tuwasiliane

Tuesday, January 31, 2012

31 JAN. 30 wanusurika kuzama Ziwa Victoria

ZAIDI ya watu 30 wakiwepo watoto wadogo wanne wamenusurika kuzama katika Ziwa Victoria baada boti mbili kugongana eneo la Mwikoko karibu na jengo la maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri, ambapo boti ya uvuvi yenye namba za usajili RMU 5234 iligongana na boti ya abiria iliyojulikana kwa jina la mv Nyanganira inayomilikiwa na Ramadhan Nyanganira.

'RIPOTA WA BLOGU HII alifika eneo la ajali na kushuhudia boti hizo zikiwa zimeharibika huku kukiwa na madai ya watu kutoonekana baada ya baadhi yao kuokolewa. Baadhi ya mashuhuda na abiria walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa boti hizo na kutozingatia sheria za unahodha.

“Kabla ya ajali kutokea kama meta mia moja hivi, abiria walimuambia nahodha aangalie mbele boti iliyokuwa ikija, lakini alishindwa kumiliki vyema boti hiyo na alipokata kona tu boti ya uvuvi iligonga katikati,” alisema mmiliki wa boti hiyo, Nyanganira na kuongeza:

"Hatuwezi kusema kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha, ukweli utapatikana baada ya siku moja au mbili”. Abiria wa boti hilo aliyejitambulisha kwa jina la Eunice Maagi, mkazi wa Kiabakari aliyedai alikuwa akitoka kwenye msiba katika kijiji cha Kibuyi wilayani Rorya, alisema kuwa hadi alipookolewa na kupata fahamu vizuri, hakuna mtu yeyote aliyelalamika kama ndugu, jamaa au rafiki yake haonekani.

“Hakuna niliyemsikia analalamika kuwa amepotelewa na mtu sijui kwa kuwa bado
tumechanganyikiwa na pia kutojuana kutokana na kila mtu kuwa na safari yake, lakini sisi tulikuwa kama sita na wote tumeokolewa na tupo salama,” alisema Maagi.

31 JAN.AZAM YAZISOGELEA SIMBA NA YANGA


AZAM FC jana ilitumia vizuri uwanja wa nyumbani Chamazi kuendeleza mbio za kuzifukuza Simba na Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, baada ya kuifunga Moro United bao 1-0, shukrani kwa mshambuliaji John Bocco aliyefunga bao peke katika mchezo huo.

Kwa ushindi huo, Azam--mabingwa wa Kombe la Mapinduzi wamefikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 14, ikiwa nyuma kwa pointi mbili tu dhidi ya vigogo Simba na Yanga.

Katika mchezo huo, Azam wangeweza kuibuka na ushindi mnono kama washambuliaji wake wake wangetumia nafasi nyingi za kufunga walizopata hasa katika kipindi cha kwanza.

Bocco alifunga bao hilo katika dakika ya 11 kwa shuti kali baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Moro United kufuatia ushirikiano mzuri na mshambuliaji mwenzake, Kipre tchche.

Azam wangeweza kufanya matokeo kuwa 2-0 mpaka dakika ya 25 kama siyo Kipre kupoteza nafasi nzuri ya kufunga, huku pia shuti lake la dakika ya 40 likigonga mwamba wa goli.

Shambulizi kubwa walilofanya Moro United kipindi cha kwanza, lilikuwa katika dakika ya 25 baada ya Kalvin Chale kupiga mpira wa adhabu ndogo uliotemwa na kipa wa Azam Mwadin Ally.

Kipindi cha pili, Moro United walioneka kucheza kwa kuelewana na nusura Geofrey Wambura afunge bao katika dakika ya 52 lakini akaishia kupaisha mpira juu pasi ya Fred Mbuna.

Winga Mrisho Ngassa alikosa bao la wazi katika dakika ya 68, baada ya kutereza ndani ya eneo la hatari wakati akijiandaa kupiga mpira kufuatia kuwatoka mabeki wa Moro United.

Kocha wa Moro United, Hassan Banyai alisema ameridhika na kipigo hicho, lakini alimtupia lawama mwamuzi aliyechezesha pambano hilo kwa madai ya kutokuwa makini kufuatilia sheria za za mchezo wa soka.
Banyai amesema ameridhishwa na kiwango walichoonyesha vijana wake na sasa anajipanga kwa ajili ya mechi ijayo.

Hall Stewart, kocha wa Azam alisema amefurahishwa na matokeo hayo kwani muhimu ni pointi tatu ambazo vijana wake wamezipata. Hata hivyo, alisema baada ya bao la kwanza wachezaji wake walijisahau na kuwafanya Moro United kurejea kwenye mchezo tofauti na kipindi cha kwanza.

31 JAN. Sudan yaingia robo fainali


Sudan ilipata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya miaka 42, ilipofanikiwa Jumatatu kuishinda Burkina Faso magoli 2-1 katika uwanja wa Bata na kufuzu kuingia robo fainali.

Sudan imekuwa miongoni mwa mataifa manane yatakayoshindana katika robo fainali, hasa kutokana na Ivory Coast kuishinda Angola magoli 2-0, katika mechi nyingine ya kundi B mjini Malabo.

Mshambulizi wa Sudan Mudather El Taib alifunga bao katika kipindi cha kwanza na vile vile katika kipindi cha pili, na kuiwezesha Sudan, mabingwa wa mwaka 1970, kuendelea kuwa na matumaini ya kupata ubingwa tena mwaka huu.

Bao la Burkina lilitiwa wavuni na Issiaka Ouedraogo.

Sudan sasa itakutana na Chipolopolo ya Zambia katika pambano la robo fainali, Jumamosi tarehe 4 Februari, katika uwanja wa Bata, nayo Ivory Coast itacheza na Equatorial Guinea.

Wachezaji wa Sudan, baada ya kushindwa na Ivory Coast 1-0 katika mechi yao ya kwanza, waliweza kujikakamua na angalau kupata pointi yao ya kwanza tangu mwaka 1976, walipotoka sare na Angola siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Kufuatia Angola kushindwa kwa mara ya kwanza katika mashindano ya mwaka huu, timu hiyo sasa imezikosa robo fainali, baada ya ushindi wa Sudan.

Angola ilijisahau katika kulinda ngome yake, na Emmanuel Eboue aliitumia nafasi hiyo kwa kumshambulia kipa akiwa karibu sana, na baadaye Wilfried Bony akautumbikiza mpira wavuni katika lango ambalo lilikuwa wazi kabisa.

Mechi za mwisho za kundi C zinachezwa Jumanne, wakati Gabon itakapocheza na Tunisia, na wengi wakisubiri kujua ni nani ataongoza katika kundi hilo, baada ya mechi hiyo ya Franceville.

Na mjini Libreville, Morocco na Niger watakutana, na kila nchi bila shaka itafanya juhudi kubwa kujipatia pointi zake za kwanza katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Africa.

Monday, January 30, 2012

30 JAN. SHIBOLI APELEKA MSIBA MANUNGU, AITUNGUA MTIBWA SUGAR.


Timu ya wakata miwa wa Manungu Turiani – Mtibwa Sugar wamendelea kufanya vibaya katika hatua ya pili ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kuchapwa na Coastal Union ya Tanga.


Mtibwa Sugar wamepoteza mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Manungu ukiwa ni mchezo wa pili kwa Mtibwa Sugar kupoteza katika uwanja huo wa Manungu.

Goli hilo la Coastal Union lilifungwa na Mshambuliaji wa Simba aliyopo Coastal kwa mkopo akitokea Kagera Sugar Ahmed Shiboli.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (14) 31
2. Yanga (15) 31
3. JKT Oljoro (14) 26
4. Azam FC (14) 26
5. Mtibwa Sugar (15) 22
6. Kagera Sugar (15) 20
7. JKT Ruvu (15) 17
8. Ruvu Shooting (15) 17
9. Moro United (14) 15
10. African Lyon (14) 14
11. Coastal Union (15) 14
12. Toto Africa (15) 13
13. Polisi Dodoma (14) 12
14. Villa Squad
(15) 10
SOURCE SHAFFIHDAUDA.COM

30 JAN. Zambia yaingia robo fainali


Zambia ilijitengea nafasi katika robo fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuwashinda wenyeji Equatorial Guinea bao 1-0 katika mechi ya kundi A, na kuongoza kundi hilo, ikiwa na pointi 7.

Nahodha Chris Katongo aliifungia Zambia bao hilo katika dakika ya 67.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Zambia huenda wakaepuka kucheza na Ivory Coast katika robo fainali, nchi ambayo inatazamiwa kuongoza kundi B.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Equatorial Guinea kushindwa, na ambao wanashirikiana na Gabon kama wenyeji wa mashindano hayo.

Ilikuwa pia ni mara ya kwanza kwa kocha mpya Gilson Paulo akiitizama timu yake ikifungwa.

Equatorial Guinea imo katika nafasi ya pili katika kundi A, ikiwa na pointi 6, Libya ina nne, na Senegal ni ya mwisho ikiwa haina pointi zozote.

Wenyeji Equatorial Guinea tayari walikuwa wamefuzu, na Zambia walihitaji tu kuondoka sare kuingia robo fainali.

Ushindi wa Chipolopolo unamaanisha kwamba sasa watasafiri kuelekea hadi uwanja wa Bata, katika kujiandaa kwa mechi yao ya robo fainali siku ya Jumamosi, tarehe 4 Februari.

Kinyume na Senegal ambao wanarudi nyumbani bila hata pointi moja, Libya inaondoka mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 katika mechi yake ya Jumapili dhidi ya Senegal.

Ihab Albusaifi alifunga katika kipindi cha kwanza, na vile vile katika kipindi cha pili.

Deme Ndiaye aliifungia Senegal, na kinyume cha matazamio ya wengi, timu hiyo sasa inarudi nyumbani baada ya kushindwa katika mechi tatu.

Hata hivyo bado ni fahari kwa timu ya Libya ya Mediterranean Knights kuondoka mashindano hayo kwa kupata ushindi katika mechi, ikiwa ni ushindi wao wa kwanza tangu mwaka 1982, wakati nchi yao ilikuwa mwenyeji wa mashindano hayo

Huu ni ushindi wao wa kwanza kwa mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika, nje ya nchi yao.

Watajipongeza kwa kufikia hatua hiyo, hasa wakikumbuka kwamba ni hivi majuzi tu nchi yao imeanza kupata kutulia baada ya matatizo mengi.

30 JAN. ARSENAL YAFANYA KWELI


Robin van Persie ilibidia afanye kazi ya ziada Jumapili, na hatimaye akifunga magoli mawili ya penalti, na kuiwezesha Arsenal kuponea chupuchupu kuondolewa katika raundi ya nne ya Kombe la FA, baada ya kupambana na Aston Villa, hatimaye ikishinda 3-2.

Kufikia mwisho wa nusu ya kwanza ya mchezo, Arsenal ikichezea uwanja wa nyumbani wa Imarati, tayari ilikuwa imeachwa nyuma kwa magoli 2-0.

