tuwasiliane

Sunday, December 25, 2016

Lwandamina: "hatuwezi kuwadharau Ngaya de Mbe"

Lwandamina: "hatuwezi kuwadharau Ngaya de Mbe"
Klabu ya Yanga imepangwa kuanza na timu ya Ngaya de Mbe ya Comoro, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika ratiba iliyotolewa jana na Shirikisho la soka Afrika CAF.
Ratiba hiyo inaonyesha Yanga wataanzia ugenini Comoro mechi ikichezwa kati ya Februari 10 au 12 na mechi ya ya marudiano itachezwa 17 na 19 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa upande wao Azam ambao wanashiriki watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wao wamepangwa kuanza michuano hiyo raundi ya kwanza kati ya mshindi wa mechi dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.

Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.
Ratiba hiyo inaonyesha kama Yanga watafanikiwa kuvuka kwa Wacomoro, watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza.

Katika hatua hiyo Yanga wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.
Baada ya kutoka kwa ratiba hiyo kocha wa Yanga George Lwandamina, amesema amefuraishwa na Caf, kwa kutoa mapema ratiba hiyo kwani imemsaidi kuwajua wapinzani wake mapema na kukiandaa vyema kikosi chake ili kuweza kupambana nao

Mzambia huyo amesema anajua watu wengi wanaipa nafasi Yanga lakini hawawezi kupata matokeo mazuri kama hakutakuwa na maandalizi mazuri yanayolingana na ugumu wa mashindano yenyewe hivyo nilazima watumie muda uliopo kujiandaa vizuri ili waweze kufika mbali kama walivyokusudia.
“Soka la Afrika, limekuwa likipiga hatua siku hadi siku hivyo hatuwezi kuwadharau Ngaya de Mbe, kwa sababu wao ndiyo mambingwa wa taifa hilo ndiyo maana wamepangwa kwenye ratiba na wao watacheza kama wanavyocheza na timu nyingine ili kuhakikisha wanapata matokeo,”amesema Lwandamina.

Kocha huyo amesema kama watakosa muda wa kupiga kambi ya kujiandaa na michuano hiyo atahakikisha anatumia mechi za ligi kuu ya Vodacom, kama mazoezi ili kujiimarisha kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika.
Katika miaka ya hivi karibuni Yanga imekuwa ikipata bahati ya kupangwa na timu za Comoro kwenye michuano ya kimataifa na imekuwa ikifanya vizuri kwa kushinda na kuzitupa nje timu hizo ambazo zimeonekana kuwa dhaifu mbele ya mabingw hao mara 26, wa Ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment