wao.

"Kila mara nimekuwa nikisema nataka wachezaji wanaojituma na kujitolea uwanjani na nafurahi wachezaji wangu wananielewa na kufuata kile inachotaka na naamini wataendelea mambo mazuri Jumamosi (leo) dhidi ya Azam na kuweza kuibuka na ushindi," alisema.

"Azam ni kati ya timu bora Tanzania, inacheza soka la pasi nyingi lazima tuzibe mianya na tusiwaruhusu watuchezee mpira naamini tutawashinda."

Kocha wa Azam, Stewart Hall alisema anaiheshimu Yanga kutokana na kiwango walichokionyesha katika michuano hii, lakini amewataka waamuzi kuchezesha kwa haki ili mshindi apatikane kihalali.

"Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wa kiwango cha juu, lakini tumejiandaa kuwakabili na tunachoangalia ni kuweka historia mpya Tanzania na hata nje ya Tanzania kwa kutwaa kombe hili," alisema Hall.

ZAWADI
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka dola 30,000 (Sh 47.4 milioni), mshindi wa pili atajinyakulia Dola 20,000 (Sh31.6 milioni) na wa tatu atajipatia Dola 10,000 (Sh 15.8 milioni).

28 JUL.Simba kusajili bonge la beki wa Rwanda


SIMBA inamwania beki kisiki wa APR ya Rwanda, Mbuyu Twite, kwa ajili ya kujiimarisha kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Kiongozi mmoja wa juu wa klabu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina, aliliambia Mwanaspoti kuwa wamevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na wameanza mazungumzo naye kuhakikisha anaichezea timu hiyo msimu ujao.

"Kila mtu ameona uwezo wake, ana umbo dogo lakini shughuli yake uwanjani imeonekana, ni beki mzuri na nafikiri atatusaidia kuziba pengo la Yondani maana timu yetu sasa hivi ina tatizo kubwa katika nafasi hiyo," alisema.

"Tumeshaanza mazungumzo naye na tunaendelea naamini atakubali, mambo yakiwa mazuri tutaweka wazi kila kitu."

Twite alikiqmbia chanzo chetu kuwa ameshamaliza mkataba na klabu ya APR, kwa hiyo milango iko wazi kwa timu yoyote inayotaka kumsajili, lakini anachoangalia ni maslahi tu.

"Hapa naichezea APR kwa makubaliano, lakini mkataba wangu na timu hii umemalizika tayari. Ila milango iko wazi kwa timu yoyote inayonihitaji, mpira kazi yangu naweza kucheza popote," alisema Twite, ambaye ana pacha wake Kabange Twite aliye naye APR.

Twite ameonyesha soka la kiwango cha juu katika nafasi ya beki wa kati kwenye michuano ya Kagame inayomalizika leo Jumamosi na amekuwa msaada mkubwa kwa APR.

Mchezaji huyo ambaye pia humudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, anakumbukwa vizuri na kipa wa Simba, Juma Kaseja. Ndiyo aliyemfunga mabao mawili ya aina moja kutoka umbali wa mita 40 wakati huo Kaseja akiidakia Yanga msimu wa 2008.

Simba inahaha hivi sasa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba kwenye michuano hiyo ya Kagame baada ya kuondoka kwa Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga.
SOURCE; GAZETI LA MWANASPOTI

28 JUL.Kaseja mbona wangu tu - Bocco


Baada ya kumfunga kipa namba moja wa Simba, Juma Kaseja mabao matatu katika mechi moja ‘hat-trick’, mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco amesema ataendelea kumtungua zaidi kipa huyo.

Kaseja alifungwa mabao hayo katika mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa, Jumanne iliyopita, iliyomalizika kwa Simba kufungwa mabao 3-1.

Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Bocco kumfunga Kaseja, mechi ya mwisho ilikuwa ya fainali ya Kombe la Urafiki ambapo akitokea benchi na kufunga kwa kichwa.
Bocco amesema juhudi binafsi na kujituma ndivyo vinamuwezesha kumfunga kipa huyo anayeaminika kuwa bora zaidi nchini kwa sasa.

“Nimekuwa nikimfunga Kaseja kila wakati kutokana na juhudi binafsi na kujituma uwanjani. Natambua majukumu yangu ndani ya uwanja na kufuata maelekezo ninayopewa na kocha wangu, nitaendelea kumfunga Kaseja kila tutakapokutana,” alisema Bocco.

28 JUL.BROGGER KISTUDIO ZAIDI

28 JUL.Kaburu anahatia kupanga kumuua Mandela


Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.

Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.
Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.

Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.

Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.

Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.
SOURCE;BBC

28 JUL.Msaada kwa Rwanda wasitishwa


Serikali ya Uholanzi imesitisha msaada wa dola milioni 6.15 kwa Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na ufadhili wa waasi katika Jamuhuri ya kjidemokrasia ya Congo.

Hatua hii inajiri siku kadhaa baada ya Marekani kutangza inanuia kupunguza msaada wa kijeshi kwa Rwanda.

Hata hivyo Rwanda imekuwa ikikanusha madai ya umoja wa mataifa kuwa inafadhili kundi la waasi wa M23 mashariki mwa DR Congo.

Waasi hao walianza kutoka jeshini kuanzia mwezi Aprili na hadi kufikia sasa takriban watu 200,000 wametoroka makwao kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi na waasi hao.

Hatua hii ya Udachi inajiri baada ya afisaa mkuu wa umoja wa mataifa kuambia BBC kuwa wanajeshi wanaotoka katika jeshi la DRC wamekiri kusajiliwa na Rwanda.

Mnamo siku ya Alhamisi, Umoja wa mataifa uliripoti kuwa wana

jeshi wake walisaidia jeshi la DRC kuwafukuza waasi hao kutoka mji wa Goma kwa kutumia helikopta pamoja na magari ya kijeshi.

SOURCE; BBC

Friday, July 27, 2012

27 JUL. BREAKING NEWZ; NYUMBA YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA RUAHA, MKOANI MOROGORO YACHOMWA MOTO


HABARI AMBAZO BLOG HII IMEZIPATA KUTOKA RUAHA, MKOANI MOROGO NI KWAMBA NYUMBA YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA RUAHA BWANA MBWILO IMECHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA USIKU WA KUAMKIA JANA.

