tuwasiliane

Monday, November 21, 2016

Taarifa mpya kutoka uongozi wa Simba SC

Uongozi wa Simba SC kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara, umetoa taarifa kwa wanachama wake kuwajulisha kuhusu mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya kurekebisha katiba yao utakaofanyika December 11, 2016 kwenye bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay .
Mabadiliko hayo ya katiba yatafanyika ikiwa lengo kuu ni kutaka kubadili mfumo wa uendashi wa klabu hiyo kongwe nchini ambapo mwekezaji Mohammed Dewji anataka kununu hisa asilimia 51 kutoka kwenye klabu hiyo.simba-barua

No comments:

Post a Comment