Mabao hayo yalikuwa yamefungwa na Richard Dunne (kwa kichwa) na goli la mkwaju wa kupinda kupitia mchezaji Darren Bent.

Lakini magoli matatu katika muda wa dakika saba yaliubadilisha mchezo kabisa, na Van Persie akibadilisha mambo kwa mkwaju wa penalti, baada ya Dunne kumchezea vibaya Aaron Ramsey.

Theo Walcott alisawazisha kabla ya Van Persie kuandikisha ushindi, kwa kupata bao la pili la penalti, kufuatia Bent kucheza mchezo usio halali dhidi ya Laurent Koscielny.

Arsenal, mabingwa mara 10 wa Kombe la FA, sasa watacheza na mshindi atakayepatikana katika mchezo wa raundi ya nne utakaorudiwa kati ya Middlesbrough na Sunderland.

Sunderland na Middlesbrough walipocheza katika mechi ya awali Jumapili mchezo ulikwisha kwa sare ya 1-1.

The Gunners watacheza mechi hiyo wakifahamu sasa wana uwezo wa hatimaye kuendelea na mashindano hayo, na kuwaletea mashabiki wao kombe ambalo wamelisubiri kwa muda mrefu.

Katika droo ya raundi ya tano, ambayo imefanyika Jumapili, klabu ya daraja ya kwanza, Stevenage, kwa mara ya kwanza katika historia yake imekuwa miongoni mwa timu 16 zilizosalia katika mashindano hayo, na sasa itacheza na Tottenham.

Brighton itasafiri hadi uwanja wa Anfield kucheza na Liverpool, Chelsea nao ni wenyeji wa Birmingham, na Crawley Town, katika daraja ya pili, itacheza na Stoke.

Sunderland ikifuzu baada ya mechi ya marudiano, itapambana na Arsenal.

Norwich itacheza na Leicester, na Everton itaikaribisha Blackpool.

Bolton itacheza aidha na Millwall, au Southampton.

30 JAN.CHEKA AMCHAKAZA NYILAWILA


HATIMAYE ubishi wa nani ni nani katika masumbwi nchini umekamilika jana usiku katika Uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Morogoro baada ya mabondia Francis Cheka ambaye anashikilia mkanda wa mabara, na Karama Nyilawila ambaye wiki iliyopita aliutema mkanda wa ubingwa wa dunia kwa sababu ya pambano hilo, kumalizika kwa Cheka kumtwanga bila huruma mpinzani wake huyo.

Cheka ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu zote na mashabiki lukuki walioongozwa na mwanamuziki Afande Sele, alijikuta gari lake likisukumwa na mashabiki hao hadi nyumbani kwake maeneo ya Kilimahewa, umbali wa takribani kilometa moja toka Uwanja wa Jamhuri.

Kwa mujibu wa matokeo ya majaji wa pambano yaliyosomwa na jaji mkuu wa pambano hilo, Boniphace Wambura, jaji wa kwanza alimpa Cheka pointi (100) Karama (96), jaji wa pili alitoa 99 kwa 97 na wa tatu alitoa 99 kwa 97.

Hata hivyo, mara bada ya pambano hilo lililoshuhudiwa na wasanii mbalimbali nchini akiwemo Joseph Haule 'Profesa Jay' na Selemani Msindo 'Afande Sele', mabondia mashuhuri nchini na Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Aziz Abood, bondia Karama alisema alishindwa kutokana na kuwa na uzito ulio chini ya mpinzani wake.

Karama alisema Cheka ana uzito wa kilo 76.5 na yeye 74.5.

Bondia huyo alivishutumu vyama vya mchezo huo nchini kuwa ndiyo chanzo cha mabondia kushuka viwango kutokana na ubabaishaji mwingi wanaoufanya.

Hii ni mara ya pili kwa wanamasumbwi hao kukutana mjini Morogoro katika uwanja huohuo, ambapo awali mwaka 2009 walitoka sare na kuamsha ubishi wa nani ni nani katika masumbwi hasa ikizingatiwa kuwa wote walikuwa na mikanda yenye hadhi kubwa.

Cheka alipohojiwa na mwandishi wetu alisema hakuna bondia anayeweza kumpiga hapa nchini.

30 JAN. Serikali ya JK presha inashuka presha inapanda


Aliyekuwa Mwenyekiti wa timu ya kampeni ya Rais Kikwete mwaka 2010, Abdurhaman Kinana ni miongoni mwa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaolalamikia mbio za urais zinavyoathiri utendaji wa chama tawala na serikali.

Kwani Mgomo huo wa madaktari, mbio za urais wa mwaka 2015 na kupanda kwa gharama za maisha ni miongoni mwa mambo yanayoutikisa na kutishia mustakabali wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho tayari wameshaanza kulalamikia harakati chafu za kuwania urais zinazolenga kuwaumiza kisiasa wale wanaotajwa kutaka kukiwania kiti hicho.

Huku Rais Kikwete akipambana kukinusuru chama chake na mpasuko uliojitokeza, hali si shwari kwenye serikali yake ambayo inakabiliwa na mdororo wa kiuchumi na kupanda kwa gharama za maisha.

Madaktari nchini wameuongezea machungu utawala wa sasa na wananchi kwa kuamua kugoma, wakiishutumu serikali wa kushindwa kuboresha mazingira yao ya kazi, vifaa, posho, mishahara, nyumba na huduma nyinginezo.

Mgomo huo uliodumu kwa takriban wiki moja sasa, unaelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii kuwa unaiweka serikali katika wakati mgumu wa kutawala.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa serikali inakabiliwa na ukata mkubwa kiasi cha kushindwa kuwalipa wabunge waliokuwa kwenye vikao vya kamati mbalimbali kwa takriban siku tisa sasa.

Msigwa alitoa kauli hiyo jana mjini Kibaha alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ambapo alisema wabunge wanaishi kwa kukopa vyakula na malazi kwenye hoteli walizofikia.

“Serikali yenu imefilisika ndiyo maana inashindwa kutulipa, sasa niambieni mishahara ya walimu, madaktari na polisi wataitoa wapi?” alihoji.

Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (Bavicha), John Heche, alisema serikali imewachoka wananchi wake na rais ameamua kwenda nchini Uswisi kuhudhuria mkutano wa kiuchumi wakati nchini kwake kuna mgomo wa madaktari.

Sunday, January 29, 2012

29 JAN. Twiga yaisambaratisha Namibia





Timu ya Taifa ya Wanawake ya Soka Twiga Stars wamewasambaratisha Namibia kwa jumla ya magoli 7 kwa 2 na sasa wanawangoja kati ya Misri ama Ethiopia ambapo mchezo wa kwanza Misri walishinda goli 4-2.

Katika mchezo wa leo ambapo Twiga Stars wameibuka na ushindi wa goli 5-2 katika uwanja wa Taifa huku wa Namibia wakienda huku wakimkumbuka mshambuliaji alivaa jezi namba 8 Mwanahamisi Omary, kwanamna alivyokuwa wanawaenyesha mabeki wa timu hiyo.

Twiga Stars walianza kuandika goli la kwanza katika dakika ya 22 kupitia kwa Mshambuliaji Hatari na mwenye kasi Mwanahamisi Omar.

Goli hilo halikukaa sana kwani katika dakika ya 30 Albert Dakisi aliisawazishia goli hilo kwa mpira wa kona na yeye kuiunga kwa kichwa na mpira kutinga moja kwa moja nyavuni. Na kupelekea timu kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi Cha pili Mwanahamisi Omari aliyekuwa ana ama kila upande alimpa pasi murua Asha Rashidi katika dakika ya 47, ambapo Asha akufanya ajizi na kuundumbukiza mpira wavuni.

Baada ya goli hilo Namibia walikuja juu huku ukuta wa Twiga ukifanya makosa ya hapa na pale lakini Namibia walishindwa kuyatumia mpaka katika dakika 72, ambapo mpira ulidundishwa chini na mwamunzi ndani ya eneo la hatari ya Twiga stars baada ya Mwanahamisi Omary kuwa chini, wakati Twiga wakitegemea Namibia wangecheza fair play kwa kutoa mpira nnje mambo yalikuwa tofauti, kwani alitoa pasi ya goli huyo mchezaji wa Namibia na kuipatia goli la 2 Namibia.

Mwanahamisi Omari aliendeleza usumbufu wake safari hii akitokea kushoto, upande uliokuwa dhaifu kwa Namibia hii leo, kwa kuwalamba chenga mabeki wa Namibia na Kipa wake lakini mpira wake ulizuiwa na mlinzi na kumkuta Eto'o Mlenzi na kuifungia Twiga goli la 3 katika dakika ya 84.

Goli hilo liliwafanya Twiga kucheza soka safi na dakika ya 88 Asha Rashidi aliipatia Twiga Stars goli la 4 na la 5 likifungwa na Mwanahamisi Omari katika dakika 90 na mchezo kumalizika kwa Twiga kushinda goli 5-2.

Kwa ushindi huo Twiga Stars imeitoa Namibia kwa jumla ya goli 7-2 hivyo wanangoja mshindi kati ya Misri na Ethiopia. Na endapo wakishinda mchezo huo utakao chezwa mei watakuwa wamefuzu kwa mara ya pili mfululizo katika michuano ya 8 ya mataifa ya Africa itakayo fanyika Equaterial Guinea hapo november mwaka huu.

29 JAN.TWIGA STARS VITANI LEO


TIMU ya soka ya Taifa ya wanawake Twiga Stars leo itaumana na wenzake wa Namibia katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Zimbabwe mwishoni mwa mwaka huu.
Twiga inaingia uwanjani ikiwa kifua mbele baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili zilizopita mjini Windhoek.

Akizungumzia mchezo huo wa leo Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili alisema kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri kiafya tayari kuikabili Namibia. Alisema kuwa kupitia Kocha wa timu yao Boniface Mkwasa wameweza kujifunza mbinu mpya za kuwakabili wapinzani wao.

“Katika mchezo wetu wa Namibia wachezaji walishindwa kutumia nafasi nyingi na kujikuta tukikosa mabao mengi lakini mechi ya kesho (leo) tumejipanga vizuri”.

Aliongeza kuwa wamejifunza mbinu za ukabaji na ushambuliaji ambazo watazitumia katika kuikabili timu ya Namibia.

“Ni kwamba kwa sasa tunaona kuwa kesho “ leo” ushindi upo mbele yetu kwa asilimia mia moja kwa kuwa tumeongeza mbinu mbadala za kuishinda timu ya Namibia” alisema. Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Namibia Klaus Staerk alisema kuwa timu yake imekuja Tanzania kupata ushindi na sio kukamilisha ratiba.

Alisema anatambua kuwa Twiga ni timu nzuri na yenye uwezo na ndio maana iliweza kuwafunga nchini kwao (Namibia) na kuongeza kwa sasa wameshagundua mbinu mpya za kukabiliana nao.

