tuwasiliane

Thursday, December 15, 2016

Oscar: Kiungo wa Chelsea kuhamia China

Oscar
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amesema ana "uhakika 90% " kwamba atahamia klabu ya Shanghai SIPG inayocheza Ligi Kuu ya China kipindi cha kuhama wachezaji Januari.
Inakadiriwa kwamba mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 atanunuliwa takriban £60m.
Alijiunga na Chelsea kutoka Internacional kwa £25m mwaka 2012.
Oscar alianza kwenye mechi tano za kwanza chini ya Antonio Conte lakini amechezeshwa mara nne pekee tangu Septemba.
"Inategemea mambo kadha tu ya urasmi," Oscar aliambia Sportv ya Brazil.Conte hakukanusha madai ya Oscar alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake baada ya ushindi wa Chelsea wa 1-0 dhidi ya Sunderland Jumatano.
Amesema hali ya Oscar itakuwa wazi zaidi siku chache zijazo.
Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai.
Oscar amechezea Chelsea mechi 202 na kufunga mabao 38.
Ameshinda Ligi ya Premia, Europa League na Kombe la Ligi.

No comments:

Post a Comment