INASEMEKANA KUWA VITU VINGI VILIWEZA KUUNGUA HUO USIKU, BAADHI YA WASAMALIA WEMA WALIWEZA KUFIKA KUMSAIDIA KUWEZA KUOKOA BAADHI YA VITU

POLISI BADO INAAENDELEA NA UCHUNGUZI YA WAHUSIKA WA TUKIO HILI

BLOG HII ITAENDELEA KUWAJUZA JUU YA TUKIO HILI KADIRI TAARIFA ZITAKAPOPATIKANA

27 JUL.SHIGONGO AELEZA UKWELI KUHUSU JOSE CHAMELEONE




MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza kurejeshewa paspoti yake.

Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.

Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.

“Tulipokubaliana nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo.

Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha.

“Chameleone alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advace ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.

“Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti wake kwetu sisi.

“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.

“Ndugu zangu, sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu.

Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.

“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya.

“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo.

Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!
SOURCE; GLOBAL PUBLISHERZ

27 JUL.EXCLUSIVE;AFANDE SELE AFUNGUKIA KUGOMBEA UBUNGE 2015


MFALME wa Rymes, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ amefungukia ishu ya yeye kugombea ubunge kwenye Jimbo la Morogoro mwaka 2015 na kusema kuna wabunge wawili wanamshashiwi kuchukua uamuzi huo kutokana na mambo wanayoyafanya.

Akipiga stori na WEBSITE ya Millardayo, Afande Sele alisema kuwa ni wengi wanaomvutia katika hilo lakini hasa ni Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Halima Mdee wa Kawe na Burhani wa Lindi.

Alisema: “Mtu kama Zitto Kabwe ni mtu ambaye ananipigia simu mara nyingi na kunishauri, namheshimu sana, yuko pia dada Halima Mdee. Hawa wananionyesha kitu flani ambacho naweza kukifanya vilevile, kwa kifupi wengi wanaonivutia wapo vyama vya upinzani,” alisema msanii huyo na kuongeza:

“Kuna vyama saba vya kisiasa vilivyoniita nijiunge navyo kugombea Ubunge lakini viwili ndiyo vyenye nafasi kubwa ambavyo ni Chadema na CUF.

27 JUL.Sunzu, Kaseja waitwa DR Congo



KOCHA wa Vita Club ya DR Congo, Lusadisu Medard amesema amefurahishwa na viwango vya wachezaji wa Simba, mshambuliaji Felix Sunzu na kipa Juma Kaseja na angependa wajiunge naye katika kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Medard alisema wachezaji hao wameonyesha uwezo mkubwa tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame 2012 na kudai kuwa anatamani waichezee Vita.

Alisema pamoja na kwamba Kaseja ni mkongwe, uwezo wake umezidi kuimarika zaidi akiwa langoni huku Sunzu akionyesha kujiamini zaidi kila anapolikaribia lango la mpinzani licha ya kwamba alifunga bao moja tu katika michuano hiyo.
Aliongeza kuwa kosa kubwa wanalolifanya Simba ni baadhi ya wachezaji kutojiamini japokuwa wana timu nzuri.

“Kuna yule mchezaji namba kumi (Sunzu), anacheza vizuri sana akiwa na mpira naona ni jinsi gani anaumiliki kwa ustadi, ni straika mzuri sana, ningependa siku moja acheze kwenye timu yangu. Kaseja uwezo wake pia unaonekana kuongezeka kwa kuwa nilishawahi kumuona kipindi cha nyuma, bado yupo vizuri, hao ndiyo ningependa kuwaona mara kwa mara,” alisema Medard.

27 JUL.Fabio Capello ni kocha mpya Urussi



Chama cha mpira cha Urussi kimethibitisha habari za kua aliyewahi kua Kocha wa klabu ya Real Madrid na England Fabio Capello ndiye Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Punde baada ya kutangazwa Capello mwenye umri wa miaka 66 amesema shabaha yake ni ufanisi wa haraka. Ledngo langu ni kuiwezesha Urussi kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil, alisema Capello.

Nilipomaliza kazi ya England, nilikua na ghadhabu na nilitaka kuendelea kufanya kazi. Ukweli ni kwamba nataka kutimiza malengo yenu Urussi na kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.

Capello alikuwa kwenye orodha ndefu iliyokuwa na majina ya magwiji kama Harry Redknapp, ambaye chama cha mpira cha Urussi kilimtaka awe Kocha wake mpya.

Kocha huyo aliacha sifa ya kiwango kikubwa cha ushindi kuliko waliomtangulia England akishinda asili mia 67% ya mechi ingawa Timu yake ilipata shida kwenye mashindano ya Kombe le Dunia nchini Afrika ya kusini mwaka 2010 ilipoondolewa mapema na Ujerumani.

Thursday, July 26, 2012

26 JUL.SIMBA, YANGA, AZAM ZATENGEWA MWALI MWINGINE



TIMU nane toka Tanzania Bara na Visiwani zinatarjiwa kushiriki katika michuano maalum inayokwenda kwa jinala ‘Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012’ inayotarajiwa kutimua vumbi Augusti 4 hadi 18.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema leo kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzipa makali timu shiriki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Alisema michuano hiyo itakayohusisha timu tatu bora kutoka Tanzania Bara, timu tatu bora kutoka Visiwani na timu moja iliyopanda katika pande hizio, itachezwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema timu hizo zitakuwa katika makundi mawili na hakutakuwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu zaidi ya kuwepo kwa zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa tu na tayari wameshaziandikia barua za kuzitaarifu kuhusiana na michuano hiyo.

“Nadhani hii ni nafasi nyingine kwa timu kuonyesha ushindani katika michuano hii, pia pamoja na kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi, makocha wa timu shiriki wataweza kujua kiwango kilichopo kwenye timu zao na kama kuna kasoro warekebishe kabla ya kuanza kwa ligi,”alisema.