Alisema kuwa timu yake inajitahidi kuyazoea mazingira ya hali ya hewa ya hapa nchini ambayo ni ya joto ikilinganishwa na Namibia ambapo kuna baridi. Pia aliongeza kuwa kocha wa timu yao anaumwa tumbo lakini hata hivyo wanatarajia kuwa atapona na kukisimamia vema kikosi chake hicho.

“Tumekuja hapa Tanzania kushinda licha ya kuwa tunaona kuwa changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni hii hali ya hewa kuwa ni joto huku kwetu Namibia tumezoea baridi, lakini hata hivyo tutajitaidi kufanya vema” alisema Stark.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah alisema kuwa TFF itaendelea na kampeni ya kuchangisha fedha za kusaidia timu hiyo.

Alisema kuwa Bohari ya Madawa imewapatia Sh milioni 10 na pia kuna wadau wengine mbalimbali wameahidi kuwasaidia zaidi. Mwisho./fm

29 JAN. Wakulima wafunga barabara ya Kilosa-Dumila


MAMIA ya wakulima kutoka vijiji vya Kata ya Msowero kikiwemo cha Mambegwa katika Tarafa ya Magole, wilayani Kilosa juzi walifunga barabara kuu ya Kilosa – Dumila na kusababisha usumbufu.

Walifunga barabara hiyo kwa saa 12 wakishinikiza uongozi wa Serikali ya wilaya hiyo kutatua mgogoro wa mipaka kati ya Kijiji chao cha Mambegwa na Mabwelebwele .

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego alilazimika kufika eneo la tukio ili kuzungumza na wananchi hao waliokuwa wamejawa na hasira huku wakiwa wameshika mabango.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Wilaya ya Kilosa na Dumila wakiwa na dhana za kutuliza fujo waliwasili eneo la tukio na kuwataka wananchi hao kuondoa mawe makubwa na magogo waliyoziba pande mbili za daraja la Mto Msowero linalotenganisha Kilosa na Dumila.

Pamoja na kukataa huko, polisi walitumia busara ya kutotumia nguvu ya kuwatawanya kwa mabomu na badala yake walimsubiri Mkuu wa Wilaya kama madai ya wananchi hao ili kupata majawabu muafaka.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mambegwa ambao wamekuwa na mgogoro wa mipaka na kijiji chenye wafugaji wengi cha Mabwerebwere, Ramadhan Munuo, Shomari Mkopi na Hamis Msabaha, kwa nyakati tofauti walidai kuwa wakulima wamekuwa wakinyanyaswa na wafugaji kutokana na uduni wa vipato vyao.

Hata hivyo, alidai kuwa pamoja na kushinda kesi ya msingi mwaka 2010 katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kuhalalisha kuwa Kijiji cha Mambegwa ni cha wakulima, baadhi ya wafugaji walienda kukata rufaa Mahakama Kuu na tangu hapo kesi hiyo haijasikilizwa na kutolewa maamuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Dendego, alisema tatizo kubwa lililipo ni Kijiji cha Mabwegele cha wafugaji kuzungukwa na vijiji vya wakulima na kukosekana maamuzi ya kijiji mama.

Hivyo aliwaomba wananchi hao na jamii ya wafugaji waliopo katika mgogoro huo, kuondoa kesi ya rufaa iliyofunguliwa Mahakama Kuu ama iharakishwe kutolewa maamuzi ili Serikali ya Wilaya iweze kuanza kupima mipaka ya vijiji hivyo ili kuondoa migogoro kama wananchi wanavyohitaji.

29 JAN. Wadaiwa sugu Bodi ya Mikopo waanikwa


ZAIDI ya watu 80,000 wakiwemo wa wanasiasa mashuhuri na watoto wao, watumishi wa umma, wafanyabiashara na wanasheria, wametajwa katika orodha ya wadaiwa sugu wa mikopo iliyotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) ili kufanikisha masomo yao katika vyuo mbalimbali nchini.

Katika orodha hiyo, BLOG HII imefanikiwa kuyaona majina ya vigogo katika taasisi mbalimbali, na watoto wa vigogo serikali katika vyama vya siasa.

Mbali ya kuanika majina hayo kwenye mtandao wa bodi, www.heslb.go.tz, pia bodi hiyo inakusudia kuwachukulia hatua za kisheria kwa watakaoshindwa `kujisalimisha’ na tayari kampuni nne za udalali zimeshapewa jukumu hilo.

Idadi kubwa ya watakaoingia katika `mshikemshike’ na bodi ni wale walionufaika na mikopo hiyo na kuhitimu kati ya mwaka 1994 na 2009 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo cha Usimamisi wa Fedha Zanzibar.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Masobwa aliyesisitiza kuwa, lazima walionufaika wabanwe kwa kuwa walichokuwa wamepewa hakikuwa msaada au ruzuku.

“Sheria iko wazi kwamba baada ya kuhitimu, mnufaika anapewa mwaka mmoja wa kupumua, na baadaye anaanza kulipa bila riba.

“Kwa kuwa tumeshasumbuana vya kutosha, sasa hatutaki kusumbuana tena na wadaiwa hawa ninaoweza kuwaita ni sugu kwa sababu zaidi ya mara tatu tumeshawakumbusha kulipa, lakini hakuna mwitikio,” alisema Masobwa.

Alifafanua kuwa, wakati Bodi inaanzishwa mwaka 2005, ilirithi madeni ya serikali kiasi cha sh bilioni 51 kilichokuwa kimekopeshwa tangu mwaka 1992/3.

Na ili kuokoa kiasi hicho cha fedha na madeni mengine, sasa imelazimika kutumia nguvu ya ziada, kwa kuingia mkataba wa kukusanya madeni na makampuni ya Msolopa Investment Co. Ltd, Nakara Auction Mart na Sikonge International Co. Ltd ya Dar es Salaam na nyingine ya Dodoma, Dodoma Universal Trading Co. Ltd.

“Kazi ya makampuni haya itakuwa kuwachimbua huko wasikotaka kutoka, na tumekubaliana kwamba wadaiwa ndio watakaobeba gharama za usumbufu wa wakusanya madeni kuwafuata huko waliko.

“Na ikumbukwe baada ya muda huo, madeni yatakwenda sambamba na riba, ingawa kwa watakojitokeza sasa na kuweka wazi utaratibu wa malipo, hawataguswa,” alisema.

Akifafanua juu ya wahitimu ambao hawana ajira, alisema hilo si tatizo, bali mdaiwa anapaswa kuiarifu bodi kwa maandishi akielezea jina alilotumia akiwa chuoni, chuo alichohitimu, kozi aliyohitimu, mwaka aliohitimu, anuani yake na namba yake ya simu.

“Mara baada ya kupata taarifa za mdaiwa Bodi itampa maelezo yahusuyo deni lake na kujadiliana naye jinsi atakavyolipa deni. Endapo mdaiwa atashindwa kulipa deni lake atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

“Na endapo atachelewa kuanza kulipa deni lake atapewa adhabu ya ongezeko la asilimia 10 ya mkopo wake, ndiyo mwongozo wetu unavyosema,” alisema.

Akizungumzia suala la wadaiwa waliojiriwa, alisema nao wanapaswa kuwasiliana na bodi ili kupata maelezo sahihi ya mkopo na kueleza jinsi watavyolipa deni, huku wakiwajibika kuhakikisha makato kwenye mishahara yao yanawasilishwa HESLB.

Pamoja na kukatwa marejesho ya mkopo kwenye mshahara, wadaiwa pia wanaweza kuweka kiasi chochote cha fedha kwenye akaunti ya bodi ikiwa ni marejesho ya mkopo, kwa lengo la kupunguza haraka deni lake.

“Vivyo hivyo kwa aliyejiajiri, anapaswa kuwasiliana na bodi ikiwa pamoja na kueleza aina ya shughuli anayoifanya na mahali ilipo, na ndipo bodi itampa maelezo yahusuyo deni lake na namna ya kulipa deni,” alisema.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 9 ya mwaka 2004 na ilianza kufanya kazi mnamo mwezi Julai mwaka 2005.

Kwa mujibu wa sheria hii, baadhi ya majukumu makuu ya Bodi ni pamoja na kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika masomo ya shahada au stashahada ya juu katika taasisi za elimu ya juu zinazotambuliwa na Serikali hapa nchini na nje ya nchi.

Aidha, sheria hii imeipa Bodi mamlaka ya kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu walionufaika na mikopo hiyo kuanzia mwaka 1994 ili pesa hizo ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine watakaohitaji.

Tangu mwaka 1994, kumekuwa na awamu tatu za ukopeshaji, ya kwanza ikianza kutekelezwa mwaka 1992/93 ambapo wanafunzi walitakiwa kujilipia gharama za usafiri kwenda chuoni na kurudi nyumbani, gharama za udahili na usajili pamoja na michango ya serikali za wanafunzi. Gharama hizi zilikuwa ni ndogo na kila mwanafunzi aliweza kuzimudu.

Katika awamu ya pili, mwanafunzi pamoja na kuchangia gharama zilizoainishwa katika awamu ya kwanza, alilazimika pia gharama za chakula na malazi. Gharama hizi ambazo kwa wakati huo zilifikia sh 350,000.00 kwa mwaka zilionekana kuwa kubwa kwa wanafunzi walio wengi.

Lakini, serikali katika kuhakikisha kuwa kuna fursa sawa katika utoaji elimu ya juu, ilianzisha utaratibu wa mikopo ili wanafunzi ambao hawana uwezo wa kujigharamia waweze kukopeshwa moja kwa moja kutoka Serikalini. Utaratibu huu ulianza kutumika mwaka 1994/95 na uliendelea kutumika hadi mwaka 2004/2005.

Na katika awamu ya tatu iliyoanza utekelezaji wake mwaka wa masomo wa 2005/06 baada ya kuanzishwa kwa Heslb, mwanafunzi anapaswa kujigharamia pamoja na gharama zilizotajwa kwenye awamu ya kwanza na pili, gharama zote zingine za masomo, ama kwa njia ya mkopo kutoka kwenye Bodi au kwa njia zake mwenyewe

29 JAN. Ghana yaelekea robo fainali


Ghana inaelekea kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya Jumamosi kuishinda Mali magoli 2-0.
Andre Dede Ayew

Ayew aliyepokea tuzo la BBC la mchezaji bora hivi majuzi alionyesha ustadi kwa kufunga bao la pili la Black Stars

Asamoah Gyan ndiye aliyefunga bao la kwanza la Black Stars.

Andre 'Dede' Ayew kisha aliwachanganya walinzi wa Mali na kupitia nafasi iliyojitokeza, aliandikisha bao la pili la Ghana.

Awali Cheick Diabate mara mbili ilikuwa nusra aifungie Mali magoli, lakini kweli bahati haikuwa yake, kwani mipira yote iligonga goli, lakini kamwe mpira ulikataa kugusa nyavu katika mechi hiyo iliyochezewa mjini Franceville.

