tuwasiliane

Saturday, June 2, 2012

02 JUN.Luis Moreno agombea nafasi FIFA


Mwanasheria mkuu wa Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza kesi za makosa ya jinai, Luis Moreno Ocampo ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Mkuu wa kundi la upelelezi kwenye makao makuu ya FIFA.

Msemaji wa mwenyekiti wa Kamati ya utawala huru ya FIFA, Mark Pieth, amethibitisha habari kua raia huyo wa Argentina ni miongoni mwa wagombea wa nafasi hio, ikiwa ni sehemu ya wimbi la mageuzi yenye lengo la kukabiliana na rushwa pamoja na ufisadi.

Pieth, ambaye ana sifa ya kua mtaalamu wa masuala ya utawala, ndiye anayewajibika na kuwazsilisha orodha ya wagombea wanaostahili kwa kamati kuu ya FIFA.

Wanachama wa Shirikisho walikubaliana kwa kura mjini Budapest wiki iliyopita kuunda tume ya nidhamu, pamoja na uchunguzi wa kina na pia afisi ya maamuzi.

Watakashinda nafasi hizo watatangazwa tarehe 29 Juni.
Mageuzi haya yalipendekezwa baada ya madai upendeleo na rushwa kutumika katika kupanga mashindano ya Kombe la dunia la mwaka 2022 katika Taifa la Ghuba la Qatar.

02 JUN.Mubarak ahukumiwa kifungo cha maisha


Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama mjini Cairo.
Mubarak akipelekwa mahakamani kwa machera mwezi uliyopita
Alikutikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia zilizopelekea yeye kutolewa madarakani mwaka jana.

Hakimu Ahmed Refaat alisema watu wa Misri walivumilia miaka 30 ya dhiki chini ya utawala wa Bwana Mubarak, lakini kesi ilikuwa ya haki.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa zamani, Habib Al Adly, naye piya amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji.

Baada ya hukumu kutolewa kulizuka mtafaruku mahakamani wakati makundi yanayopingana yalipoanza kupigana.

02 JUN.Wafungwa wauana kwa visu Mwanza!


Jeshi la Magereza, limeingia katika kashfa nzito baada ya nyapara mkuu wa wafungwa katika Gereza la Butimba mkoani hMwanzaapa kuuawa kwa kuchomwa visu na wafungwa wenzake juzi mchana.

Nyampara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kishiwa, aliuawa chumbani kwake wakati akila chakula cha mchana, baada ya wafungwa wenzake kumfuata na kufunga mlango, kisha kumkaba na kumchoma visu sita shingoni, ubavuni na kifuani.

Imedaiwa kuwa wafungwa wengine walishuhudia watuhumiwa hao wakiingia ndani mwake, kabla ya kusikia tafrani kubwa iliyowafanya wavamie chumba hicho na kukuta mkuu wao kauawa.

Watuhumiwa hao walishambuliwa vibaya kwa kipigo na wafungwa wenzao pamoja na baadhi ya askari magereza kiasi cha kulazimika kupelekwa hospitali kupata matibabu.

Habari za kina kutoka ndani ya gereza hilo zilisema chanzo cha mauaji hayo ni hali ya kutoelewana baina ya wafungwa wanaotumikia vifungo virefu.

Hata hivyo, kuna madai kwamba mauaji hayo yamechangiwa na uzembe wa uongozi wa gereza hilo wa kushindwa kuyafanyia kazi malalamiko ya siku nyingi ya wafungwa, yakiwemo ya ukatili.

Baadhi ya askari magereza ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walisema kwa muda mrefu wafungwa wamekuwa wakimtuhumu nyapara huyo kuwa ana uongozi wa kibabe ambao unakumbatiwa na viongozi wakuu wa gereza.

“Nyapara huyo alikuwa ni kama mkuu wa gereza, chochote ambacho alikuwa akisema ndicho kilichokuwa kikifuatwa na uongozi wa gereza,” alisema askari mwingine.

