Hatimaye klabu za Simba na Yanga zimeruhusiwa kuutumia uwanja wa Taifa, baada ya Serikali kuufungia tangu Oktoba 1, kutokana na vurugu za mashabiki wa timu hizo mbili.
Mkuu wa mawasiliano Zawadi Msella, amekiambia chanzo chetu, leo kwamba uwanja huo unafunguliwa baada ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kujiridhisha na ukarabati uliofanywa.
“Waziri Nape Nnauye amefanya ziara na kuridhika na ukarabati uliofanywa na kuziamuru klabu hizo mbili kuendelea kuutumia uwanja huo lakini kwa taratibu maalumu ambazo zinaweza kuufanya uendelee kuwa salama,”amesema Msalla.
Siku hiyo kulitokea vurugu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baina ya mahasimu, Simba na Yanga hadi kuvunja viti.
Mashabiki wa Simba walifanya vurugu uwanjani hapo kwa kuvunja viti na kuvitupa uwanjani kufuatia mwamuzi Martin Saanya kumtoa nje kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba Janos Mkude.
Utata ulianzia baada ya Amissi Tambwe kufunga bao la kuongoza kwa Yanga akitumia mkono kuupoza mpira kabla ya kufungwa kwa mguu na baadhi ya wachezaji wa Simba kumzonga mwamuzi huyo ndipo alipoamua kutoa kadi nyekundu kwa Mkude ingawa Simba walisawazisha bao hilo dakika za mwishoni.
Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Kichuya alipofunga bao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo huo kumalizika.
Oktoba 2, Wizari Nape akatangaza kuufungia uwanja huo usiweze kutumika kwa timu hizo mbili na kuzuia mapato yao hadi hapo garama za matengenezo zitakapo kamilika .
Lakini leo, ikiwa ni zaidi ya siku 100 tangu Uwanja ufungiwe, Serikali inarudi nyuma na kuzifungulia timu hizo pamoja na kutoa ruksa kwa mambo mengine yote ya kijamii kufanyika kwa baraka ya wizara hiyo na TFF wameamua kuuhamishia mchezo wa ligi ya Vodacom kati ya Simba na Azam uliokuwa upigwe uwanja wa Uhuru sasa utapigwa hapo
No comments:
Post a Comment