Ghana inaongoza kundi D kwa pointi sita, lakini kimahesabu, mataifa ya Guinea na Mali bado yana nafasi ya kufuzu kuingia robo fainali.

Guinea kwa hakika ilithibitisha uwezo wake katika mashindano hayo kwa kuiangamiza bila huruma Botswana, magoli 6-1, katika mechi ambayo pia ilichezewa mjini Franceville.

Guinea inatazamia wingi huo wa mabao huenda ikawa jambo zuri, na inasubiri kwa hamu kusikia matokeo ya mechi kati ya Mali na Botswana Jumatano ijayo mambo yatakuwa vipi, na wakati ambao wao watacheza na Ghana.

Lakini kumbuka Jumapili kuna mechi za kuvutia pia, wakati wenyeji wenzao Guinea wakipumzika, Equatorial Guinea watakuwa na kibarua cha kucheza na Zambia mjini Malabo, huku Libya nayo ikicheza na Senegal mjini Bata.

29 JAN.YANGA YAFANYA KWELI


Alikuwa mshambuliaji na mchezaji bora wa Uganda, Hamisi Kiiza aliyeokoa jahazi la mabingwa wa Tanzania Bara Yanga kutokomea kwenye gwaride la JKT Ruvu kabla ya Mwasika kuipoteza JKT Ruvu.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa, JKT Ruvu walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 33 kupitia kwa Amos Mgisa.

Kama yanga wangekuwa makini wangekwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2 ama zaidi, lakini walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli moja huku wakipoteza nafasi walizopata kupitia kwa Kenneth Asamoah.

Yanga iliwabidi wangoje mpaka dakika ya 60, ambapo walisawazisha goli kupitia kwa Hamisi Kiiza kwa Mkwaju wa penati, na dakika 19 mbele Kiiza alirejea tena nyavuni kwa kuifungia Yanga goli la pili.

Wakati JKT Ruvu wakiwa wanajiuliza kilicho wasibu walijikuta wanatundikwa msumari wa tatu katika dakika ya 89 kupitia kwa Stephan Mwasika, hivyo kuwaashia indiketor Simba waliopo kileleni.


Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliochezwa Mlandizi ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 pale Ruvu shooting ulipo wakaribisha Kagera Sugar.

Katika mchezo huo magoli yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza, huku Ruvu Shooting wakiwa wa mwanzo kupata goli katika sekunde ya 33 kupitia kwa Abdurahman Abdurahman.

Kagera Sugar walikuja kusawazisha goli hilo katika dakika ya 26, na kupelekea mchezo kuisha kwa sare ya goli 1-1.


Katika uwanja wa Azam, Toto Africa imekubali kupokea kichapo cha pili mfululizo toka kwa Villa Squad inayoangaika kujinasua toka mkiani, wakati jahazi la Toto likiendelea kuzama.

Magoli ya mshambuliaji wazamani wa Moro united na Yanga Nsa Job na Makundi yalitosha kuwapa point 3 muhimu Villa Squad na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (14) 31
2. Yanga (15) 31
3. JKT Oljoro (14) 26
4. Azam FC (14) 26
5. Mtibwa Sugar (14) 22
6. Kagera Sugar (15) 20
7. JKT Ruvu (15) 17
8. Ruvu Shooting (15) 17
9. Moro United (14) 15
10. African Lyon (14) 14
11. Toto Africa (15) 13
12. Polisi Dodoma (14) 12
13. Coastal Union (14) 11
14. Villa Squad (15) 10

Saturday, January 28, 2012

28 JAN. TUCTA waanzisha moto upyaaaaaa


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limewasha moto mpya wa kutaka kima cha chini cha mshahara kiwe sh 500,000 badala ya kile ilichopendekeza mwaka juzi cha sh 315,000.

TUCTA imesema inataka kima cha chini kwa wafanyakazi kiwe sh 500,000 kwa kuwa gharama za maisha zimepanda maradufu ilhali kima cha chini kwa watumishi wa umma hakizidi sh 200,000.

Msimamo huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicholaus Mgaya, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa TUCTA, mkoa wa Dsm ambaye alisema mishahara ya wafanyakazi wa umma nchini ni midogo ukilinganisha na ile wanayolipwa wenzao wa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Mgaya alisema mwaka juzi TUCTA ilitaka serikali kulipa kima cha chini cha sh 315,000 lakini sasa gharama za maisha zimepanda zaidi hivyo ni vema kikaongezeka na kuwa sh 500,000.

Alisema ni aibu kuzungumzia kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa umma hapa nchini kutokana na udogo wake ambao serikali haionekani kushtushwa na upandaji wa gharama za maisha ambao hauendani na kipato.

“Mishahara yetu ni midogo huwezi kumwambia mtu unapata sh 150,000 kwa kuwa ni aibu. Hata mshahara wa kima cha chini wa sh 315,000 tulioupendekeza Tucta wakati ule, hivi sasa umepitwa na wakati, hivyo mapendekezo yetu kima cha chini kiwe ni sh 500,000,” alisema.

Kwa mujibu wa Mgaya, hivi sasa maisha yanapanda kila kukicha, wenye nyumba nao hasa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakipandisha kodi kila wakati bila kujali hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida.

Pia alisema kuwa, Tucta imelizingatia suala la kupanda kwa gharama za umeme na vitu vingine, hivyo utafiti unafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Mzumbe, ili kuwapatia hali halisi ya suala la uchumi nchini kabla ya kulizungumza.

SOURCE DARHOTWIRE

28 JAN. Man U nje FA


Mkwaju wa dakika za mwishomwisho wa Dirk Kuyt uliiwezesha Liverpool siku ya Jumamosi kuiondoa Manchester United katika mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA, ilipoishinda magoli 2-1.

Bao la mshambulizi huyo lilikuwa muhimu sana katika mechi iliyochezewa uwanja wa nyumbani wa Liverpool wa Anfield.

Awali ilielekea kana kwamba timu hizo zitakutana tena katika uwanja wa Old Trafford, kwani Ji-Sung Park alikuwa amefanikiwa kuisawazishia Manchester United.

Nyota ya Liverpool inaelekea kung'ara, kwani meneja Kenny Dalglish tayari amekiwezesha klabu kufanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Carling, mechi ambayo itakuwa ni nafasi yao ya kwanza tangu mwaka 1996 kucheza katika uwanja wa Wembley, baada ya kuiondoa Manchester City.

Mechi hiyo ilichezwa kukiwa na wasiwasi kwamba ilikuwa ni rahisi ghasia kuanza, kufuatia mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez, hivi majuzi kuchukuliwa hatua kwa kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya nahodha wa Manchester United, Patrice Evra.

Suarez, kutoka Uruguay, pia aliadhibiwa na chama cha soka cha FA asicheze katika mechi nane.

Licha ya makocha wa timu zote kuwataka mashabiki kuwa watulivu, Evra alizomewa mara kwa mara katika mechi hiyo.

28 JAN. MATONYA AUZA MJENGO WAKE


SIRI imefichuka kwamba Matonya ameuza nyumba yake ya jijini Tanga, lakini amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba amefanya hivyo ili mambo yaende sawa kimaisha na siku si nyingi ataibukia kwingine.

Staa huyo aliyewahi kuvuma na nyimbo kama 'Anita' na 'Tax Driver' amekuwa akijaribu kurudi kwenye chati ya muziki bila mafanikio ingawa habari zinasema ameamua kujihusisha na biashara zingine.

Pamoja na rafiki zake kudai alikuwa akisoma kozi fupi ya kompyuta, lakini wamedokeza kuwa msanii huyo ameuza nyumba ili kupiga dili zingine na huenda akaanza kujenga tena baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa karibu, msanii huyo aliwaambia; Nimeuza na natumia hizo pesa kujenga nyumba nyingine, halafu nashindwa kuelewa hata watu wamejuaje

Msanii huyo hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo kwa madai kuwa anaandaa mipango ya shoo zake za Ulaya.

28 JAN. YOUSSOU N`DOUR ATOSWA KUWANIA URAIS WA SENAGAL


Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amewasihi wananchi wawe watulivu baada ya maandamano ya ghasia kuzuka kufuatia uamuzi wa mahakama kumruhusu agombee muhula wa tatu wa urais.

Bwana Wade, mwenye umri wa miaka 85, alisema kuonesha hasira kwa fujo hakutaleta tija yoyote.

Alitokeza kwenye televisheni huku ghasia zinatapakaa katika miji kadha ya Senegal.

Katika mji mkuu, Dakar, vizuizi viliwekwa, magari yalipinduliwa na maduka kadha yalichomwa moto.

Wakuu wanasema askari polisi mmoja aliuwawa.

Mpinzani maarufu, mwimbaji Youssou N'Dour, ameonya kuwa hukumu ya mahakama ya katiba haitakubalika.

Mahakama hayo yalitupilia mbali ombi la Bwana N'Dour kutaka kugombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao

28 JAN.BREAKING NEWS; WEMA, KAJALA WAGOMBEA BWANA


Na Mwandishi Wetu
KIMENUKA! Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja, wanadaiwa kuingia kwenye bifu ‘babkubwa’ kisa kikidaiwa ni kugombea mwanaume, Ijumaa lina fulu data.
NI KIGOGO WA IKULU
Kwa mujibu wa chanzo kisicho na shaka, hivi karibuni warembo hao ‘wanaokinukisha’ katika tasnia ya filamu Bongo, walijikuta wakiingia kwenye gogoro kufuatia Kajala kutuhumiwa ‘kumtokea’ mwanaume mpya wa Wema aliyetajwa kwa jina moja la Clemence ambaye anadaiwa ni kigogo wa Ikulu.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wema alimtambulisha Kajala kwa mwanaume huyo mwenye noti zake tofauti na msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ aliyekuwa ‘akiminya’ na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

KAJALA ASAKA NAMBA YA GARI
Ilidaiwa kuwa, baada ya Kajala kutambulishwa kama shemeji, ulipita ukimya f’lani, nyuma kukiwa na madai kuwa alikuwa akisaka namba ya gari la jamaa huyo ili kumsaidia kufahamiana naye kabla ya kunasa namba yake ya simu.
“Asikwambie mtu, Kajala alipokosa namba ya simu, mwanzoni alikuwa akisaka mpaka namba ya gari, lakini Mungu si Athumani, alifanikiwa kupata ya kilongalonga ‘coz’ Wema aliachia mwanya fulani akijua ni shosti wake hivyo hawezi kufanya chochote.
“Kikulacho ki nguoni mwako, fumba fumbua Wema akapelekewa malalamiko na mwanaume kuwa Kajala anataka mambo,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki mkubwa wa wawili hao.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, baada ya Wema kufikishiwa ushahidi wa ‘sms’, kama kawaida yake, hakuhoji chochote zaidi ya kumvaa Kajala mzimamzima na kukinukisha na sasa hawaivi.


Huku kikilionesha Ijumaa ushahidi kwenye mtandao wa BBM, chanzo hicho kilidai kuwa ishu hiyo ilihamia kwenye mtandao huo ambapo Kajala aliweka picha ya Jokate Mwegelo na Diamond akiandika: “Chezea Hao!”
Ilisemekana kuwa, picha hiyo ilitoa nafasi kwa wadau wa mtandao huo kumtukana Wema kwa kuweka maoni ya matusi.
Habari zilizidi kuweka kweupe kuwa, Wema aliposikia ishu hiyo, alizama mtandaoni humo na kujionea mwenyewe.

WEMA AJIBU MAPIGO
Ilielezwa kuwa, katika vitu ambavyo Wema huwa hapendi ni kusikia au kutajiwa ishu ya Jokate na Diamond hivyo naye akajibu mapigo.
Ilifahamika kuwa, Wema naye alitafuta picha ya bwa’mdogo anayedaiwa kutoka naye aliyetajwa kwa jina moja la Petty Man akiwa kimahaba na kidemu kingine kilichotajwa kwa jina moja la Hamisa, hivyo Kajala naye akapokea za uso laivu kutoka kwa wadau wa mtandao huo.
Hata hivyo, pamoja na hayo, ilidaiwa kuwa Kajala hakufanikiwa kumnasa mwanaume huyo kufuatia Wema kuweka ulinzi mkali na kuvunja ushosti wao.

MSAKO KUWEKA HESHIMA MJINI
Chanzo kiliendelea kusema kuwa, baada ya wawili hao kutifuana kwa maneno, sasa wanasakana ili kushikishana adabu na kuwekeana heshima mjini.

KAJALA ANASEMAJE?
Kama kawa, kama dawa, baada ya mtiti huo kutua kwenye dawati la Ijumaa, mtu wa kwaza kutafutwa ili kuweka wazi anachokijua ni Kajala ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Duh! Kweli nyie mnatisha, mimi sina ‘comment’ muulizeni huyo Wema.”

HEBU MSIKIE WEMA
Alipotafutwa Wema na kumwagiwa ‘upupu’ mwanzo hadi mwisho, alikuwa na haya ya kusema:
“Siwezi kugombea mwanaume na Kajala, ila kuna kitu kilitugombanisha.
“Huyo Hamisa ni mdogo wangu wa hiari ‘so’ nina uhuru wa kuweka kitu chochote kwenye ukurasa wangu wa BBM.”
Alipotakiwa kueleza hicho kilichosababisha wakagombana, Wema hakuwa tayari, lakini Ijumaa linaendelea na mchakato kujua kisa na mkasa kwani ndiyo muvi imeanza, kaa tayari.

SOURCE GLOBAL PUBLISHERS

28 JAN. Gabon yaingia robo fainali


Gabon ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 katika dakika ya mwisho, ilipocheza dhidi ya Morocco siku ya Ijumaa, na kufuzu kuingia robo fainali katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kwa muda mrefu, Morocco ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 katika mchezo huo, bao ambalo lilikuwa limepatikana kupitia nahodha Houssine Kharjah katika kipindi cha kwanza.

Lakini kupitia magoli ya Pierre-Emerick Aubameyang na Daniel Cousin, wenyeji Gabon waliweza kuongoza, hadi mkwaju wa Kharjah ulipoiwezesha Morocco kupata nafasi ya kwanza, na ilielekea mechi itaishia kwa sare ya 2-2.

Lakini Morocco walipoadhibiwa kwa kucheza vibaya, Bruno Zita Mbanangoye alipiga mkwaju kwa ufundi mkubwa, na mpira ulipinda hadi kuingia wavuni, na bao hilo la wakati wa majeruhi likawa ndio kwaheri kwa timu ya Morocco.

Gabon sasa inajiunga na wenyeji wenzao Equatorial Guinea, katika hatua ya robo fainali.

Equatorial Guinea walifanikiwa kuiondoa Senegal siku ya Jumatano, taifa ambalo lilitazamiwa na wengi kuwa miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mwaka huu.

Katika mechi ya awali siku ya Ijumaa, ambayo pia ilichezewa mjini Libreville, Niger iliondolewa na Tunisia, kwa kufungwa magoli 2-1.

Hata hivyo Niger ilikuwa bado na matumaini ya kusonga mbele, ikitazamia Morocco kuwafanyia kazi yao, kama ingeliweza kuishinda Gabon.

Lakini hayo hayakuwezekana, na hivyo basi Niger inajiunga na Morocco katika safari ya kurudi nyumbani.

Mechi za Jumamosi pia zinatazamiwa kuwa za kusisimua, wakati Botswana itakapokutana na Guinea, na Ghana nayo itacheza na Mali.

Mechi zote mbili ni za kundi D, na zote zitachezewa mjini Franceville.

Friday, January 27, 2012

27 JAN. MABADILIKO MAKUBWA NDANI YA FACEBOOK, KUWA MAKINI




Facebook ikiwa ni nyumba ya online kwa mamilioni ya watu duniani, hivyo mabadiliiko yanayotokea kwenye facebook ni dhahiri yanaathiri wengi wetu. Katika siku za karibuni Facebook wamekuja na kitu kipya ambacho wenyewe wanakiitaTimeline, hii Timeline ni mpangilio mpya wa kurasa za facebook ambao unamuwezesha mtumiaji kupanga picha, matukio n.k kulingana na muda husika.
Katika Timeline, utaweza kupanga taarifa zako kwa mtindo wa kipekee zaidi huku ukimpa nafasi mtembeleaji kuzipitia kwa haraka zaidi. Kama utaangalia picha ya hapo juu, utaona kwenye timeline yangu mtu akija mara ya kwanza ataona marafiki, picha na mengine mengi. Siyo hayo tu, kwa kutumia Timeline mtu anaweza kuangalia matukio yako toka siku ya kwanza uliyojiunga na facebook.
Katika siku zilizopita Timeline ilikuwa ni kwa wanaohitaji, ila kuanzia tarehe moja mwezi wa pili Timeline itakuwa ni lazima, utake usitake ni lazima utumie au kwa lugha ya kiufundi tunaweza iita default. Hivyo usishangae kuona mabadiliko kwenye kurasa yako.

Kitu ambacho kimenivuta kuandika hii makala ni kuwa, ingawa Timeline ni nzuri na ya kuvutia, ila Facebook inaonekana wanazidi kufanya mambo kuwa magumu, ni dhahiri kuwa kufanikiwa kwa facebook kumekuja kutokana na urahisi wa utumiaji. Hivyo kufanya mambo kuwa magumu kutawafanya watu wengi kuikimbia au kushindwa kuifungua hususan wale walio kwenye mgao wa bandwith (internet zilizo taratibu mno). Kuna siku niliwahi kuona mpachiko wa rafiki yangu ambaye ni mtumiaji mzuri mno wa facebook, yeye alikuwa akilalamika kwa kusema nani amesema tunataka hii Timeline?

Kitu kingine kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa ni privacy, facebook wenyewe mara kibao wamekiri kuwa privacy ni moja ya vitu vinavyowaumiza kichwa, kwenye facebook ya sasa mtu anaweza kuona matukio yako ndani ya wiki hadi mwezi, ila sasa kwenye hii Timeline mtu anaona tukio tangu siku ya kwanza uliyojiunga facebook, sasa huku si kuwaumbua watu? Chukulia mfano kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuongopa, huu si ndio mwanzo wa kukamatwa? Hivyo basi kwa kuweka Timeline kuwa default kutawatatiza wengi. Habari njema ni kuwa kuanzia sasa unaweza kuanza kufuta matukio kadhaa usiyopenda kuwaonesha watu hadi hapo Januari 31.

27 JAN. Papic awashukia washambuliaji


KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic amekemea uzembe wa washambuliaji wake na kudai makosa yao yanaiweka timu hiyo kwenye wakati mgumu.Papic aliyasema hayo wakati wa mazoezi ya jana asubuhi kwenye viwanja vilivyopo katika shule ya Sekondari ya Loyola.

Katika kile kinachoonekana kuchoshwa na tabia hiyo ya washambuliaji kushindwa kufunga, Papic alisisitiza kwamba anataka umakini wa kufunga kutoka kwa wachezaji hao.

Mchezaji mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa siku mbili hizi kocha amekuwa mkali kwa washambuliaji kwa madai kuwa wanamuangusha mara zote hasa wakiwa wanakabiliwa na mechi muhimu.

"Kocha amekuwa mkali sana kwa washambuliaji akidai kuwa hata timu ikicheza vizuri sehemu nyingine zote washambuliaji wasipofunga ni kazi bure,"alisema mchezaji huyo.

Baada ya mazoezi hayo kocha Papic alisema kuwa nia ya mchezo wowote ni ushindi hata kama utacheza vizuri vipi usiposhinda utabaki kuwa wa mwisho.Alisema ili timu ifanye vizuri na iweze kusonga mbele ni lazima iwe na washambuliaji makini na wenye uwezo wa kufunga kila nafasi inapojitokeza.

"Kwenye kila mchezo ushindi lazima hivyo ni lazima washambuliaji wajue namna ya kuzitumia nafasi hizo zinazopatikana," alisema Papic.

27 JAN.Ivory Coast yaingia robo fainali


Ivory Coast ilifanikiwa kuishinda Burkina Faso 2-0 katika uwanja wa Malabo na kufuzu kuingia robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika.
Salomon Kalou

Mshambulizi wa klabu ya Chelsea ya England, Salomon Kalou, ndiye aliyeanza kuona wavu kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 16, na Bakary Kone akamfunga kipa wake mwenyewe, zikiwa zimesalia dakika nane kabla ya mechi hiyo kumalizika.

Lakini licha ya wachezaji wengi wa Ivory Coast ambao huwa wanacheza katika ligi kuu ya Premier nchini England kuwa uwanjanji, hawakuonyesha mchezo wa kusisimua, kwani wachezaji wa Burkina Faso waliweza kuumiliki mpira kwa muda mrefu.

Kwa kushindwa katika mechi mbili mfululizo, juhudi za Burkina Faso hazikufika popote, na itabidi kurudi nyumbani.

Katika mechi iliyotangulia Alhamisi, Sudan iliweza kupata pointi yake ya kwanza katika mashindano hayo, baada ya miaka 36, kufuatia sare ya 2-2 ilipocheza na Angola.

Mechi hiyo pia ilichezewa mjini Malabo.
Airosa Marco na Ahmed

Sudan ilijikakamua na kutoka sare na Angola

Angola iliweza kupata bao la kwanza, baada ya dakika nne tu, wakati Manucho alipogundua kosa lililofanywa na washambulizi wa Sudan, na kwa haraka akaitumia nafasi iliyojitokeza kuandikisha bao.

Lakini baada ya juhudi kubwa, Sudan iliandikisha bao lake la kwanza katika fainali za mashindano hayo, tangu mwaka 1976, wakati Ahmed Bashir aliingiza wavuni bao la kichwa.