Banc ABC ambayo imedhamini michuano hiyo kwa miaka mitatu, kupitia kwa mkurugenzi wake Mkuu Boni Nyoni alisema wameamua kuandaa michuano hiyo ili kuunga mkono jitihada za maendeleo ya soka hapa nchini.

26 JUL. AZAM NA YANGA ZATINGA FAINALI KAGAME CUP



Azam na Yanga watachuana katika mchezo wa fainali wa kombe la Kagame baada ya leo kufanikiwa kuwafunga AS Vita ya DR Congo na APR ya Rwanda katika michezo ya nusu fainali.

Azam walikuwa wa mwanzo kuting fainali baada ya kuwachapa AS Vita goli 2-1. Magoli ya Azam yamefungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 88 na John Raphael Bocco dakika 68.

Goli la AS Vita walio maliza mchezo wakiwa pungufu, baada ya beki yao kuzawadiwa kadi nyekundi katika dakika ya 40, lilifungwa katika dakika 33 kupitia kwa Afrey.

Yanga ilibidi wangoje dakika 30 zanyongeza kuiondosha APR, baada ya dakika 90 kumalizika bila nyavu kutingishwa, huku kukiwa na kosa kosa kibao.

Goli pekee katika mchezo huo wapili wa nusu fainali lilifungwa katika dakika ya 100 kupitia kwa Hamisi Kiiza na katika dakika ya 104 Godfrey Taita alizawadiwa kadi nyekundu.


Mchezo wa fainali kati ya Azam FC na Yanga itachezwa jumamosi (julai 28) uwanja wa Taifa, ukitanguliwa na wa mshindi wa 3 kati ya APR na AS Vita saa 8 mchana.

26 JUL.KIKOSI CHA AZAM LEO DHIDI YA VITA


1. Deogratius Munishi GK (27)

2. Ibrahim Shikanda (21)

3. Erasto Nyoni (6)

4. Aggrey Morris (13) Captain

5. Said Moradi (15)

6. Jabir Aziz (25)

7. Kipre Tchetche (10)

8. Ibrahim Mwaipopo (4)

9. John Bocco(19)

10. Salum Abubakar (8)

11. Ramadhan Chombo (17

26 JUL.Alves awaambia mahabiki wa Barcelona, matatizo yake na klab yameisha


Barcelona right-back Dani Alves has assured that he is no longer frustrated at the club's handling of the transfer rumours surrounding his future earlier in the summer.

The Brazil international stated on Tuesday that he was disappointed with the Blaugrana's decision to stay tight-lipped about his future at Camp Nou, with Manchester City and Anzhi Makhachkala both understood to be keeping tabs on the 29-year-old.

Barca coach Tito Vilanova later took the time to address the issue, insisting he was unaware of Alves' state of mind, and the former Sevilla stopper has now indicated that the problem is water under the bridge now.

"We have solved it," Alves told TV3. "What I wanted was to express my dissatisfaction, that is what I said that.

"Now we have talked about it and this issue is settled."

Alves scored Barca's first goal in Tuesday's 2-1 friendly victory against Hamburg at the Imtech Arena.

26 JUL.Chelsea yakamilisha usajili wa Oscar kutoka Internacional




The Blues have confirmed the acquisiton of the 20-year-old Internacional midfielder, who had also interested Tottenham and is currently representing Brazil at the Olympic Games'
The Blues confirmed the deal on their official website on Wednesday, having verbally agreed the transfer, according to the Brazilian club's president, Giovanni Luigi, earlier in the week.

No details have been released regarding the player's transfer fee or contract, but reports had claimed that the playmaker would cost around £25 million.

Oscar is currently representing Brazil at the Olympic Games and played in the Selecao's pre-tournament warm-up friendly against Great Britain.
Oscar joined Internacional from Sao Paulo in 2010 and has won the Campeonato Gaucho state championship twice with the Porto Alegre-based side.

He scored 13 goals in 44 matches in all competitions last season and has found the net six times in 20 appearances during the current campaign.
source; goal.com

26 JUL.AMFUMA MKEWE AKIZINI NA MTOTO WAO, AWAUA

AMA kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Msemo huu unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mkazi mmoja wa Kijiji cha Nghoboko wilayani Meatu mkoani hapa, Stephano Mihilu mwenye miaka 60, kudaiwa kumfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa.
Taarifa za kipolisi zilizotua kwenye dawati la Amani zinadai kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa Julai 22, mwaka huu ambapo baada Stephano kulishuhudia tukio hilo, aliwaua mama na mwanaye kwa kuwacharanga mapanga bila huruma.
“Jamaa aliporudi nyumbani, aliingia ndani na kukutana na tukio ambalo hakuwahi kulifikiria, alimkuta mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa, nadhani akili ilihama, akachukua panga na kuwacharanga wote mpaka walipokata roho,” alisema afande mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwani si msemaji wa jeshi la polisi.

HUYU HAPA KAMANDA WA POLISI WA SIMIYU
Akilizungumzia tukio hilo la kusikitisha na kushangaza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Afande Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikuwa mkewe na Boyani Stephano mwenye miaka 27 ambaye ni mtoto wao wa kumzaa.
Alidai kuwa, Mihilu alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake wa kumzaa ndipo alipopandwa na hasira kisha kuwashambulia kwa kuwakata mapanga na baadaye kuwachinja.
Kamanda Salum alisema, baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikwenda mwenyewe kujisalimisha kwenye kituo cha polisi ambapo alikabidhi silaha alizotumia katika mauaji hayo ambazo ni panga na fimbo.
“Mihilu alitembea kuanzia saa 7 usiku hadi asubuhi kwenda katika Kituo cha Polisi cha Mwahuzi wilayani Meatu kwa lengo la kujisalimisha akidai kuwa hakutaka kuwasumbua wanausalama hao kwani yeye ndiye mhusika wa mauaji hayo,” alisema kamanda huyo.

WANANCHI WANALIZUNGUMZIAJE TUKIO HILO?
Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya tukio hilo, baadhi ya wananchi wameonesha kushangazwa nalo huku wakieleza kuwa, kama ni kweli basi dunia inaelekea mwisho.
“Hivi inawezekanaje mama kufanya tendo la ndoa na mwanaye wa kumzaa? Au kuna mazingira ya ushirikina?” alihoji Juma Sagala wa Meatu.
Naye Mama Josephine, mkazi wa kijiji ambacho tukio hilo lilitokea alisema: “Hili tukio lina utata lakini kwa kuwa limeshafika kwenye vyombo vya dola, ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo wake ila limetushangaza sana.”

SOURCE; GLOBAL POBLISHERZ

26 JUL.Blatter tayari kumfunga Bale FA ikishtaki



Rais wa FIFA Sepp Blatter amesema kua mchezaji wa klabu ya Tottenham Gareth Bale anaweza kukabiliwa na vikwazo kwa kuichezea klabu yake wakati wa mashindano ya Olympic ikiwa chama cha FA kitawasilisha malalamiko yake kua mchezaji huyo ameweza kuichezea klabu yake na kukataa kuichezea Timu ya Uingereza(GB).

Bale alifunga bao la Spurs katika mchuano uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya LA Galaxy katika ziara ya klabu hiyo nchini Marekani. Bale alijiondoa kutoka timu ya GB inayojumuisha wachezaji kutoka kote Uingereza, Wales na Scotland kwa kudai majeruhi.

Gareth Bale

Chama cha mpira cha FA na shirikisho la Olimpiki hayajatoa tamko lolote kuhusu kujitokeza kwa mchezaji huyo lakini Bw.Blatter anasema ikiwa shirika hilo litawasilisha malalamiko yao kwetu basi mchezaji huyo atawekewa vikwazo wakati wa Olimpiki.

Hata hivyo klabu ya Spurs inaweza kujitetea kwa kusema kua mchezaji huyo Bale alipata nafuu katika siku chache zilizopita, na hivyuo kutetea uwamuzi wa mchezaji huyo kujiondoa kwenye kikosi cha Blatter cha GB.

Bale alicheza kwa mda wa dakika 74 za mechi hio dhidi ya Galaxy, na baadaye Villas-Boas akasema kua "Gareth bado ni kijana na ana nguvu za kupindukia kwa hiyo aliweza kuongeza juhudi zake.

26 JUL.Tafakuri kuhusu Simba ndani ya wiki 2



SIMBA SC juzi imetolewa katika Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kufungwa na Azam FC mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika Robo Fainali ya mwisho.

Mbaya wa Simba jana alikuwa John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga mabao yote matatu, wakati bao la kufutia machozi la Simba lilifungwa na Shomary Kapombe.

Japokuwa Bocco aliondoka na mpira jana, lakini nyota wa mchezo alikuwa Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr’, ambaye alitawala sehemu ya kiungo na kuiongoza vema timu yake hata ikapata ushindi huo mnono.

Maneno mengi yameibuka baada ya matokeo hayo, jambo ambalo ni kawaida kwa timu zetu hapa nchini, dosari na kasoro nyingi huzungumzwa baada ya matokeo mabaya. Leo ndio wanasema timu mbovu na hata kocha Milovan Cirkovick amesema timu yake haikuwa tayari kwa mashindano haya.

Najaribu kujiuliza, Simba imetolewa na Azam, timu ambayo wiki mbili zilizopita ilikutana nayo kwenye fainali ya Kombe la Urafiki na ikashinda kwa penalti 3-1, baada ya sare ya 2-2.

Umefika wakati sasa tuwe watu wa kujadili zaidi hali halisi, kufanya tathmini ya kina ili kubaini makosa yetu, badala ya kupenda kuzungumza kwa chuki, jazba na mazoea. Nimewasikia wachambuzi fulani wa radio moja nchini wanazungumzia Simba- kwanza huwezi kujua pointi yao ni ipi. Mara kukosekana kwa Emanuel Okwi kumepunguza makali ya Simba, ndiyo manaa hata Felix Sunzu amekuwa hatishi sasa.

Jamani, hilo ni tatizo lililofanya Simba ipoteze mechi ya jana? Watanzania tunapenda kukurupuka tunapotaka kusajili wachezaji bila kufuatilia rekodi zao na ndiyo maana kuna wakati tunaingia mkenge kwa magarasa.

Sunzu katika mashindano haya ameonyesha hayuko sawa- amekosa mabao ya wazi yasiyopungua 10. Sasa kwa nini uwadanganye wana Simba kukosekana kwa Okwi kunamfanya hata Sunzu awe butu, wakati anapata nafasi akiwa yeye na kipa anamdakisha, anapiga nje, anaanguka, au mpira unamgonga unaondoka.

Mimi nawaambia wachambuzi wa kibongo, wakumbuke mashindano haya hata kwa ambao hawaendi mpirani, wanapata fursa ya kuona kupitia Super Sport na Star TV- wamekuwa wakimuona Sunzu akipokea pasi za mwisho kama alizokuwa akipewa na marehemu Patrick Mafisango, akipigiwa krosi kama ambazo alikuwa akipigiwa na Okwi, lakini anaishia ‘kumbwelambwela’.

Lakini Sunzu tangu atue Simba, lini alikuwa mkali hata akawanyima watu usingizi? Aliwafunga Yanga kwa penalti kwenye mechi ya Ngao mwaka jana na kwenye Ligi Kuu, kiungo Mafisango alikuwa mfungaji bora wa timu kwa mabao 10, sikumbuki yeye kama alifikisha hata matano.

Huyu ni mchezaji anayelipwa dola za Kimarekani 3,500, takriban Sh.Milioni 5 kwa mwezi Simba SC na huwezi kupata jibu kwa nini anamzidi maslahi Shomary Kapombe. Simba ilimsajili Sunzu baada ya kutupiwa virago El Hilal kwa sababu alikuwa hafungi mabao.

Simba ilimsajili Sunzu kwa kukumbuka alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Challenge, au watuambie walimfuatilia wapi maendeleo yake baada ya hapo, ikiwa klabu aliyokuwa anaitumikia iliamua kuachana naye kwa sababu hafungi na sasa tushangae nini hafungi Simba?

