tuwasiliane

Saturday, November 19, 2016

AZAM FC YABISHA HODI MBEYA CITY,YAMTAKA JOSEPH MAHUNDI

Image result for joseph mahundi
KLABU ya Azam ipo kwenye mazungumzo na kiungo wa Mbeya City, Joseph Mahundi ambaye amemaliza mkataba na timu hiyo inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri.

Azam leo Jumatano imekutana na mchezaji wao huyo wa zamani kwa ajili ya makubaliano ya mkataba baada ya kuwa mchezaji huru huku Mbeya City wao wakishindwa kufanya naye mazungumzo ya mkataba mpya hadi sasa.

Mtendaji mkuu wa Azam, Saady Kawemba leo ameweka wazi kuwa watasajili wachezaji wawili wazawa ingawa hajawataja majina wao ila tayari kuna habari kwamba mbali na Mahundi pia kuna mazungumzo na Hassan Kabunda wa Mwadui FC.

Meneja wa mchezaji huyo, Herry Mzozo amekiambia chanzo chetu kuwa hawawezi kuendelea kuwasubiri Mbeya City wakati dirisha la usajili limefunguliwa hivyo wamekwenda kusikiliza ofa ya Azam na wakifikia makubaliano basi atasaini mkataba.

"Azam wameonyesha nia tofauti na Mbeya City ambao hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa alipobakiza miezi sita hadi sasa, hivyo tukiwasubiri wao tunaweza kukosa kote maana hawajasema kama wanahitaji huduma yake," alisema Mzozo.

Walipoulizwa Mbeya City, Katibu wao Emmanuel Kimbe alisema kuwa "Mambo ya usajili tutayazungumzia Novemba 30 ila Mahundi hatumuachi,".

Kimbe hakutaka kufafanua zaidi kama wamewahi kufanya mazungumzo ya kumwongeza mkataba huo. Mahundi alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Coastal Union Juni mwaka jana ambapo umemalizika rasmi.


No comments:

Post a Comment