Manucho alifunga tena kwa mkwaju wa penalti, lakini naye Bashir akapata bao la kusawazisha, katika dakika za mwishomwisho za mchezo.

Mechi za Ijumaa zitachezewa katika uwanja wa Libreville, wakati Gabon, ambao wanashirikiana na Equatorial Guinea kuandaa mashindano, watawakaribisha Morocco.

Hii inatarajiwa kuwa mechi ngumu na ya kusisimua.

Hata hivyo, kabla ya mechi hiyo, Niger, ambayo inashiriki katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza, itapambana na Tunisia.

27 JAN. Tevez aingia hasara ya paundi milioni 9


Mzozo baina ya Carlos Tevez na Manchester City umemgharimu mshambuliaji huyo wa Argentina paundi milioni 9.3 za mshahara wake, faini alizotozwa na kupoteza bakhshishi.
Mzozo wa Tevez wamgharimu mchezaji huyo paundi milioni 9

Mzozo wa Tevez wamgharimu mchezaji huyo paundi milioni 9

Taarifa zinazohusiana

Kandanda,
Michezo

Imefahamika hajalipwa mshahara wake, unaokadiriwa kuwa paundi 200,000 kwa wiki, tangu mwishoni mwa mwezi wa Novemba.

Na pia hivi majuzi alitozwa faini ya paundi milioni 1.2 kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kurejea akitokea Amerika Kusini.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Manchester City Khaldoon al-Mubarak aliishutumu klabu ya AC Milan kutokana na mwenendo wao kujaribu kumsajili Tevez, akisema mbio za kumchukua zinawashinda.

Tevez mwenyewe anapendelea kujiunga na AC Milan lakini Al-Mubarak aliishutumu klabu na makamu mwenyekiti wa AC Milan Adriano Galliani, akisema Wataliano hao mazungumzo yao na Tevez pamoja na washauri wake yalikuwa ya "haraka".

"Kadri mambo yanavyokwenda, AC Milan si chaguo la Carlos," alisema Al-Mubarak, ambaye atakuwa tayari kumuachia Tevez kwa kitita cha paundi milioni 25.

Akizungumza kwa mara ya kwanza hadharani, Al-Mubarak aliliambia gazeti la Abu Dhabi: "Iwapo wanataka tuwasikilize wakati huu wa dirisha dogo la usajili, wanawajibika kuacha mara moja kupongezana na waanze kufikiria namna watakavyokubaliana na matakwa yetu.

Mzozo huu unaoendelea ulianza wakati Tevez alipotozwa faini ya kukatwa mshahara wa wiki mbili baada ya meneja Roberto Mancini kudai mshambuliaji huyo alikataa kucheza akiwa mchezaji wa akiba wakati Manchester City walipopambana na Bayern Munich mwezi wa Septemba katika patashika za Ubingwa wa Ulaya, ingawa Tevez alidai hawakuelewana.

Alikwenda Amerika Kusini na kugoma kwake kurejea kumemsababishia atozwe faini ya kukatwa mshahara wa wiki sita ambao ni sawa na paundi milioni 1.2.

Mkataba wa sasa wa Tevez unamalizika mwezi wa Juni mwaka 2014, lakini mshambuliaji huyo hajacheza kandanda tangu tarehe 21 mwezi wa Septemba na kwa sasa yupo kwao Argentina.

Wednesday, January 25, 2012

25 JAN. KAULI MPYA YA BOB JUNIOUR KUHUSU DIAMOND!



Mwimbaji/Producer wa SHAROBARO RECORDS Bob Juniour, leo amezungumza ukweli wake kwamba japo walimaliza ugomvi uliokuwepo kati yake na msanii mwenzake DIAMOND PLATNUMS, hajawah kuongea hata kwenye simu na msanii huyo kwa kipindi kirefu, toka walipopatana.
Bob amesema alipatana na DIAMOND ili kumaliza skendo zilizokua zikiandikwa na magazeti ya udaku kuwahusu wao, ishu ambazo ambazo ziliichukiza familia yake na fans wake ndio maana akaamua kupatana ili kuzinyamazisha hizo skendo.
akiongea exclusive na millardayo.com BOB JUNIOUR amesema “kiukweli sasa hivi mimi na DIAMOND hatuongei, na nimeufuta mpango wa kufanya nae chochote kwenye muziki”
mwishoni mwa mwaka jana wakati Bob Juniour alipofanya interview na Millard Ayo siku chache baada ya kupatana na Diamond, alisema huenda december mwaka jana wangefanya kolabo na kuungana kwenye consert moja ambayo ingethibitisha zaidi kwamba wamepatana.

25 JAN. Fifa yaipa Yanga siku 30 imlipe Njoroge


SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) limeipa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam siku 30 iwe imemlipa beki wa zamani wa timu hiyo, John Njoroge, Sh 17, 159,800.

Uamuzi huo uliotolewa na Fifa kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (DRC) umeelezwa kuwa fedha hizo ni fidia kwa mchezaji huyo baada ya Yanga kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa uamuzi huo wa DRC uliotolewa chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu.

Njoroge ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake Fifa kupinga Yanga kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano. Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa Kenya.

“Yanga ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo.

“Klabu hiyo inatakiwa iwe imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo. Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa mwaka ya fedha hizo.

“Ikiwa Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Fifa kwa hatua zaidi,” alisema Wambura.

Akizungumzia suala hilo jana, Ofisa Habari wa Yanga, Luios Sendeu alisema bado hawajapokea barua hiyo na kwamba watakapoipata watatoa tamko.

“Tumesikia jambo hili, lakini tukishajulishwa rasmi, basi tutatoa taarifa yetu,” alisema Sendeu.

25 JAN. Simba, Coastal mambo hadharani leo


VINARA wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wanashuka dimbani kuzindua ngwe ya lala salama ya ligi hiyo, huku wakitarajia kutumia vizuri mwanya wa wapinzani wao Yanga kushindwa kuwashusha kileleni mwa msimamo pale wakatapokuwa wenyeji wa Coast Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilikuwa na fursa nzuri ya kuishusha Simba kileleni mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini ilishindwa kufanya hivyo kufuatia kubanwa na sare ya 2-2 dhidi ya Moro United katika siku ya kwanza ya mwanzo wa mzunguko wa pili.

Zote sasa zina pointi 28, lakini Yanga ikibaki nafasi yake ya pili kutokana tofauti ya mahesabu ya mabao ya kufunga na kufungwa kuwapa faida zaidi wapinzani wao, ambao pia wako nyuma kwa mchezo mmoja mpaka leo.

Wekundu wa Msimbazi watasaka pointi tatu dhidi ya Coastal katika hali ya kujiamini yenye kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata kwenye mechi ya kwanza mwaka jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Lakini pengine hilo halitatosha kuwapa matumaini sana Simba, hasa ukizingatia kuwa karibu timu zote za Ligi Kuu zilifanya marekebisho ya usajili wakati wa dirisha dogo Januari hii.

Katika usajili wao, Coastal Unionn waliomaliza mzunguko wa kwanza na ushindi wa mechi tatu kati ya 13, imemuongeza kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Edwin Mukenya.

Ni wazi mechi hiyo itakuwa ngumu kwa vile vijana hao wa Tanga hawatapenda kuwa ngazi kwa Simba, lakini pia ushindi kwao itakuwa faraja ya ukombozi wa kujinasua toka kwenye mstari wa kushuka daraja.

Wakati Wagosi wakijipanga hivyo, wapinzani wao leo watashuka dimbani bila kuwa na nyota wawili tegemeo akiwemo wa bei mbaya, Felix Sunzu na winga Ulimboka Mwakingwe ambao wote ni majeruhi.

Kwa maana hiyo, Kocha Milovan Cirkovic atalazimika kumtumia chipukizi Ramadhan Singano ili acheze na mshambuliaji Gervais Gargo, huku wakisaidiwa na viungo Uhuru Seleman na Haruna Moshi'Boban'.

Mbali ya kipute hicho, utamu mwingine wa msuguano wa mzunguko wa pili utakuwa nje kidogo ya jiji, wakati wenyeji na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC watakapokuwa wakisaka pointi kwenye Uwanja wa Chamazi dhidi ya African Lyon.

Azam katika nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na pointi 23, tano nyuma ya vigogo Simba ya Yanga na pointi tatu nyuma ya wanaoshia nafasi ya tatu, JKT Oljoro, itakuwa na kila sababu ya kuthibitisha ubora wao kama mashabiki wengi wanavyoona.

Usajili mzuri waliofanya wakati wa dirisha dogo kwa kuwaongeza Gaudence Mwaikimba, Kipre Bolou na kiungo Abdi Kasim ni wazi wataweza kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 na wapinzani wao hao duru la kwanza.

Wakati huohuo, mchezo wa Ligi Kuu kati ya Toto African na African Lyon uliopangwa kuchezwa Februari 5, na sasa kuchezwa Aprili 18, huku pia mabadiliko hayo yakiathiri mechi za Villa Squad dhidi ya Lyon na Azam na Toto African.

Sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni matumizi ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambao tarehe hiyo utatumika kwa sherehe za kichama.

Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema mechi kati ya Villa na Lyon utachezwa Aprili 22 badala ya Aprili 18, huku Azam na Toto wakishuka dimbani Aprili 26 badala ya Aprili 29.

25 JAN. Ocampo asema hakati rufaa kuhusu Kenya


Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ua Jinai,ICC, iliyoko mjini The Hague Louis Moreno Ocampo anasema atawasilisha ushahidi zaidi kutaka mashtaka yathibitishwe dhidi ya wakenya wawili mashuhuri, ambao majaji katika mahakama hiyo walikataa kuthibitisha mashtaka dhidi yao kuhusiana na ghasia za baada ya uchagzui wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Siku ya jumatatu mahakama ya ICC ilithibitisha mashtaka dhidi ya washukiwa wanne akiwemo naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, lakini majaji wakasema hawakuridhishwa na ushahidi ulitoloewa na kiongozi wa mashtaka dhidi ya aliyekuwa mkuu wa Polisi Major Generali Hussein Ali na waziri wa zamani Bwana Henry Kosgey, na kwa hivyo wakakataa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Wengine ambao mashtaka yao yalithibitishwa ni mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura, aliyekuwa waziri wa elimu ya juu William Ruto na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang.

Akihutubia waandishi wa habari katika mahakama ya ICC, Bwana Ocampo amesema hatakata rufaa dhidi ya uamuzi wa majaji, lakini ataendelea kukusanya ushahidi zaidi kutoka waathirika na kuuwasilisha tena mbele ya jopo la majaji watatu walioshughulikia kesi hiyo ya washukiwa wa ghasia za Kenya.

Amesema atafanya uchunguzi zaidi juu ya Bwana Ali na Bwana Kosgey wakati kesi dhidi ya watuhumiwa wanne ambao mashtaka dhidi yao yalithibitishwa itakapoanza.

