tuwasiliane

Thursday, December 15, 2016

USAJILI WA SIMBA DIRISHA DOGO HUU HAPA

img_0240
Klabu ya Simba inapenda kutangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog.
Kwenye maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu
Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, pamoja na Emmanue Semwanza atakaekwenda Maji Maji fc ya Songea,
Huku pia klabu ikiachana rasmi na golikipa muaivory coast Vicent Angban na kiungo Mcongo, Mussa Ndusha.
Sambamba na kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, huku tukikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Liuzio anayekuja kwa mkopo toka Zesco United ya Zambia.
Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Alli kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta kwetu kwa mkopo.
Tunaamini maboresho haya yataongeza chachu ya ushindani katika kikosi chetu na Hatimaye kutupa mataji msimu huu.
Niwaarifu pia timu yetu imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda Fc, mchezo utakaopigwa siku ya jumapili ya tarehe 18/12/2016 huko Mtwara.
Imetolewa na ;
Haji S. Manara
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sc

No comments:

Post a Comment