Baada ya tetesi za muda mrefu kwamba Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Cannavarro ana hati hati ya kutemwa katika dirisha dogo hatimaye amefunguka na kuongelea tetesi hizo.
Pia Soma: Nafasi Yanga wanahitaji kusajili dirisha dogo la usajili
Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema hata kama atatemwa kwenye kikosi cha timu hiyo ana uhakika hatakosa timu ya kuichezea kutokana na uwezo alionao katika kusakata kabumbu
Cannavaro ameiambia Goal yeye ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa hivyo haofii kuachana na timu hiyo ambayo ameichezea kwa misimu 10.
"Sina hofu kwani nina amini bado nina uwezo wa kucheza soka kwa kiwango cha juu kwenye timu yoyote hapa Tanzania na kupata mafanikio," amesema Cannavaro.
Kocha mpya wa Yanga George Lwandamina yupo kwenye mipango ya kukisuka upya kikosi chake kwa kumsajili wachezaji wapya kwenye nafasi za ulinzi kiungo na ushambuliaji huku jina la Cannavaro lilidakwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaotemwa kwenye dirisha dogo.
Cannavaro ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alitangaza pia kungoka katika timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ baada ya kutoridhishwa na mwenendo katika timu ya Taifa hususani ni kitendo kilichofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumteua mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa nahodha bila kumpa taarifa kabla na kingine ni lawama anazopata kutoka kwa mashabiki ambao wanadai yeye ndiye anayeifungisha timu hiyo.
Pia Soma: Wikendi ya Samatta ilivokwenda
Lawama za kwamba anaifungisha timu ziliongezeka baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kuondolewa kwenye mbio za kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 na Algeria baada ya kufungwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Algeria. Baada ya mechi hio kuliibuka maneno kuwa Cannavaro na beki mwenzake Kelvin Yondani wameshuka viwango vyao kutokana na umri wao kuwa mkubwa.
No comments:
Post a Comment