02 JUN.KIKOSI CHA STARS LEO DHIDI YA IVORY COAST



1. Juma Kaseja

2. Shomari Kapombe

3. Amir Maftah

4. Kevin Yondani

5. Aggrey Morris

6. Shabani Nditi

7. Salum Abubakari

8. Frank Domayo

9. Mwinyi Kazimoto

10. Mbwana Samata

11. Mrisho Ngasa

02 MAY.CCM waanza kumkaanga Maige

[Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige] VIKAO VYAANZA KUJADILI KAULI ZAKE, WENZAKE WANNE NAO KUJADILIWA KWA KUUNGA MKONO PINDA ANG’OLEWE
Waandishi Wetu SIASA za minyukano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi na sasa wabunge wanne wa chama hicho wanatajwa kuwa wamekalia kuti kavu kutokana na kuanza kujadiliwa na vikao mbalimbali kwa matendo yao yanayoonekana kukiudhi chama hicho tawala.

Miongoni mwao ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ambaye tangu alipong’olewa katika nafasi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete Mei 4, mwaka huu amekuwa akitoa shutuma nzito dhidi ya CCM na baadhi ya makada wake.

Tayari chama hicho kimeonyesha kutoridhika na kauli hizo za Maige baada ya juzi Katibu wa Siasa na Uenezi wilaya ya Kahama, Mirco Ng'wanangolelwa kutoa taarifa ya kukanusha kauli zake dhidi ya chama na viongozi. "Tunakemea na kulaani utaratibu huu wa watu kukurupuka na kushutumu viongozi wa chama chetu kwa staili aliyotumia Maige. Lengo lake sio jema na wala halina nia ya kujenga chama chetu bali ni kubomoa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Tangu atimuliwe uwaziri, Maige amekuwa akitoa shutuma nzito kuhusu kufukuzwa kakwe kwamba kulitokana na majungu na fitina za wana CCM wenzake na kwamba kwa mtindo huo chama hicho kiko hatarini kufa. Pia mbunge huyo alimshambulia Katibu wa Itikadi na Uenenzi wa CCM, Nape Nnauye kwamba amekuwa akikiharibu chama hicho kutokana na kauli zake ambazo alisema zinakiua chama badala ya kukijenga, kauli ambayo hata hivyo ilikemewa na CCM Kahama.

Wengine ambao Maige amewashambulia hadharani ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, James Lembeli kwamba wanahusika na kusherehekea kung’olewa kwake.

Habari ambazo Mwananchi limezipata kutoka Kahama na Shinyanga Mjini, zinasema Maige ambaye pia ni Mbunge wa Msalala atajadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ambacho kimepangwa kufanyika Jumanne ijayo wilayani humo. Habari zaidi zinasema kikao hicho ni cha dharura na ajenda zake bado ni siri ya Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Adam Ndalahwa ambaye ametoa maelekezo kiitishwe. Ng'wanangolelwa alithibitisha kuitishwa kwa kikao hicho lakini hakuwa tayari kuzungumzia ajenda kwa maelezo kwamba anayezifahamu ni Ndalahwa. Kuhusu suala la Maige kujadiliwa Ng'wanangolelwa alisema: “Hilo kwa kweli sifahamu maana sisi kama chama wilaya tumepokea maelekezo kwamba Katibu wa CCM wa Mkoa atafika kuzungumza na Kamati ya Siasa, kwa hiyo kama hiyo ajenda ipo au haipo mimi sifahamu”.
Kwa upande wake Ndalahwa alikiri kutaka kukutana na Kamati ya Siasa ya Wilaya lakini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kichama wilayani humo, lakini akakanusha kuwapo kwa ajenda ya kumjadili Maige.

“Mimi ni Katibu wa CCM wa Mkoa, na nimepanga kwenda kwenye ziara ya kufuatilia chaguzi zetu ndani ya chama, tena nilipanga ratiba hii hata kabla ya Maige hajaanza ziara kwenye jimbo lake,”alisema Ndalahwa.

Sakata la Maige ni dhahiri sasa linachukua sura ya siasa za makundi ndani ya CCM kwani kauli ambazo zinafanya ajadiliwe amekuwa akizitoa kwenye mikutano ambayo imekuwa ikihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.

