tuwasiliane

Sunday, January 15, 2017

Sevilla inataka kumsajili kwa mkopo Rashford hadi mwisho wa msimu

Sevilla inataka kumsajili kwa mkopo Marcus Rashford hadi mwisho wa msimu
Klabu ya Sevilla inataka kumchukua nyota kinda wa Manchester UnitedMarcus Rashford kwenye ligi ya Hispania, La Liga kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kwa mujibu wa habari.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa ndani na nje ya kikosi cha Mshetani Wekundu msimu huu kufuatia maajabu aliyofanya msimu uliopita pale Old Traford.
Imedaiwa na The Sun kuwa Sevilla wanatamani sana kuwa na Rashford katika dimba la Ramon Sanchez Pizjuan kwa kipindi cha miezi minne ijayo, baada ya kumfuatilia kwa karibu sana tangu alipoibukia kwenye soka la Uingereza takribani miezi 12 iliyopita.
Bosi wa United Jose Mourinho amekuwa mzito kumruhusu nyota huyo kuondoka, ingawa, inaaminika kuwa West Ham United nao wanaitamani saini ya mchezaji huyo.
Hata hivyo, ripoti hizo zinadai kuwa wakali wa Europa League Sevilla wapo tayari kumpa muda Rashford ambaye ameanza mechi nane za ligi chini ya Mourinho – kusema neno la mwisho kuhusu mustakabali wake kwa kipindi kifupi cha msimu kilichobakia.

No comments:

Post a Comment