tuwasiliane

Friday, January 27, 2017

Mamelodi waja Dar kuvipima vigogo

mamelodi
Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mamelodi Sundowns wanatarajiwa kuja nchini wiki ijayo kucheza mechi za kirafiki na vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga.
Timu hio yenye wachezaji mahiri kama Mchezaji bora wa ndani ya Afrika, Denis Onyango na mshambuliaji, Khama Biliat inatarajiwa kuanza kucheza na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga katikati ya wiki kisha kuwavaa Simba.
Licha ya kuwa mechi hizo mbili zimeandaliwa kama sehemu ya kampeni ya kulinda tembo, Mamelodi Sundowns itazitumia kama sehemu ya maandalizi yake ya kuivaa TP Mazembe katika pambano la Super Cup lililopangwa kupigwa Februari 18 nchini JK Kongo.
Kwa upande wa Yanga, mechi hii itakuwa kipimo kizuri kuelekea mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo inatarajia kuanza kampeni kwa kuivaa Ngaya ya Comoro  mwezi ujao.
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Sundowns kucheza na Yanga. Mwaka 2001 Mamelodi Sundowns waliitoa Yanga katika Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga mabao 3-2 Afrika Kusini na kisha kulazimisha sare ya mabao 3-3 katika pambano la marudiano lililopigwa CCM Kirumba na kuweka historia ya mapato makubwa zaidi Tanzania iliyodumu hadi Uwanja wa Taifa ulipofunguliwa mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment