tuwasiliane

Thursday, July 26, 2012

26 JUL. AZAM NA YANGA ZATINGA FAINALI KAGAME CUP



Azam na Yanga watachuana katika mchezo wa fainali wa kombe la Kagame baada ya leo kufanikiwa kuwafunga AS Vita ya DR Congo na APR ya Rwanda katika michezo ya nusu fainali.

Azam walikuwa wa mwanzo kuting fainali baada ya kuwachapa AS Vita goli 2-1. Magoli ya Azam yamefungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 88 na John Raphael Bocco dakika 68.

Goli la AS Vita walio maliza mchezo wakiwa pungufu, baada ya beki yao kuzawadiwa kadi nyekundi katika dakika ya 40, lilifungwa katika dakika 33 kupitia kwa Afrey.

Yanga ilibidi wangoje dakika 30 zanyongeza kuiondosha APR, baada ya dakika 90 kumalizika bila nyavu kutingishwa, huku kukiwa na kosa kosa kibao.

Goli pekee katika mchezo huo wapili wa nusu fainali lilifungwa katika dakika ya 100 kupitia kwa Hamisi Kiiza na katika dakika ya 104 Godfrey Taita alizawadiwa kadi nyekundu.


Mchezo wa fainali kati ya Azam FC na Yanga itachezwa jumamosi (julai 28) uwanja wa Taifa, ukitanguliwa na wa mshindi wa 3 kati ya APR na AS Vita saa 8 mchana.

No comments:

Post a Comment