Wakati wa kutoa uamuzi siku ya Jumatatu, jaji kiongozi Ekaterina Trendafilova alisema hawakushawishika na ushahidi uliotolewa wa kumhusisha Bwana Kosgey na ghasia dhidi ya wafuasi wa chama cha PNU katika maeneo kadhaa mkoani Rift Valley.

Alielezea kwamba kiongozi wa mashtaka alitegemea shahidi mmoja tu dhidi ya Bwana Kosgey, na ambaye hakuthibitishwa.

Pia aliongeza kwamba upande wa mashtaka ulibana tarehe ambazo inadaiwa Bwana Kosgey alihudhuria mikutano ya kupanga ghasia, na hivyo kumkosesha fursa ya kuandaa utetezi.

Jaji huyo pia alisema ushahidi uliowasilishwa haukuwa na misingi ya kutosha kuonyesha kwamba Polisi walishiriki kwenye ghasia katika maeneo ya Nakuru na Naivasha.

Kuhusu uamuzi huo, Bwana Ocampo amesema atafanya uchunguzi zaidi katika sehemu za Kisumu na Kibera mjini Nairobi, ambako anadai Polisi walishiriki kwenye ghasia.

Amesema atatafuta ushahidi zaidi kuthibitisha kwamba Bwana Kosgey alihusika kwenye ghasia pamoja na Bwana Ruto na Bwana Sang.

Tuesday, January 24, 2012

24 JAN. Wenger awajia juu mashabiki wa Arsenal


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, ametetea uamuzi wake wa kumpumzisha Alex Oxlade-Chamberlain na nafasi yake kuchukuliwa na Andrey Arshavin wakati walipolazwa mabao 2-1 na Manchester United.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walisikika wakizomea wakati Oxlade-Chamberlain, aliyekuwa chachu ya kupatikana bao la kusawazisha la Arsenal, alipompatia pasi nzuri mfungaji Robin van Persie alipopumzishwa.

"Nimekuwa meneja kwa miaka 30 na nimeshabadilisha wachezaji mara 50,000. Siwajibiki kueleza sababu za kumpumzisha mchezaji kwa mtu yeyote," alisema.

Arsenal iko nyuma ya Chelsea wanaoshilikia nafasi ya nne kwa pointi tano katika mbio za kuwania kufuzu kwa ajili ya kuwania Ubingwa wa Ulaya msimu ujao.

Oxlade-Chamberlain alikuwa mmoja wa wachezaji waliong'ara kwa Arsenal katika mtanange huo uliochezwa katika uwanja wa Emirates.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuanza kucheza mechi yake ya Ligi Kuu ya England, alikuwa akimlisha sana mipira Van Persie wakati wa kipindi cha pili ambapo Arsenal walionekana kucharuka.

"Naelewa mashabiki wamechukizwa kutokana na kumbadilisha Oxlade-Chamberlain, hasa baada ya mabadiliko hayo yaliposhindwa kuzaa matunda, lakini alianza kuchoka," Wenger alifahamisha kutokana na uamuzi wake wa kumpumzisha winga huyo wa zamani wa Southampton.

"Wiki hii alikuwa akiumwa. Arshavin ni nahodha wa timu ya taifa ya Urusi. Una kijana mwenye umri wa miaka 18 akiwa ndio anaanza kwa mara ya kwanza mechi ya Ligi Kuu na mchezaji ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi yake na watu wanahoji kwa nini nimefanya mabadiliko hayo?"

Alipoulizwa namna kufungwa huko kulivyoiathiri timu yake, Wenger alisema ilikuwa ni mechi ya Arsenal "ambayo isingepaswa kupoteza" kabla ya kuongeza: "Imetuweka katika nafasi ngumu sana."

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson alisema kikosi chake kilistahili kushinda hali iliyowaweka pointi tatu nyuma ya Manchester City wanaoongoza ligi kwa sasa.

"Hatimaye nilihisi kikosi chetu kilikuwa imara," alisema. "Hongera kwa wachezaji nafasi ya ulinzi, ambao walifanya kazi kubwa.

Alipoulizwa juu ya kuikamata Manchester City, alisema: "Itakuwa ni kibarua kigumu kwetu sote."

24 JAN. Essien kuingoza Ghana dhidi ya Botswana


GHANA wamepata somo sahihi katika mechi za ufunguzi za Kombe la Mataifa ya Afrika na kusisitiza kuwa hakuna timu mbovu kwenye mashindano hayo.Black Stars waanza kampeni yao leo jijini Franceville kwa kuivaa Botswana huku kocha wao Goran Stevanovic akidai wanataka kuionyesha dunia kwanini Ghana inapewa nafasi ya kuchukua ubingwa huo.

Wachezaji wa Ghana wana morali ya hali ya juu kwenye kambi yao huko Villa Ngoni, lakini kiungo Sulley Muntari amesema hakuna mechi rahisi."Kama ukiangalia nini kilichotokea siku ya ufunguzi utakubalia kwamba hakuna mechi rahisi," alisema Muntari akizungumzia ushindi wa Zambia dhidi ya Senegal. "Tunajiamini vya kutosha, lakini hatupaswa kudharau timu yoyote."

Upande wa pili Botswana watashuka dimbani bila ya kiungo wake tegemeo Joel Mogorosi aliyejiengua kutokana na majeruhi. Mogorosi alivunjika mkono wakati wa mazoezi ya Zebra nchini Cameroon wiki iliyopita na nafasi yake imechukuliwa na Abednego Powell.

Zebra hao tayari walishampoteza kiungo wao Dipsey Selolwane aliyefungiwa kucheza mechi hiyo ya ufunguzi.
Zambia ilichapa Senegal timu inayoaminiwa kutwaa taji hilo, huku Sudan wakiacha maswali mengi kwa Ivory Coast pamoja na kuwa walishinda bao 1-0.

Katika mechi nyingine ya Kundi D, nahodha wa Mali, Seydou Keita huenda akakosa mechi ya kwanza ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea kutokana na maumivu.

Kiungo huyo wa Barcelona, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika, ana maumivu ya goti na enka na huenda akakosa mechi hiyo ya Kundi D itakayochezwa huko Franceville, Gabon leo Jumanne.
Kocha Alain Giresse alikuwa na nia ya kumpanga Cheick Tidiane Diabate, ambaye ni mshambuliaji wa Girondins Bordeaux lakini mchezaji huyo pia ana maumivu ya misuli.

Vile vile Mahamane Traore, ambaye ni kiungo kutoka Metz, hajapona maumivu yaliyomfanya akosekane katika mechi za maandalizi.Keita ndiyo kwanza amerudi katika kikosi cha Mali baada ya awali kuwa amejitoa kwa madai kwamba viongozi wa soka hawatendi haki. Kocha Giresse ndiye aliyemshawishi kurudi katika kikosi hicho.

24 JAN.Kibaki awataka Wakenya wawe watulivu



Wagombea wawili wa urais nchini Kenya wana kesi ya kujibu juu ya uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imeamua.

Naibu Waziri mkuu Uhuru Kenyatta na aliyekuwa waziri William Ruto wote wanakabiliwa na mashtaka.
Ni miongoni mwa wakenya wanne mashuhuri - wote ambao wamekanusha madai hayo - wanaokabiliwa na mashtaka.

Rais wa Kenya amewaomba raia wawe watulivu baada ya uamuzi huo.

" Nchi hii yetu tukufu imekuwa na changamoto kubwa," Mwai Kibaki alisema katika taarifa yake.

Bw Kenyatta - mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya na mtu ambaye ameorodheshwa kama mmoja ya watu matajiri - anakabiliwa na mashtaka yeye pamoja na mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura.

Wawili hao, wote washirika wa rais, wanashutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji na mateso.

Waziri wa zamani wa Elimu William Ruto na mwandishi wa habari Joshua arap Sang wanakabiliwa na mashtaka katika kesi tofauti, kwa kuwa walikuwa wapinzani wa Bw Kibaki wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007. Mahakama ya mjini the Hague iliamua hakuna ushahidi wa kutosha wa kuanzisha kesi dhidi ya maafisa wengine wawili.

Zaidi ya watu 1,200 waliuawa katika wiki kadhaa za vurugu na watu takriban 600,000 wakalazimishwa kukimbia makazi yao. Wengi bado wanakaa katika makambi ya muda.

Monday, January 23, 2012

23 JAN. ICC kutoa uamuzi kuhusu washukiwa Kenya


Mahakama ya kimataifa ya jinai,ICC iliyoko mjini The Hague, Uholanzi, itaamua leo jumatatu ikiwa naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na watu wengine watano mashuhuri wana kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma dhidi yao za kuhusika katika ghasia zilizoikumba nchi hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1,300 waliuwawa.

Washukiwa wengine ni aliyekuwa waziri wa elimu ya juu William Ruto, aliyekuwa waziri wa viwanda Henry Kosgey, mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura, aliyekuwa mkuu wa Polisi Generali Hussein Ali na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang.

Kwa mujibu wa taarufa kutoka ICC, jopo la majaji watatu linaloongozwa na Ekaterina Trendafilova litawasilisha uamuzi wao kwa watuhumiwa na mawakili wao kwanza kupitia maandishi, kisha saa tano na nusu kwa saa za mjini The Hague, ambayo ni sawa na saa saba na nusu Afrika mashariki majaji hao watatangaza hadharani katika mahakama ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kuwashtaki washukiwa hao.

Mahakama hiyo iliendesha kikao mwaka uliopita kusikiliza upande wa mashtaka na pia upande wa utetezi kutathmini ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kuwashtaki.

Katika kesi ya kwanza, mawaziri wa zamani William Rutto , Henry Kosgey na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang wanatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, kuwahamisha watu kwa nguvu, na kuwatesa watu.

Uhalifu huo unadaiwa kutekelezwa dhidi ya wafuasi wa chama cha Rais Kibaki cha Party of National Unity (PNU), katika maeneo kadhaa mkoani Rift Valley.

Kwenye kesi ya pili, Bwana Kenyatta , mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na aliyekuwa mkuu wa Polisi Hussein Ali wanakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu , mkiwemo mauaji, kuwahamisha watu kwa nguvu, ubakaji na mateso.

Kiongozi wa mashtaka katika ICC Luis Moreno Ocampo anadai kwamba Kenyatta na wenzake walifadhili na kutekeleza mashambulizi dhidi ya wafuasi wa chama cha Orange Democratic Party,ODM, chake waziri mkuu Raila Odinga, katika maeneo ya Nakuru na Naivasha mkoani Rift Valley.

Watu wasiopungua 1,300 waliuwawa wakati wa ghasia hizo, na wengine zaidi ya 500,000 wakapoteza makazi.

Ghasia zilizuka baada ya Rais Kibaki kutangazwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali kati yake na Bwana Odinga.

Kufuatia ghasia hizo, jamii ya kimataifa iliwashinikiza Bwana Kibaki na Bwana Odinga kufanya mazungumzo ili kuzimaliza.

