tuwasiliane

Friday, January 27, 2017

Juuko atakiwa na miamba wa Scotland

Juuko Murushid
Mlinzi wa kati wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Murushid Juuko anatajwa kuwavutia vigogo wa soka nchini Scotland, Celtic.
Wakala wa Juuko, Ronnie Mwine Santos amenukuliwa na mtandao wa Soka25East akielezea timu mbalimbali zilizoonesha kuvutiwa na Juuko ikiwemo miamba hao ambao ni mabingwa mfululizo wa Ligi Kuu Scotland.
” Celtic wamemtazama Juuko akiwa timu ya taifa na kuvutia naye kwa hio tunawasiliana nao. Watatuma maskauti wao katika pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Februari 25.” Amenukuliwa Santos.
Wakala huyo raia wa Uganda ameongezea kuwa, anatambua Juuko bado ana mkataba na Simba hivyo anazungumza na uongozi wa klabu kujadili ofa mbalimbali kutoka Misri, Afrika Kusini na Uturiki zilizo mezani kwa sasa. ”Juuko alijiunga na Simba akitokea klabu ya nchini kwao, SC University na ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara aliyecheza mechi za fainali za AFCON 2017 nchini Gabon.

No comments:

Post a Comment