tuwasiliane

Saturday, January 28, 2017

JOHN BOCCO ATAMBA KUIKALISHA SIMBA,TAIFA LEO

John Bocco
Nahodha wa klabu ya Azam FC John Bocco, amesema mbinu za kocha wao mpya Mromania, Aristica Cioaba, zinampa matumaini ya kuifunga tena Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu, utakaopigwa leo  Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Bocco ameiambia www.heavytalio.blogspot.com,  kwa muda wa wiki moja waliyofanya mazoezi chini ya kocha huyo wameweza kujifunza mambo mengi ikiwemo mbinu muhimu  za kuwasaidia kupata ushindi katika mechi zao ikiwemo ule wa Jumamosi dhidi ya Simba.

“Mbinu za kocha Cioaba ukweli zimetufanya tuwe na matumaini makubwa ya kuifunga Simba na kufanya vizuri kwenye mechi nyingine za ligi na michuano ya kimataifa, kwasababu ametufundisha vile vitu muhimu ambavyo vipo kwenye wakati huu tuliopo naamini hata ubingwa tunaweza kuchukua,”amesema Bocco.

Mshambuliaji huyo alisema pamoja na mafunzo ya kocha lakini hata yeye mwenye angependa kuendeleza rekodi yake ya kuifunga Simba kama anavyofanya kwenye mechi zilizopita .
Bocco alisema msimu huu ameshaifunga Yanga kwenye kombe la  mapinduzi hivyo angependa kufanya hivyo na kwa Simba ili kuendelea kuimarisha rekodi yake ya kuzifunga timu hizo kongwe kwenye ligi ya Tanzania Bara.

Cioaba anatarajiwa kuiongoza Azam kwa mara ya kwanza tangu, alipo saini mkataba wa miezi sita kuifundisha timu hiyo akichukua mikoba ya Mhipania Zeben Hernandez mwishoni mwa mwaka jana.
Mshambuliaji huyo  mwenye rekodi ya pekee kwenye klabu hiyo ndiyo anashikilia rekodi ya kuzifunga timu hizo mbili ambapo kwa pamoja ameshazifunga mabao 43  hiyo ikiwa tangu Azam ilipoanza kushiriki Ligi Kuu miaka nane iliyopita.

No comments:

Post a Comment