tuwasiliane

Sunday, January 15, 2017

Diego Costa awachwa nje baada ya mgogoro na kocha

Costa mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 14 na kusaidia kutengeza mabao 5 msimu huu
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa jana aliachwa nje katika kikosi cha Chelsea dhidi ya Leicester baada ya mgogoro na kocha kuhusu uzima wake.
Raia huyo wa Uhispania hajashiriki mazoezi kwa siku tatu na hajasafiri na viongozi hao wa ligi ili kushiriki mechi dhidi ya bingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Leicester.
Habari hizo zinajiri huku kukiwa na ripoti kwamba anashirikishwa na uhamisho nchini China wenye thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka.
Costa mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 14 na kusaidia kutengeza mabao 5 msimu huu.
Chelsea hatahivyo imekataa kutoa tamko lolote.
Inaeleweka kwamba mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich hataki kumwachilia katika kandarasi yake inayokamilika 2019, na hafurahii mpango wa kushinikizwa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment