tuwasiliane

Friday, December 2, 2016

Taasisi ya Drogba yafutiliwa makosa ya ufisadi

Didier Drogba
Uchunguzi dhidi ya shirika la kutoa msaada la mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, haujapata ushahidi wa ufisadi au ulaghai,lakini umebaini shirika hilo ''liliwapotosha'' wafadhili.
Tume ya taasisi hiyo ya ufadhili iliyoanza uchuguzi wa madai ''makali ya udhibiti''katika shirika lake la Didier Drogba mwezi April.
Baadaye gazeti la Daily Mail liliripoti kwamba kati ya pauni milioni 1.7 za hisani ni pauni elfu 14,115 ndizo pesa pekee zilizotumika kusaidia barani Afrika.
Drogba , 38, amesema anataka kulipwa na kuombwa msamaha na gazeti hilo la Daily Mail.
Kamati hiyo iliyotumia mamlaka yake ili kuchunguza akaunti za shirika hilo, imesema imeridhika kwamba hakuna udanganyifu wowote.
Lakini ilikuwa vigumu kubaini ukweli kuhusu taasisi hiyo, ilivyogawanya mipango yake binafsi ya ili ya kutoa msaada Afrika.
Hilo nidhihirisho kamili kwa ufadili uliokuwa ukitoka Uingereza haukuwa unatumika kwa mahospitali au kwa makliniki, kama vile wafadhili walivyodhani, lakini pesa hizo zilikuwa zikiwekezwa kwenye akaunti za Uingereza.
''Wafadili walitarajia ufadhili wao ungetumika kwa madhumuni ya usaidizi, na sikuekeza kwenye akaunti za benki,''ripoti hiyo ilisema.
Wafadhili wa Uingereza labda yalidanganywa kuhusu miradi ya shirika hilo ambalo wamekuwa wakilifadhili.
Kamati hiyo imetoa ''mpango tekelezi'' kwa shirika la Didier Drogba kujiimarisha.

No comments:

Post a Comment