Waliotaka Pinda ang’olewe Wakati hayo yakiendelea, wabunge wengine watatu wa CCM ambao walisaini kusudio la kumng’oa madarakani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nao huenda wakajadiliwa kutokana na hatua yao hiyo. Wabunge hao Deo Filikunjombe (Ludewa), Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) na Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara) walisaini hoja yenye kusudio la kutaka kumng’oa Waziri Mkuu, Pinda ambalo lilikuwa likitaka kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Habari zinasema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yaliwagawa wajumbe wa kikao cha Halmshauri Kuu ya CCM (Nec) kilichofanyika mwezi uliopita mjini Dodoma, lakini hakuna mwafaka wowote uliopatikana. “Wapo ambao tulitaka hawa wabunge wachukuliwe hatua za kinidhamu, lakini pia wapo ambao walikuwa na msimamo kwamba wabunge hao walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba, mjadala ulikuwa mkali lakini hitimisho lilikuwa kwamba suala hilo lirejeshwe kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM,”alisema mmoja wa wajumbe wa NEC.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alithibitisha suala hilo kijadiliwa ndani ya kikao hicho na kwamba ni kweli limerejeshwa katika kamati ya wabunge wa chama hicho. “Kimsingi hoja zote zinaanzia pale bungeni, na hata hayo ambayo yanadaiwa kuwa ni makosa yalifanyika katika mazingira ya Bunge, sasa kama chama tuliona ni vyema tuiachie kamati ya wabunge wetu, nao wataangalia kwa kutumia kanuni zao kama wataona kuna kosa, basi watachukua hatua,”alisema Nape na kuongeza: “...wanatakiwa watumie kanuni zao sasa inategemea zinawaelekeza vipi, kama wanaweza kutoa adhabu sawa, kama wanalifoward (wanalileta) kwetu nasi tutalipangia utaratibu mwafaka, lakini lazima lianzie huko kwa wabunge wenyewe, sisi hatuwezi kuwaingilia”. Katibu wa Wabunge wa CCM, Janester Mhagama kwa upande wake, alisema alikuwa hajapata taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa NEC na kwamba baada ya kuarifiwa, angeweza kulizungumzia.

“Kwa bahati mbaya katika NEC iliyopita sikuweza kuhudhuria nilikuwa na matatizo ya kifamilia, lakini niseme tu kwamba kama watatuletea kama walivyosema, basi kanuni zetu zipo na tutaangalia zinasemaje kuhusu hilo,”alisema Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho. Mhagama ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa Bunge aliweka wazi kwamba anachofahamu yeye ni kwamba wabunge hao walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba lakini akakumbusha kuwa chama nacho kina nafasi yake.

Aliongeza: “Ndiyo maana nimesema lazima twende kwenye kanuni zetu za Bunge halafu pia tuangalie kanuni zetu za wabunge wa CCM, tutapata mwafaka hakuna haja ya kuwa na haraka”. Akizungumzia suala hilo, Filikunjombe alisema kuwa aliyoyazungumza bungeni ikiwa ni pamoja na kusaini fomu ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni kwa maslahi ya Serikali na CCM.

“Ukweli ni kwamba nilichokizungumza sikumsingizia mtu na nilifanya hivyo kwa maslahi ya Serikali yangu na chama change,” alisema Filikunjombe. Alifafanua kwamba wanaomuona adui na kutaka achukuliwe hatua na chama, wao ndio maadui namba moja wa Serikali na CCM.

“Rais Jakaya Kikwete mwenyewe aliwahi kukiri wazi kuwa amefurahishwa na mawazo ya wabunge waliyoyatoa kuhusu suala zima la kuwajibishwa kwa mawaziri”. Aliongeza, “Unajua watu wanadhani kwamba wenye uchungu na nchi hii ni wapinzani pekee…,hilo jambo sio kweli nchi hii ni yetu wote”. Mwisho………………….
SOURCE. WWW.MWANANCHI.CO.TZ

Friday, June 1, 2012

01 JUN.Rodgers ahadi makubwa Liverpool


Meneja mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers, ameahidi atafanya juhudi za "kufa kupona" katika kuiletea ubingwa klabu hiyo ya uwanja wa Anfield.

Rodgers, mwenye umri wa miaka 39, alithibitishwa kama mrithi wa Kenny Dalglish baada ya klabu yake ya Swansea kukubali kuchukua senti za fidia katika kumpoteza meneja huyo.

"Ninatoa ahadi za kupambana kufa kupona maishani kwa niaba ya watu wa mji huu," alielezea raia huyo wa Ireland ya Kaskazini.

"Pengine sasa hivi hatujajiandaa kwa ubingwa, lakini utaratibu wa kufanya hivyo unaanza leo."

Inafahamika Swansea wamekubali kitita cha pauni milioni 7 kumruhusu Rodgers kuondoka, na vile vile wasaidizi wake kocha Colin Pascoe, Chris Davies anayehusika na ubora wa mchezo, na Glen Driscoll, mshauri wa klabu kuhusiana na ubora wa mchezo, na waliopata mkataba wa miaka mitatu.

Liverpool wametwaa ubingwa wa ligi mara 18 katika historia yao, na mara ya mwisho walipata ubingwa msimu wa 1989-90.

"Huu ni muda mrefu uliopita na ndio maana kazi hii ni kivutio," alielezea kocha huyo wa zamani wa timu za Watford na Reading vilevile.

"Kilichonivutia mimi ni historia ya klabu na mashaka iliyoyapata. Ni miaka 20 sasa tangu walipopata ubingwa."

"Hii ni klabu ambayo ukipata ufanisi, basi utakuwa hapa kwa miaka mingi.

"Hii ndio sababu ya kufika hapa. Bila shaka yote yanahusiana na matokeo na ufanisi wa timu. Of course that is about results and the progress of the team.

"Ni fahari kubwa kwangu. Ninahisi nimebarikiwa kuipata nafasi hii kuisimamia klabu.".

Mashabiki wa Liverpool bado hawana uhakika kumpokea vipi Rodgers, lakini meneja huyo amesema ataweza kuwashawishi mashabiki wote wa uwanja wa Anfield kwamba ataweza kukimudu kibarua hicho.

"Natumaini baada ya muda wataweza kunikubali na kuniheshimu," alielezea.

"Ni klabu maalum. Nina hamu sana ya kuhamia na kuishi katika mji huu."

01 JUN.Simba waanza kujifua


SIMBA imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Bara huku klabu za Yanga na Azam FC zikiwa bado hazijaanza.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu walianza mazoezi yao juzi hasa wakijiandaa na mashindano ya Kagame yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa sita jijini Dar es Salaam.

Simba wameanza kwa kufanya mazoezi GYM iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo kocha msaidizi wa Simba, Richard Amatre alisema wameanzia huko kwa ajili ya kujiimarisha kistamina zaidi.

"Tumeanza mazoezi tangu jana (juzi) kwa ajili ya maandalizi yetu na mazoezi yanaendelea vizuri,"alisema Amatre ambaye ndiye amebaki na kikosi hicho kwa sababu kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic yupo kwao Serbia kwa mapumziko.

"Tumeanza ratiba ya GYM kama ilivyo kawaida, wachezaji wengi walikuwa katika mapumziko baada ya kumaliza mashindano, tunafanya hivi kwa ajili ya kuistua miili yao,"alisema Amatre.

Aliongeza kuwa ratiba hiyo, itaendelea hadi hapo baadaye watakapohamia uwanjani.

Kati ya wachezaji waliokuwapo katika mazoezi hayo mmojawapo alikuwa, Paul Ngalema ambaye alisema,"maandalizi mazuri, kama hivi unavyoona tumeanzia GYM, haya ni mazoezi ambayo yatatuweka katika hali nzuri."

Alisema,"tumeanza vizuri kama unavyoona, naamini mambo yatakuwa mazuri hapo baadaye,"alisema Ngalema aliyesajiliwa kutoka Ruvu Shooting.

Hata hivyo bado baadhi ya wachezaji wa Simba hawajajiunga na mazoezi hayo kwa sababu wengine wapo katika vikosi vya timu zao za Taifa.

