tuwasiliane

Saturday, June 2, 2012

02 JUN.Wafungwa wauana kwa visu Mwanza!


Jeshi la Magereza, limeingia katika kashfa nzito baada ya nyapara mkuu wa wafungwa katika Gereza la Butimba mkoani hMwanzaapa kuuawa kwa kuchomwa visu na wafungwa wenzake juzi mchana.

Nyampara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kishiwa, aliuawa chumbani kwake wakati akila chakula cha mchana, baada ya wafungwa wenzake kumfuata na kufunga mlango, kisha kumkaba na kumchoma visu sita shingoni, ubavuni na kifuani.

Imedaiwa kuwa wafungwa wengine walishuhudia watuhumiwa hao wakiingia ndani mwake, kabla ya kusikia tafrani kubwa iliyowafanya wavamie chumba hicho na kukuta mkuu wao kauawa.

Watuhumiwa hao walishambuliwa vibaya kwa kipigo na wafungwa wenzao pamoja na baadhi ya askari magereza kiasi cha kulazimika kupelekwa hospitali kupata matibabu.

Habari za kina kutoka ndani ya gereza hilo zilisema chanzo cha mauaji hayo ni hali ya kutoelewana baina ya wafungwa wanaotumikia vifungo virefu.

Hata hivyo, kuna madai kwamba mauaji hayo yamechangiwa na uzembe wa uongozi wa gereza hilo wa kushindwa kuyafanyia kazi malalamiko ya siku nyingi ya wafungwa, yakiwemo ya ukatili.

Baadhi ya askari magereza ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walisema kwa muda mrefu wafungwa wamekuwa wakimtuhumu nyapara huyo kuwa ana uongozi wa kibabe ambao unakumbatiwa na viongozi wakuu wa gereza.

“Nyapara huyo alikuwa ni kama mkuu wa gereza, chochote ambacho alikuwa akisema ndicho kilichokuwa kikifuatwa na uongozi wa gereza,” alisema askari mwingine.

No comments:

Post a Comment