Mashauriano yaliyosimamiwa na katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Koffi Annan yaliishia kwa viongozi hao wawili kukubali kuunda serikali ya mseto, huku Bwana Kibaki akihifadhi kiti cha urais, naye Bwana Odinga akawa waziri mkuu

23 JAN. Manchester United yaikaribia Man.City


Manchester United imezidi kuipa shinikizo Manchester City iliyo kwenye kilele cha Ligi kuu ya England kufuatia mkwaju wa Danny Welbeck dakika chache kabla ya mechi kumalizika.

Mwanzoni mwa mechi hii United ilikua nyuma kwa pointi sita baada ya Manchester City kuirarua Tottenham hotspurs 3-2 kwenye uwanja wa Ettihad mapema siku ya jumapili.

Manchester United iliongoza kwa bao la Antonio Valencia dakika moja kabla ya kipenga cha mapumziko kuipa klabu yake bao 1-0. Bao hilo lilifutwa na la nahodha wa Arsenal katika kipindi cha pili na kuonekana kama liliowaamsha wachezaji wa Arsenal.

Mabadiliko yaliyofanywa na pande hizi mbili hayakuonekana kubadili mchezo ingawa wadadisi wengi wanajiuliza sababu iliyomfanya Arsene Wenge kumuondoa mchezaji wake aliyeonyesha mchezo mzuri Alex Oxlade-Chamberlain.

Licha ya juhudi na kuonyesha matumaini ya kuongezea mabao kwa Arsenal Manchester United ikitumia uzowefu wake na kuzingatia mpango wake waliokuja nao waliendelea kuizuia Arsenal isifurukute na kama ilivyo tabia yao ya kukamilisha tamaa yao dakika za mwisho,zikisalia dakika tisa kabla ya kumalizika kwa mechi Danny Welbeck akatikisa nyavu za Arsenal na kuipatia ushindi na pointi tatu. Arsenal 1 Manchester United 2.

.

23 JAN. Man.city yazipi kupaa


Kwa mara nyingine mshambuliaji Mario Balotelli alijitokeza kua kiini cha mgogoro na sababu ya kuipatia Manchester city ushindi ikipiga hatua dhidi ya mshindani wake wa karibu Manchester United

Balotelli aliingia wakati Manchester City ikisukumwa na Tottenham 2-2 baada ya kurudisha mabao mawili katika kipindi kifupi ikionekana kuondoka na angalau pointi moja.

Wakati ikionekana kua Manchester City imepungukiwa na maarifa Bario Balotelli aliangushwa ndani ya eneo la hatari na beki Ledley King na mshambuliaji huyo kufunga bao la City na kuiweka Spurs nyuma ya viongozi wa Ligi kwa tofauti ya pointi nane.

Habari kubwa kutoka mchuano huo hata hivyo haukua ushindi wa City bali gumzo lilizunguuka jinsi Balotelli alivyomkanyaga kichwani Scott Parker.

Harry Redknap aliwambia wandishi habari kua alishangazwa na jinsi refa alivyoshindwa kuliona kosa la Balotelli akimkanyaga Parker makusudi. Hivyo, Balotelli akaongezea umaarufu wake kwa mashabiki wa klabu yake wanaompenda licha ya wengi kuhusu ni juha katika soka ya England.

Sunday, January 22, 2012

22 JAN.ITAZAME MAMBO IKO PALE

22 JAN. Yanga yabanwa


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana walishindwa kukwea kileleni mwa
msimamo wa ligi hiyo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Moro United katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga ilihitaji ushindi ili kufikisha pointi 30 na kukaa kileleni ikisubiri matokeo ya vinara wa ligi hiyo Simba yenye pointi 28 ambao leo watashuka kwenye uwanja huo kumenyana na Coastal Union.

Matokeo hayo yameifanya Yanga ifikishe pointi 28. Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza jana kupitia kwa Kenneth Asamoah aliyefunga katika dakika ya 43 baada ya kuunganisha krosi safi ya Haruna Niyonzima kutoka wingi ya kushoto.

Bao hilo liliingia dakika moja baada ya beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Benedict Ngassa wa Moro United.

Moro United ilipata bao la kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Ngassa aliyefunga bao hilo kwa kichwa baada ya kuunganisha pasi ya Erick Mawala.

Dakika mbili baadae Davis Mwape aliikosesha Yanga bao baada ya kupiga mpira pembeni huku akiwa peke yake na kipa wa Moro, Jackson Chove.

Baada ya kupata bao la kusawazisha, Moro walibadilika na kulishambulia lango la Yanga
mithili ya nyuki.

Moro ilipata bao la pili katika dakika ya 74 lililofungwa na Simon Suya baada ya kutumia vema makosa yaliyofanywa na beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'.

Yanga ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 79 kupitia kwa Kiiza aliyefunga kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi Hashim Abdallah baada ya Salum Kanoni kunawa mpira eneo la hatari.

Katika mechi nyingine iliyochezwa jana, Mtibwa Sugar ilishindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani Manungu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa JKT Oljoro.

Ligi hiyo inaendelea tena leo ambapo mbali na Simba itakayoikaribisha Coastal kwenye Uwanja wa Taifa, Azam itakuwa kwenye uwanja wake Chamazi ikimenyana na African Lyon .

22 JAN. Fulham yaizima Newcastle


Clint Dempsey alipata 'hat-trick', magoli matatu katika mechi moja, wakati alipoiwezesha Fulham kuizaba Newcastle magoli 5-2.

Fulham, ikichezea uwanja wa nyumbani wa Craven Cottage, ilikuwa imefungwa bao la kwanza na Danny Guthrie, kabla ya Danny Murphy kutumia nafasi ya mkwaju wa penalti kusawazisha na kuipatia Fulham fursa ya kuzinduka na kuanza kufunga magoli.

Kisha Dempsey alifunga bao lake la kwanza, na kufululiza wavuni la pili, kabla ya mwenzake Bobby Zamora kufunga lingine la mkwaju wa penalti, na ikawa ni 4-1.

Bao la Hatem Ben Arfa liliwapa matumaini Newcastle kwa muda mfupi, kabla ya Dempsey kufunga bao la tano na kuwavunja moyo kabisa.

Mabao mawili ya Robbie Keane, mchezaji wa Aston Villa, yaliwaangamiza Wolves, ambao wamo katika hatari ya kuondolewa katika ligi kuu ya Premier.

Darren Bent alipewa nafasi ya kupiga penalti baada ya kuchezewa vibaya, na pasipo kusita, aliiwezesha Villa kutangulia, kabla ya Michael Kightly kusawazisha.

Wolves walipata kwa muda nafasi ya kuongoza baada ya Roger Johnson kuusindikiza mpira wa kona, na David Edwards kufunga kwa kichwa, akimwacha kipa Shay Given akiduwaa.

Lakini hatimaye mkwaju wa Keane katika kipindi cha pili ukayafanya matokeo kuwa 2-2.

Karl Henry alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Marc Albrighton, na kufuatia tukio hilo, Keane akauelekeza mkwaju hadi wavuni kuandikisha bao la tatu, na Villa kushinda 3-2.

Katika mechi nyingine, Everton na Blackburn waliondoka na sare ya 1-1.

Tim Cahill alipata bao la kwanza, na la utata, kwa kufunga baada ya Maroune Fellaini kuuweka mpira sawasawa kwa kutumia mkono, jambo ambalo lilimpita mwamuzi.

Blackburn Rovers walisawazisha kupitia mchezaji David Goodwillie.

Chelsea waliendelea kusononeka, baada ya kutofungana na Norwich, na mshambulizi wa Chelsea, Fernando Torres, akicheza mchezo wake wa 17 pasipo kufunga goli.

Magali ya Heidar Helguson, Akos Buzsaky na Tommy Smith yaliinyanyua QPR kutoka hatari ya kushuka daraja, na sasa wakiiacha Wigan ikiendelea kukandamizwa katika nafasi ya mwisho ya ligi kuu ya Premier.

QPR iliishinda Wigan magoli 3-1.

Stoke nayo ilifungwa na West Brom magoli 2-1, huu ukiwa ni ushindi wa kwanza wa West Brom mwaka 2012.

Sunderland iliweza kuishinda Swansea magoli 2-0, na timu hiyo chini ya meneja mpya Martin O'Neill kukomesha mchezo laini wa Swansea, ambayo ilikuwa imecheza mechi nne mfululizo pasipo kushindwa.

Mchezo wa mwisho Jumamosi ulikuwa ni kati ya Bolton na Liverpool, na ambao ulikwisha kwa ushindi wa Bolton magoli 3-1.

Mechi inayozungumzwa sasa ni ya Jumapili, kati ya Arsenal na Manchester United.

Saturday, January 21, 2012

21 JAN.RATIBA YA MECHI ZA EPL WIKIEND HII


LEO

NORWICH CITY VS CHELSEA SAA 9.45 ALASIRI


EVERTON VS BLACKBURN SAA 12.00 JION


FULHAM VS NEWCASTLE UNITED SAA 12.00 JION


QPL VS WIGAN ATHLETICS SAA 12.00 JION


STOKE CITY VS WEST BROM SAA 12.00 JIONI


SUNDERLAND VS SWANSEA CITY SAA 12.00 JIONI


WOLVES VS ASTON VILA SAA 12.00 JIONI


BOLTON VS LIVERPOL SAA 2.30 JIONI


KESHO



MAN CITY VS TOTTENHAM SAA 10.30 JIONI

21 JAN. Ghana, Demba Ba matawi Afcon 2012


WAKATI LEO michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2012, inaanza kutimua vumbi katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon, timu ya Taiga ya Ghana inapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo.

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wasomaji wa mtandao wa goal.com, Senegal imetajwa kushika nafasi ya pili, huku Ivory Coast ikitwaa nafasi ya tatu.

Kura hizo zinaonesha kwamba, mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayechezea klabu ya Newcastle inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Demba Ba, ataibuka Mfungaji Bora.

Kiungo Andre Ayew wa Ghana ambaye ni mtoto wa gwiji, Abedi Pele, ametajwa kuwa ndiye atakayeibuka mchezaji bora chipukizi wa michuano hiyo.

Ghana mwaka 2010 ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na Misri bao 1-0 katika fainali, michuano ikiwa imefanyika nchini Angola.

Michuano hiyo inashirikisha timu 16, huku timu za kundi A na B zikiwa kwenye miji ya Guinea ya Ikweta, Malabo na Bata, wakati miji ya Gabon ya Libreville na France Vile itakuwa na timu za kundi C na D.

Timu zinazoshiriki michuano hiyo ni Guinea ya Ikweta, Libya, Senegal, Zambia, Ivory Coast, Sudan, Burkina Faso, Angola, Gabon, Niger, Morocco, Tunisia, Ghana, Botswana, Mali na Guinea. Michuano hiyo itafikia tamati Februari 21 mwaka huu.