tuwasiliane

Thursday, July 26, 2012

26 JUL.SIMBA, YANGA, AZAM ZATENGEWA MWALI MWINGINE



TIMU nane toka Tanzania Bara na Visiwani zinatarjiwa kushiriki katika michuano maalum inayokwenda kwa jinala ‘Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012’ inayotarajiwa kutimua vumbi Augusti 4 hadi 18.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema leo kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzipa makali timu shiriki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Alisema michuano hiyo itakayohusisha timu tatu bora kutoka Tanzania Bara, timu tatu bora kutoka Visiwani na timu moja iliyopanda katika pande hizio, itachezwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema timu hizo zitakuwa katika makundi mawili na hakutakuwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu zaidi ya kuwepo kwa zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa tu na tayari wameshaziandikia barua za kuzitaarifu kuhusiana na michuano hiyo.

“Nadhani hii ni nafasi nyingine kwa timu kuonyesha ushindani katika michuano hii, pia pamoja na kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi, makocha wa timu shiriki wataweza kujua kiwango kilichopo kwenye timu zao na kama kuna kasoro warekebishe kabla ya kuanza kwa ligi,”alisema.

Banc ABC ambayo imedhamini michuano hiyo kwa miaka mitatu, kupitia kwa mkurugenzi wake Mkuu Boni Nyoni alisema wameamua kuandaa michuano hiyo ili kuunga mkono jitihada za maendeleo ya soka hapa nchini.

No comments:

Post a Comment