01 JUN.TERRY AONGEZEWA ADHABU NA UEFA


Mlinzi wa klabu ya Chelsea, John Terry, atazikosa mechi mbili msimu ujao utakapoanza wa mechi za Ulaya, kufuatia adhabu ya UEFA kumzuia asicheze katika mechi tatu.
John Terry

Aongezewa adhabu kwa kumpiga kwa goti mchezaji wa Barcelona

Tayari aliikosa fainali dhidi ya Bayern Munich, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali, wakati Chelsea ilipopambana na Barcelona.

Lakini UEFA sasa imeamua kumuongezea adhabu, kwa kumkataza kucheza katika mechi mbili zaidi.

Terry pia hatakuwepo katika mechi ya Kombe la Super dhidi ya washindi wa ligi ya Europa, Atletico Madrid ya Uhispania, itakayochezwa mwezi Agosti, na vile vile mechi ya kwanza ya Chelsea katika hatua ya makundi ya kufuzu kwa ligi ya klabu bingwa Ulaya.

Terry na Chelsea wana muda wa siku tatu kuamua ikiwa watakata rufaa au la kufuatia uamuzi huo.

Terry, mwenye umri wa miaka 31, alitolewa kadi nyekundu na mwamuzi, kufuatia kushindilia goti lake dhidi ya mchezaji wa Barca, Alexis Sanchez, pasipo hata mpira kuwa karibu, wakati Chelsea ilikuwa tayari imefungwa bao 1-0 usiku huo.

Aliwaomba msamaha wenzake kwa kuwaletea fedheha.

Hata hivyo licha ya kuondolewa Terry katika mechi hiyo, hatua hiyo haikuinyima Chelsea ushindi, kwani hatimaye iliondoka kwa sare ya 2-2, na katika uwanja wa Nou Camp, waliibuka washindi kwa jumla ya magoli 3-2.

Kisha baada ya hapo walipata ubingwa wao wa kwanza katika fainali ya klabu bingwa, licha ya kuwakosa wachezaji mahiri Terry, Ramires, Branislav Ivanovic na Raul Meireles.

01 JUN .Baada ya TOUR ndefu LINAH arejea!


Baada ya kukaa unyamwezini 'Marekani' kwa show zilizodumu takriban miezi 3, hatimaye mwanadada kifaa Linah Sanga amerejea Bongo.

Bila shaka amekuja na morali mpya na mashabiki wategemee mabadiliko ya mambo mengi kutoka kwa mwanadada huyu hasa kwenye video kwakuwa amekuja na swag za Marekani.

Peter Ligate CEO wa kampuni ya J&P Investiment Inc. iliyosababisha tour hiyo amesema, “After a successful "tamani" us tour the #1 female artist Linah is back in Tanzania. Thanks to all that supported her & continue to support our artist & bongo fleva..godspeed ma people!!”

01 JUN; EXCLUSIVE;Nsajigwa (fuso) amwagwa rasmi Yanga!


Klabu ya watoto wa Jangwani Dar Young Africans, imewatupia virago beki wake wa kulia na nahodha, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ na Abuu Ubwa, imefahamika.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es Salaam zinasema, nyota hao wameachwa kutokana na kushuka viwango.

Chanzo cha uhakika kimedokeza kuwa kushuka kwao kiwango kuliwafanya washindwe kutoa mchango uliotarajiwa kutoka kwao katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyofikia tamati Mei 6.

Yanga chini ya Kocha wake Mserbia, Kostadin Papic ilimaliza ligi hiyo kwa kushindwa kutetea ubingwa wake, ikimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.

Chanzo hicho kimedokeza kuwa, kuachwa kwa nyota hao, ni sehemu ya mkakati wa kukisuka upya kikosi cha timu hiyo kuelekea vita ya kutetea ubingwa wa Kombe la Kagame na msimu mpya wa Ligi Kuu.

Mbali ya kiwango, pia kiongozi huyo amedokeza kuwa, walikerwa na utovu wa nidhamu wa ndani na nje ya uwanja wa Nsajigwa aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, T