tuwasiliane

Monday, December 26, 2016

Wenger: Ozil atawashangaza wakosoaji wake

Sanchez kushoto na Ozil Kulia
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil atawashangaza wakosoaji wake katika mechi inayofuata.
Ozil alikosolewa vibaya baada ya Arsenal kushindwa 2-1 na Manchester City .
Lakini Wenger amesema kuwa Ozil kama wachezaji wengine shupavu katika timu yake amekuwa akichukua jukumu kubwa na hivyobasi hapaswi kulaumiwa sana.
Anasema kwamba tatizo la Arsenal kupoteza mechi hiyo ilikuwa kushindwa kudhibiti mchezo katikatika ya uwanja.
Wenger: Wachezaji kama Ozil wanapokosolewa wao hujibu kwa kucheza vizuri katika uwanja katika mechi inayofuata.

No comments:

Post a Comment