Beki wa kulia wa timu ya PSG Serge Aurier amezuiliwa kuingia nchini Uingereza na mamlaka ya taifa hilo kabla ya mechi ya Jumatano ya klabu bingwa na Arsenal katika uwanja wa Emirates.
Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 23 alipewa kifungo cha miaka miwili kilichoahirishwa mnamo mwezi Septemba kwa kumshambulia afisa wa polisi.
PSG inasema kuwa ilimpa Aurier kibali cha Visa mwezi Oktoba lakini ikakifutilia mbali mnamo terehe 16 mwezi Novemba kufuatia hukumu hiyo.
Mabingwa hao wa Ufaransa wanasema kuwa uamuzi huo ''ni ukosefu wa heshima''.
Lakini katika taarifa ,afisi ya maswala ya ndani nchini Uingereza imesema ''sheria za uhamiaji zinasema kwamba raia wasiotoka Ulaya ambao wamepata hukumu isiozidi miezi 12 katika kipindi cha miaka mitano hawatakubaliwa katika misingi ya kihalifu''.
Aurier amekata rufaa dhidi ya hukumu yake,swala linaloifanya klabu yake kuamini kwamba hana hatia hadi atakapohukumiwa.
No comments:
Post a Comment