tuwasiliane

Thursday, December 15, 2016

KUFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO;HOOD MAYANJA,TITO OKELLO NA MRISHO NGASA WATUA MBEYA CITY

Titto Okello
Kocha Kinnah Phiri  wa Mbeya City ameamua kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kuwachukua nyota
wawili wa African Lyon, Hood Mayanja na Tito Okello.
Washambuliaji hao raia wa Uganda, walikuwa wachezaji muhimu katika kikosi cha African Lyon toka ikiwa Ligi Daraja la Kwanza.
Mbeya City inashikilia nafasi ya nane ikiwa na tatizo la ufungaji wa mabao baada ya kufunga mabao 13 tu katika mechi 15 ilizocheza msimu huu.Wakati huo huo leo mchezaji Mrisho Ngassa    leo ametangazwa rasmi mchezaji halali wa Mbeya Cityna kuungana na kocha wake Kinnah Phiri aliyefanya naye kazi wakiwa Free State ya Afrika Kusini.
Ngassa

No comments:

Post a Comment