tuwasiliane

Sunday, December 25, 2016

Shime asema JKT Ruvu itawashanga Watu

Image result for bakari shime
Kocha wa JKT Ruvu  Bakari Shime, amemtupia lawama mwamuzi Hans Mabena, kwa kukubali bao la Simba katika mchezo wa ligi ya Vodacom uliopigwa jana Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Shime ameiambia chanzo chetu kuwa, mwamuzi huyo ndiyo aliyechangia wao kupoteza mchezo huo na kushuka hadi nafasi ya mwisho kwenye msimamo wakisaliwa na pointi zao 13, walizozipata kwenye mzunguko wa pili

“Wachezaji wangu walicheza vizuri kwa muda wote wa mchezo lakini mwamuzi hakututendea haki kwa kukubali bao ambalo siyo halali kwani kipa wetu alichezewa madhambi, mapema nay eye akaacha mchezo uendelee,” amesema Shime.
Kocha huyo amesema kama kocha ameyapokea masikitiko matokeo hayo kwakuwa walijipanga kupata ushindi katika mchezo huo, lakini imekuwa tofauti na kile ambacho walikitarajia baada ya dakika 90.

Amesema baada ya kupoteza mchezo huo wanajipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata akiamini wanaweza kupata matokeo kutokana na ubora wa kikosi chake na kiwango walichokionyesha katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Simba na Yanga
Amesema pamoja na kikosi chake kuburuza mkia lakini anauhakika hawatoshuka daraja kwani  anauhakika wa kupata ushindi katika mechi zinazofuata ambazo amezipa umuhimu mkubwa kwa kuzingatia nafasi waliyopo.
“Sina hofu kwasababu bado tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu na kuondoka kwenye nafasi mbaya tuliyopo hivisasa , imani yangu JKT Ruvu itamaliza msimu huu kwenye nafasi za juu  na kuwashangaza watu, “amesema  kocha  huyo.
Shime ameichukua timu hiyo kwenye mzunguko wa pili, akiziba nafasi ya Malale Hamsini ambaye amekwenda Ruvu Shooting, ambayo ilikuwa ikifundishwa na kocha msaidizi baada ya kuondoka kwa Tom Olaba.

No comments:

Post a Comment