Kuisaidia Simba ni kuzama ndani na kuangalia matatizo ya msingi ya timu, kwa sababu huwezi kuwaambia watu eti Simba leo mbovu, wakati wiki mbili zilizopita wachambuzi hao hao waliisifia Simba inatisha na Juma Kaseja ni kipa bora na wakaitabiria kufanya vizuri kwenye Kagame.
Sasa nataka nieleze matatizo ya msingi ya Simba yaliyowagharimu leo.


BEKI YA KUSHOTO;

Simba ilifanya kosa kumuacha Juma Jabu bila kusajili beki mwingine mbadala hodari wa kushoto, kwani Paul Ngalema aliyesajiliwa badala yake hajamvutia kocha Milovan na ndiyo maana jana akampanga Shomary Kapombe beki ya kushoto.

Ikumbukwe Amir Maftah aliumia kidole baada ya mechi na AS Vita na ikaelezwa hatacheza tena mashindano haya.

Kapombe asili yake ni kiungo na anaweza kuchezesha timu vizuri akicheza kulia na hata katikati, ila amekuwa akitumiwa kama beki wa kulia na kati na anacheza vizuri tu, lakini upande wa kushoto umemshinda.

Kama utaurejea vizuri mchezo wa jana, mipira mingi Azam walikuwa wanapitishia upande wake.

Kikosi cha Simba kilichoanza fainali Urafiki; Kutoka kulia Kaseja, Obadia, Kiemba, Nyosso, Abdallah Juma na Sunzu. Walioinama kutoka kulia ni Mussa Mudde, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Salim Kinje na Mwinyi Kazimoto.


UPANGAJI MBOVU WA KIKOSI:

Lino Masombo na Juma Nyosso wote ni mabeki wa aina moja na lilikuwa kosa kubwa kuwapanga pamoja na hadi sasa bila shaka tumejiridhisha Simba haina beki wa uhakika wa kati, au kocha anataiwa kuisuka upya safu kwa kutumia wachezaji alionao kikosini ikibidi hata kumrejesha sentahafu Mussa Mudde.

Sina neno Jonas Mkude, alicheza vizuri katika nafasi ya kiungo mkabaji, pasi zake zilikuwa zinafika na mwanzoni alijitajidi na kupunguza makali ya Kipre Michael Ballou hadi alipoumia na kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

Takriban mechi mbili au tatu, Mussa anamdhihirishia Milovan, kwamba hawezi kucheza kama kiungo wa pembeni, lakini anandelea kumlazimisha na hapo ndipo unapoweza kujiuliza viungo wa pembeni akina Kiggi Makassy, Salim Kinje, Uhuru Suleiman na hata Christopher Edward walisajiliwa wa nini?

Sunzu, tangu mashindano yanaanza amekuwa akiboronga na bado ameendelea kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na Danny Mrwanda yupo tena ni huyu aliyeingia kwenye fainali ya Kombe la Urafiki akaenda kusababisha penalti iliyofungwa na Mwinyi Kazimoto, wakati Simba ikiwa nyuma kwa mabao 2-1.

Kuna vitu vinaendelea ndani ya Simba kiasi kwamba inakuwa vigumu kuamini kama ni matakwa ya kocha, au kuna nguvu za ziada kutoka kwa wajuaji? Tumeona mara kadhaa Haruna Moshi ‘Boban’ huwa mzuri zaidi anapotokea benchi na tumeona cheche za Abdallah Juma, lakini mambo mbona yanaenda kinyume sasa?

Suala si kufungwa, bali ni kiwango duni cha timu- kwa sababu kufungwa hata timu bora kama Barcelona hufungwa na timu za kawaida kama Chelsea, bali inashitua kuona wachezaji ambao hawako vizuri wanalazimishwa kucheza.

Lino Masombo kila mpira anaosha- hadi kuna wakati Boban akamkaripia, jamani Simba hawachezi hivyo, Simba wanamtembeza nyoka chini- soka ya kutungua maembe ina wenyewe hapa na wanafahamika.

Kote nilipoogelea ni katika kutanua mjadala tu, lakini hoja yangu ya leo ni kwamba; wiki mbili zilizopita Simba ilikuwa inatisha, wiki mbili baadaye Simba mbovu, jamani!
SOURCE; BIN ZUBERY

26 JUL. YANGA, AZAM VITANI LEO





MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga na Azam FC, leo zinaweza kuandika tena historia ya timu za Tanzania kukutana kwenye fainali ya michuano hiyo kama ilivyokuwa mwaka jana, lakini hilo likiwezekana tu endapo zitashinda mechi zao ngumu za hatua ya nusu fainali leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwaka jana Yanga ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kuwafunga bao 1-0 wapinzani wao wakubwa katika soka la Tanzania, Simba.

Hali hiyo inaweza kujirudia tena mwaka huu, endapo Yanga wataifunga timu ngumu ya APR ya Rwanda katika nusu fainali ya pili, baada ya ile ya kwanza itakayoikutanisha Azam na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kufikia hatua hiyo, mabingwa watetezi Yanga, waliwatoa wenzao wa Zanzibar timu ya Mafunzo kwa mikwaju ya penalti 5-3 katika robo fainali iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya dakika 90.

Azam, ikicheza kwa mara ya kwanza Kombe la Kagame, ilisonga mbele baada kuitia aibu ya kipigo cha mabao 3-1, mabingwa wa mara sita michuano hiyo, Simba katika mchezo uliochezwa Jumanne wiki hii.

Mechi zote zinatarajia kuwa ngumu kutokana na hatua iliyofikiwa, lakini bila shaka taswira ya ushindani itakayoliteka jiji la Dar es Salaam, itakuwa mchezo wa Yanga na APR.

Ushindani huo unategemewa katika dhana mbili, kwanza ubora wa timu hizo zinazoundwa na wachezaji wenye viwango vinavyolingana, na pili ni kisasi cha mchezo wa kwanza hatua ya makundi, ambapo Jangwani walitikisha kamba za APR mara mbili bila majibu.

Kiufundi, Yanga italazimika kubadili mbinu ilizozitumia katika mechi yao ya kwanza dhidi ya APR ambayo haitakuwa tayari kuruhusu kipigo cha pili mfululizo ndani ya siku tatu.

Mabingwa Yanga, itawategemea washambuliaji wake Saidi Bahanuzi na Hamis Kiiza katika kuzivuruga kamba za APR, ambao nao watakuwa na Leonel Preus na Seleman Ndikumana kuiandama ngome ya Yanga.

Pia ushindani mkubwa unatarajiwa kuwepo katika idara ya kiungo, ambako Haruna Niyonzima na Athuman Iddi wanakuwa wakionyesha manjonjo yao kama ilivyo kwa Jean Claude Iranzi na Jean Claude Mugiraneza wanaosubiriwa kung'aa kwa upande wa Wanyarwanda .

Hakuna shaka, beki kisiki Mbuyu Twite ataongoza jopo la ulinzi wa APR akisaidiwa na Jonson Bagoole kama itakavyokuwa kwa Nabir Haroub atatengeneza ngtome ya Yanga akisaidiana na Kelvin Yondan.

Kwa upande wa Azam ambayo haijapoteza mchezo kwenye michuano hii, itashuka dimbani ikiwa maazimio ya kutaka kuweka rekodi ya kushiriki mara kwanza na kutwaa taji.

Aina ya soka lao lenye pasi nyingi linaloshabihiana na wapinzani wao AS Vital, pamoja na kujivunia wachezaji waliokaa pamoja kwa muda mrefu kunaufanya mchezo wa leo kuwa mgumu.

Wednesday, July 25, 2012

25 JUL. LEO NI SIKU YA KUZALIWA YA MDAU WA BLOG HII JAMILAAH HASSAN


BLOG HII INAPENDA KUMPONGEZA SANA BI JAMILAH KWA KUFIKISHA MIAKA 30. INA MUOMBEA AISHI MAISHA MAREFU NA ASIACHE KUTEKELEZA IBADA, AEPUKE ANASA ZA DUNIA

25 JUL. BREAKING NEWZ; JAHAZI LILILOKUWA LIKITOKEA TANGA, KWENDA UNGUJA YAZAMA

HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUNA JAHAZI AMBAYO ILIKUWA INATOKEA TANGA KWENDA UNGUJA IMEZAMA, JAHAZI HIYO INASEMEKANA ILIKUWA NA ABIRIA ILA BADO HATUJAJUA KUWA ILIKUWA NA ABIRIA WANGAPI.

JAHAZI HIYO INASEMEKANA IMEZAMA MAENEO YA MKOKOTONI.JUHUDI ZA KUWAOKOA ABIRIA ZINAENDELEA.

KWA TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWAJUZA BAADAE KIDOGO,HAPA HAPA HAPA NDIO KILA KITU BOG

25 JUL. DENTI IFM ATEKWA, AFARIKI




MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
“Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

“Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.

“Walipokwenda kuangalia wakakuta ni mtu akiwa hoi hajitambui. Baada ya kupelekwa hospitali siku ya pili alikuja mama mdogo wa marehemu Agnes aitwaye Veronica Galus na akaleta taarifa kuwa binti yao huyo amefariki dunia. Polisi tunaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika,” alisema Kenyela. Hata hivyo, kifo hicho kimeacha maswali mengi kuwa binti huyo alilishwa nini na nani?

Mzazi wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Bernad King’unza mkazi wa Kimara Dar, hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa safarini Iringa kwenye mazishi ya mpendwa wao huyo yaliyofanyika nyumbani kwao Kalenga, Iringa Julai 19, mwaka huu.

SOURCE; global publisherz

25 JUL.Simba yamkatia rufaa Yondani kwa Tibaigana


UONGOZI wa Simba umesema licha ya uamuzi wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kuamua Kelvin Yondani (pichani) aichezee Yanga katika michuano ya Kagame, kwa upande wao tayari wameshakata rufaa katika Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na kamishna mstaafu wa polisi, Alfred Tibaigana.
Yondani amesaini mkataba wa kuichezea Yanga, lakini Simba imekuwa ikidai kuwa mchezaji huyo ni halali kwao kwani kabla hajajiunga na Yanga alikuwa na mkataba wao, ila ulikuwa na tatizo la uchapaji badala ya kuonyesha unaanza Desemba 2011 ulionyesha unaanza Desemba 2012.

Akizungumza na Championi Jumatano juzi, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Alex Mgongolwa, kuamua Yondani aichezee Yanga katika michuano ya Kagame imekuja wakati wao tayari wakiwa wameshakata rufaa katika kamati ya Tibaigana, hivyo wanasubiri uamuzi wa kamati hiyo ambayo ni ya juu zaidi.

“Sisi tayari tumeshakata rufaa katika kamati ya nidhamu chini ya Alfred Tibaigana na sasa tunasubiri uamuzi wa mwisho ili tuweze kuona hatima ya mchezaji huyo.
“Uamuzi wa Mgongolwa ulikuja huku tukiwa tayari tumeshakata rufaa katika kamati ya Tibaigana, hivyo tunaamini tutashinda kwani Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni ndogo zaidi ya kamati ya Tibaigana,” alisema Kamwaga.

Alisema wanaamini kila kitu kitakwenda sawa juu ya mchezaji huyo kwa kuwa mkataba walionao ni halali.
SOURCE; GLOBAL PUBLISHERZ

25 JUL. REKODI ZA JOHN BOKO


John Bocco ana rekodi ya Ajabu, Amecheza na Simba mara 15 na kufunga magoli 14, Amecheza na Yanga mara 13 na kufunga magoli 9. Jumla amezifunga Simba na Yanga magoli 23 katika mechi 28... Juma Kaseja ndo kipa aliyefungwa magoli mengi zaidi na Bocco 14 wakati Bero kafungwa mara 5. Dah... Kuna watu wanamponda eti hajui kufunga... Sitaki kubishana na mtu na sitaki unazi... Hakuna Number9 wa kiwango cha JB19 Afrika Mashariki

25 JUL.Kada CCM jela miaka 18 kwa wizi wa EPA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka 18 jela Kada wa CCM, Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein katika kesi ya tuhuma za kuchota Sh2.2 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mahakimu wawili katika jopo la waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo waliwatia hatiani watuhumiwa kwa makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo hilo, Jaji Fatuma Masengi aliwaachia huru washtakiwa hao kwa maelezo kwamba upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka yote saba yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo, hukumu hiyo haikuweza kuwaokoa watuhumiwa na hasa Farijala na Maranda watatumikia adhabu yao kwa miaka mitatu jela kwa kuwa adhabu zote walizopewa zitakwenda kwa wakati mmoja.

Tayari Maranda na Farijala wanatumikia kifungo kingine cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za EPA, ambapo walihukumiwa na mahakama hiyo Mei 23, 2011.

Jopo lagawanyika
Jopo la mahakimu watatu lililokuwa likisoma hukumu hiyo liligawanyika na kusoma hukumu mbili tofauti, ambapo hukumu moja iliyoandaliwa na kusomwa na kiongozi wa jopo hilo, Jaji Masengi aliyewaachia huru washtakiwa.

Hata hivyo, katika hukumu ya pili, iliyoandaliwa na Hakimu Projestus Kahyoza na mwenzake Catherine Revocate iliwatia hatiani washtakiwa katika makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili, na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa.

Hata hivyo, wakati wakisoma hukumu hiyo, mahakimu hao walisema badala ya washtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 18, hukumu yao itaenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Kabla ya hukumu
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, hakimu Kahyoza na mwenzake walipitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwamo mtaalamu wa maandishi, Joseph Mgendi ambaye aliweza kuangalia saini katika nyaraka halisi na zinazodaiwa kughushiwa, ikiwamo hati ya usajili ambapo alibainisha kuwa zilikuwa zimeghushiwa.

Pia walipitia utetezi uliotolewa wa mshtakiwa Maranda, ambaye aliyakana mashtaka yote saba yanayowakabili na kwamba, alikataa katakata kuwa hakuwahi kula njama na kughushi hati ya usajili wa Kampuni ya Money Planners & Consultant.

Hakimu Kahyoza alisema, Maranda alidai kuwa yeye hakuwahi kwenda Brela kusajili kampuni hiyo na kwamba, aliyewahi kwenda kusajili kampuni ni binamu yake, Farijala.

Hakimu Kahyoza alisema, Maranda katika utetezi wake alisema yeye hakuwahi kughushi hati yoyote hivyo, haikuwa rahisi kwake kutoa hati iliyoghushiwa pia, hakuwahi kuiba fedha BoT na wala hakuwahi kujipatia fedha yoyote kwa njia ya udanganyifu.

Kahyoza alifafanua kwamba, Maranda alidai mfumo uliotumika kuwaingizia fedha kwenye akaunti yao iliyopo katika Benki ya CBA uliendeshwa kihalali ndiyo maana, BoT hawakuwahi kulalamika hivyo, aliiomba mahakama imuone hana hatia.

Akisoma utetezi uliotelewa na Farijala, Hakimu Kahyoza alisema, Farijala naye alikataa madai ya kughushi, kuwasilisha nyaraka bandia benki, kuiba fedha yoyote na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na aliiomba mahakama imwachie huru kwa sababu hana hatia.

Yasiyo na utata
Hakimu Kahyoza alisema kuwa mahakama ilibaini kuwapo kwa masuala yasiyokuwa na utata ambayo ni pamoja na kwamba Maranda na Farijala ni ndugu, waliwahi kufanya biashara pamoja na waliingiziwa fedha kwenye akaunti namba 0101379004 ya United Bank of Africa ambazo ni kiasi cha Sh2.2 bilioni.

“Baada ya kuweka msingi huo, mahakama ilijiuliza je, washtakiwa walikula njama ya kuiibia BoT, walighushi hati ya usajili wa kampuni namba 150731, walighushi hati ya mkataba kati ya Kampuni ya Money Planners & Consultant na Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani, waliwasilisha nyaraka za kughushi benki, waliibia BoT na kwamba je, walijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,” alihoji Kahyoza.

Hakimu huyo alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, hakuna utata kuwa hakuna mahali panapoonyesha washtakiwa ndiyo walikuwa wamiliki wa kwanza wa kampuni hiyo Money Planners & Consultant na kwamba majina yanayodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni hiyo ya Thobias Kitunga na Paulo ni majina ya uongo na ya kufikirika.

Alisema licha ya majina hayo kuwa ya kufikirika, mabadiliko ya kampuni hiyo ya Money Planners & Consultant hayakuwahi kufanyika na hata Brela hakuna kumbukumbu, hivyo saini zilizopo katika nyaraka za kampuni hiyo ikiwamo hati ya usajili ni za kughushi.

Alisema sababu ya kuthibitisha hilo ni kwamba, ofisi ni ileile iliyopo Magomeni Mapipa, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 hata baada ya mabadiliko.

“Hati hizo za usajili hazikusainiwa na Msajili wa Biashara toka Brela, Noel Shani bali zilisainiwa na washtakiwa wenyewe. Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 333 na 335 (c) (e) vimetufanya tufikie hitimisho kuwa washtakiwa walighushi nyaraka hizo,” alisema Hakimu Kahyoza.

Alisema Maranda na Farijala walighushi hati ya mkataba ya Septemba 8, 2005, wakitumia majina ya Thobiasi na Paul na kwamba hati hiyo haikusainiwa na Kampuni ya Money Planners & Consultant.

“Maombi ya kupewa fedha hizo Sh 2.2 bilioni, yalipitiwa na watu kadhaa wakiwamo Mwanasheria wa BoT na kupeleka kibali cha mwisho kwa Gavana aidhinishe malipo, hakuna hata mmoja aliyebaini kuwa katika hati ya mkataba kati ya Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani na Kampuni ya Money Planners & Consultant, haikuwa na saini ya Kampuni ya Money Planners & Consultant,” alisema.

Aliongeza: “Kwa sababu hiyo inaonyesha wazi, washtakiwa ndiyo walighushi nyaraka hizo hivyo hati ya usajili wa kampuni hiyo, hati ya mkataba ni za kughushi.”

“Tuna haki ya kuamini kuwa washtakiwa kwa kujua, walifanya hivyo kwa nia mbaya ya kuwasilisha hati hizo za kughushi CBA na baadaye BoT”, alisema Kahyozi.

Alisema hakuna ubishi kuwa hakuwapo hata shahidi mmoja aliyewahi kuthibitisha kuwa washtakiwa hao waliwahi kuiibia BoT Sh 660,210,000.

“Katika hili hatupo tayari kukubaliana na upande wa mashtaka kwa sababu halijathibitika”.

Aliongeza kwamba, hakuna utata kuwa BoT iliweka kwenye akaunti ya washtakiwa zaidi ya Sh2.2 bilioni na kwamba, kiwango hicho cha fedha kiliwekwa baada ya washtakiwa kuwasilisha hati za kughushi katika benki hiyo kuu ikiwamo hati ya usajili na hati ya mkataba.

Hakimu alisema kulikuwapo na maofisa wa juu BoT waliotakiwa walithibitishe hilo, lakini, Mwanasheria wa BoT yeye alikuwa anathibitisha uhalali wa hati hiyo ya mkataba ambayo haikusainiwa upande mmoja na Kampuni ya Money Planners kuwa, “Ina nguvu kisheria hivyo, inaweza kutumiwa na BoT kuhamisha au kuchukua fedha zinazoongelewa katika maombi ya washtakiwa”.

Alifafanua hakimu, “Mwanasheria alimaanisha kuna watu wengine walithibitisha, sisi kwa mtazamo wetu ni ajabu kwa maofisa hao hata mmoja hakuwahi kuona katika hati ya mkataba hakuna saini ya Kampuni ya Money Planners.

Tunajiuliza walimezwa katika huu mtego au walipumbazwa? Kama walipumbazwa, upumbazo huo ulikuwa ni wa hali ya juu na kujikuta wote wanaingia kwenye mtego huu.” alisema Hakimu Kahyoza.

Aliongeza kwamba washtakiwa hao walifanya matendo hayo yote kwa nia mbaya na kuwafanya watu wengine, wawe sehemu ya kughushi.

Kuhusu shtaka la kula njama, kwa ujumla maelezo yote yanaonyesha Maranda na Farijala, walikubaliana makazi ya ofisi yawe Magomeni, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 ambako ni nyumbani kwao, waliwasiliana, walikutana, walijadiliana hivyo walitenda kosa la kula njama.

“Sisi hatuna sababu za kusitasita kuwa kweli washtakiwa walikula njama dhidi ya BoT. Ni kweli walikula njama,” alisisitiza Kahyoza.

Jaji Masengi
Kwa upande wake, Jaji Masengi aliwaachia huru washtakiwa wote kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuyathibitisha mashtaka yote saba yanayowakabili.

Jaji Masengi alisema BoT ndiyo wangekuwa walalamikaji wakuu, lakini haikuwahi kulalamika kutoa fedha hizo zinazodaiwa kuibwa na washtakiwa wala Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani.

Kuhusu kughushi, alisema ushahidi uliotolewa haukutosheleza kuthibitisha kosa hilo na kwamba licha ya utetezi kuwa na upungufu lakini hakukuwa na sababu za kuwatia hatiani.

Kabla ya hukumu
Kabla ya kusomwa kwa hukumu ya Hakimu Khayoza na Hakimu Catherine, Wakili wa Serikali, Alapha Msafiri aliiambia mahakama kuwa washtakiwa siyo wakosaji wa mara ya kwanza, wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela katika kesi namba 1161 ya mwaka 2008.

Msafiri aliiomba mahakama itumie kifungu cha 348 na 358 cha Makosa ya Jinai (CPA), kutoa amri Maranda na Farijala walipe fidia au warejeshe kiasi walichojipatia kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Majura Magafu, anayewatetea Maranda na Farijala, alidai kuwa ni kweli washtakiwa walitiwa hatiani lakini, isiwe kigezo cha kuwapa adhabu kali kwa sababu kesi namba 1163 na 1161 zilifunguliwa siku moja, zinahusu makosa ya aina moja isipokuwa zilipangiwa jopo tofauti.

“Hii ni tofauti na mtu aliyetenda kosa akaachiwa halafu akafanya tena kosa lingine, pia mazingira ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa yalikuwa na utata kwa namna moja au nyingine na kwamba washtakiwa walitenda makosa bila ya kujua kama wanatenda makosa,” aliwatetea wakili huyo na kuongeza:

“Kwa hiyo ni dhahiri, matukio hayo hayakufanyika kwa makusudi kwa asilimia 100, kwa kuwa wao waliamini ni halali lakini baadaye ilibainika kuwa si halai”.

“Waheshimiwa washtakiwa wote wana matatizo ya kiafya, Farijala ana matatizo ya presha ya macho na Maranda ana tatizo la Figo, naomba kama mahakama itaridhia chini ya kifungu cha 38, ina mamlaka ya kuangalia mazingira ya utendwaji wa matukio, hali za watuhumiwa na kuwaachia kwa masharti maalumu kutokana na afya zao,”alisema Magafu.

Pia aliiomba mahakama itamke wazi wazi kuwa adhabu watakayopewa washtakiwa kama itakuwa ni ya kifungo, inastahili kuanza lini kwa sababu kumekuwapo na utata wa sheria, kuwa ni lazima wamalize kifungo cha awali ndiyo waanze kingine.

Kwa upande wa Hakimu Catherine Revocate, alisema wamejadiliana kwa kuangalia mazingira ya kesi, afya za washtakiwa na kwamba ni wakosaji wa mara ya kwanza kwa sababu kesi hiyo inasimama peke yake, katika shtaka la kwanza hadi la saba kasoro shtaka la sita waliloachiwa huru; washtakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kila kosa.

Pia alifafanua kuwa badala ya washtakiwa hao kutumikia kifungo cha miaka 18 katika mashtaka sita yanayowakabili, kifungo hicho kitakwenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela

source;gazeti la mwananchi